Karibu tena Prof. Mark Mwandosya...!

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Karibu tena baba baada ya kuugua zaidi ya mwaka....

Mungu ni Mkubwa na azidi kuaminiwa na kuabudiwa. Hivi punde, Samuel Sitta ameomba mwongozo wa Spika na kuomba Professor MWandosya ajitambulishe na kusalimia wabunge kwani sasa afya yake imerudi katika yake ya kawaida. Na kweli, kiongozi wetu huyu mpendwa akasimama na kwenda kwenye podium kwa ukakamavu kabisa na kutoa maneno machache ambayo kama kawaida, hufanya ukumbi husika utulie kama maji kwenye mtungi. Professor amewashukuru watanzania wote waliokuwa wanamuombea usiku na mchana, na vile vile Rais, makamu wa rais, na wabunge wa vyama vyote vya siasa. Baada ya kusalimia wabunge na kutoa shukrani zake, Mh Sitta akamuomba Mwandosya amsalimie Zitto kabwe on his way kwenda kuketi, na akafanya hivyo na kumpa mkono Mh. Zitto ambae nae akapata wasaa wa kumsalimia Mwandosya na kumkaribisha kama naibu kiongozi wa kambi ya upinzani.

Sala zetu mwenyezi mungu hakika amezisikiliza kwani ni jana tu tulikuwa tunamzungumzia hapa. Hatukukata tamaa, na faida yake tumeiona sasa. Tulimkosa kwa muda mrefu sana, lakini sasa tunae tena. Sala zetu zisiishie hapa, ziongezeke mara dufu kwani ndizo zitakazomlinda mzalendo wetu huyu na msomi ambae dunia nzima inamtambua na kumheshimu. Hakujatokea kipindi kingine ambacho tuna muhitaji Prof Mwandosya kama kipindi hiki. Najivunia kuwa CCM kwa sababu ya mtu huyu.

Karibu sana Professor Mwandosya, Tupo nyuma yako mpaka pale mwenyezi mungu atakapoamua vinginevyo.
 
Kitendo cha kambi rasmi ya upinzani kupitia zitto kabwe kuungana na bunge kumkaribisha prof.mwandosya ni kitendo cha busara na kama 2kiendelea hivi.hakika 2tafika.naungana nao kumuombea heri mwandosya.
 
Nimemwona Prof akikafagiliwa na Jenista. Mwandosya ameponda sana Pinda kuhusu kilimo kwanza na pia akamponda Lukuvi kuhusu kuomba miongozo. Anasema bila afya njema huwezi kulima wala kuomba miongozo bungezi
 
Hivi alikuwa wapi kumbe? oohh ndio alikua anamalizia kuandika kile kitabu chake ee
 
Ameitumia nafasi vibaya, pamoja na shukrani aliwajibika kuueleza umma kupitia bunge aliugua nini!!!!!! Jambo ambalo hakufanya.
Upuuzi wa kibunge.
 
Kitendo cha kambi rasmi ya upinzani kupitia zitto kabwe kuungana na bunge kumkaribisha prof.mwandosya ni kitendo cha busara na kama 2kiendelea hivi.hakika 2tafika.naungana nao kumuombea heri mwandosya.

Ni kweli VYAMA NI KWENYE NGUO TU,MIOYONI WATANZANIA.
 
Nimemwona Prof akikafagiliwa na Jenista. Mwandosya ameponda sana Pinda kuhusu kilimo kwanza na pia akamponda Lukuvi kuhusu kuomba miongozo. Anasema bila afya njema huwezi kulima wala kuomba miongozo bungezi

Ni kweli afya kwanza ndipo utasoma au kulima!
 
Nimemwona Prof akikafagiliwa na Jenista. Mwandosya ameponda sana Pinda kuhusu kilimo kwanza na pia akamponda Lukuvi kuhusu kuomba miongozo. Anasema bila afya njema huwezi kulima wala kuomba miongozo bungezi

Kama amekuwa fit mbio za uraisi CCM sasa zinogile! Ila aangalie sana, CCM bwana kuna watu ambao si wema kabisa. Pamoja na madudu mengi ya CCM, huyu jamaa ni mojawapo ya watu ninaowaheshimu sana kwamba wako serious katika mambo ya kazi.
 
Ameitumia nafasi vibaya, pamoja na shukrani aliwajibika kuueleza umma kupitia bunge aliugua nini!!!!!! Jambo ambalo hakufanya.
Upuuzi wa kibunge.

Afya(ugonjwa) wa mtu ni siri yake unless aamue mwenyewe!
 
Leo asubuhi kabla ya Waziri wa Uchukuzi kuwasilisha Hoja Za Serikali-Wizara ya Uchukuzi,Mwenyekiti wa Bunge J.Mhagama alimpa mda Prof.Mwandosya kutoa neno ktk Bunge. Prof. Mwandosya amewambia wabunge wasicheze na sekta ya afya,amewakumbusha kuwa kilimo na elimu si lolote kama mtu hana afya njema!amesema wabunge wabunge wasijisahau kuwa kuna maisha baada ya Bunge,ambapo huduma muhimu za afya hazitaghalamiwa na Bunge bali wao wenyewe...hivyo wanapaswa kuipigania huduma na sekta ya afya wakiwa bado Bungeni ili ije iwasaidie baada ya kuwa nje ya Bunge. Ametoa shukrani kwa wabunge wa upinzani kwa kusema kuwa wengi wa walio mpigia simu na kumtakia kheri ni wabunge wa upinzani!!Mwisho amewashukuru Watanzania wote kwa kumtakia kheri,na amesema alipougua amegundua kuwa Wapinzani ni wenye upendo,mana hawakuangalia itikadi yake ktk kumuombea bali Utaifa wake kama Mtanzania
 
Kama amekuwa fit mbio za uraisi CCM sasa zinogile! Ila aangalie sana, CCM bwana kuna watu ambao si wema kabisa. Pamoja na madudu mengi ya CCM, huyu jamaa ni mojawapo ya watu ninaowaheshimu sana kwamba wako serious katika mambo ya kazi.

Hata mim namkubali jamaa,....!MVI NYEUPE mmmh?
 
Back
Top Bottom