Karibu tena Prof. Mark Mwandosya...!

Karibu tena Prof. Mark Mwandosya...!

Afya(ugonjwa) wa mtu ni siri yake unless aamue mwenyewe!

Badili fikra!!! ni wajibu wa jamii kujua kilichomsibu kiongozi wao. Tutakuwa jamii ya watu wapuuzi kabisa kama tutaliacha hili kwenye hiari ya mwandosya.
 
Kama amekuwa fit mbio za uraisi CCM sasa zinogile! Ila aangalie sana, CCM bwana kuna watu ambao si wema kabisa. Pamoja na madudu mengi ya CCM, huyu jamaa ni mojawapo ya watu ninaowaheshimu sana kwamba wako serious katika mambo ya kazi.

"Amekuwa fit" alikuwa anaumwa nini?
 
Kama amekuwa fit mbio za uraisi CCM sasa zinogile! Ila aangalie sana, CCM bwana kuna watu ambao si wema kabisa. Pamoja na madudu mengi ya CCM, huyu jamaa ni mojawapo ya watu ninaowaheshimu sana kwamba wako serious katika mambo ya kazi.

Ni kweli mkuu. Kitendo hiki tu cha yeye kupewa fursa kusimama mbele kinaweza kuwa kimewaharibia wengine siku yao. Sidhani Pinda kama angeweza kuomba huyo fursa
 
''presidential hopeful'' ameshaanza press conference yake?........ndo saa tano hii
 
Prof. Mwandosya amewambia wabunge wasicheze na sekta ya afya,amewakumbusha kuwa kilimo na elimu si lolote kama mtu hana afya njema!amesema wabunge wabunge wasijisahau kuwa kuna maisha baada ya Bunge,ambapo huduma muhimu za afya hazitaghalamiwa na Bunge bali wao wenyewe...hivyo wanapaswa kuipigania huduma na sekta ya afya wakiwa bado Bungeni ili ije iwasaidie baada ya kuwa nje ya Bunge.

Sijui niseme Amen au? Hii ni sala tosha ya kuwaombea wabunge.
 
Mwisho amewashukuru Watanzania wote kwa kumtakia kheri,na amesema alipougua amegundua kuwa Wapinzani ni wenye upendo,mana hawakuangalia itikadi yake ktk kumuombea bali Utaifa wake kama Mtanzania

Katika kumfahamu kwang Mwandosya, siku zote msimamo wake kuhusu wapisani ulinitia shaka sana. Ikiwa imechukua kuugua kwake kuwa na mtazamo kama huu kuhusu wapinzani, basi ninaweza kusema hili ni jambo moja kati ya mengi yaliyo "positive" katika kuumwa kwake. Naweja hata kusema nitakuchukulia kuumwa kwake kama moja wapo ya njia ya kumfanya awe "humble" na mwenye busara zaidi. Nina ukakika kumemfungua macho na kumpa context mpya ya jinsi ya kushughulika na Watanzania wenzake. Kila la kheri Prof katika awamu yako ya pili kwenye dira za siasa. Japo kuumwa siku zote ni kubaya, ninaamini kwa dhati kabisa kuumwa kwako kumekufanya a much better and wiser leader.
 
Kama amekuwa fit mbio za uraisi CCM sasa zinogile! Ila aangalie sana, CCM bwana kuna watu ambao si wema kabisa. Pamoja na madudu mengi ya CCM, huyu jamaa ni mojawapo ya watu ninaowaheshimu sana kwamba wako serious katika mambo ya kazi.

Watamlimbokaaa!!!!
 
Karibu tena baba baada ya kuugua zaidi ya mwaka....

Mungu ni Mkubwa na azidi kuaminiwa na kuabudiwa. Hivi punde, Samuel Sitta ameomba mwongozo wa Spika na kuomba Professor MWandosya ajitambulishe na kusalimia wabunge kwani sasa afya yake imerudi katika yake ya kawaida. Na kweli, kiongozi wetu huyu mpendwa akasimama na kwenda kwenye podium kwa ukakamavu kabisa na kutoa maneno machache ambayo kama kawaida, hufanya ukumbi husika utulie kama maji kwenye mtungi. Professor amewashukuru watanzania wote waliokuwa wanamuombea usiku na mchana, na vile vile Rais, makamu wa rais, na wabunge wa vyama vyote vya siasa. Baada ya kusalimia wabunge na kutoa shukrani zake, Mh Sitta akamuomba Mwandosya amsalimie Zitto kabwe on his way kwenda kuketi, na akafanya hivyo na kumpa mkono Mh. Zitto ambae nae akapata wasaa wa kumsalimia Mwandosya na kumkaribisha kama naibu kiongozi wa kambi ya upinzani.

Sala zetu mwenyezi mungu hakika amezisikiliza kwani ni jana tu tulikuwa tunamzungumzia hapa. Hatukukata tamaa, na faida yake tumeiona sasa. Tulimkosa kwa muda mrefu sana, lakini sasa tunae tena. Sala zetu zisiishie hapa, ziongezeke mara dufu kwani ndizo zitakazomlinda mzalendo wetu huyu na msomi ambae dunia nzima inamtambua na kumheshimu. Hakujatokea kipindi kingine ambacho tuna muhitaji Prof Mwandosya kama kipindi hiki. Najivunia kuwa CCM kwa sababu ya mtu huyu.

Karibu sana Professor Mwandosya, Tupo nyuma yako mpaka pale mwenyezi mungu atakapoamua vinginevyo.

Amen..
 
Karibu tena baba baada ya kuugua zaidi ya mwaka.... Karibu sana Professor Mwandosya, Tupo nyuma yako mpaka pale mwenyezi mungu atakapoamua vinginevyo.

Tupo nyuma yake tunafanya nini? Tunapaswa kuwa naye bega kwa bega tunashirikiana naye kuendeleza nchi yetu!
 
Karibu sana prof.mwandosya mungu akulinde ili ulitumikie taifa lako bado linakuhitaji
 
Kama amekuwa fit mbio za uraisi CCM sasa zinogile! Ila aangalie sana, CCM bwana kuna watu ambao si wema kabisa. Pamoja na madudu mengi ya CCM, huyu jamaa ni mojawapo ya watu ninaowaheshimu sana kwamba wako serious katika mambo ya kazi.

Prof ni mtu makini hana makuu, makundi, siasa chafu, visasi, ni technocrat, mtekelezaji, mzalendo, ana uzoefu, mvumilivu na msikivu..huyu ndiyo Rais JMT inahitaji katika kipindi hiki cha historia yake.
 
Prof kanifurahisha zaidi na nimeamini kwamba ni kweli huwa anamdharau dhaifu (jk), wakati anatoa shukrani hakumtaja dhaifu kama dr! Well done Prof!
 
Back
Top Bottom