Jumbe Kondo
Senior Member
- Oct 18, 2011
- 109
- 68
Lamu ni mji mkubwa katika kisiwa cha Lamu kwenye pwani ya Kenya. Ina wakaazi takribani 10,000. Mji pia ni makao makuu ya Wilaya ya Lamu na Jimbo gatuzi la Lamu.
Mji upo upande wa kaskazini-mashariki mwa kisiwa kando na mkondo unaotenganisha visiwa vya Lamu na Manda. Mkondo huu ni bandari asilia inayohifadhiwa na dhoruba na mawimbi makali ya bahari.
Mji wa Lamu
Lamu lina umbo la kanda ndefu mwambaoni. Mji wa kale umegawiwa kwa mitaa arobaini lakini kuna sehemu mbili hasa - Mkomani upande wa kaskazini penye nyumba kubwa ya mawe na Langoni upande wa kusini ambako wakazi wageni walijenga nyumba za udongo.
Jengo kubwa la mji ni ngome lililioko ufukweni.
Mwambao wa leo umepatikana tu karne ya 19. Mwambao wa kale unaonekana kwa barabara ya Harambee (au: Usita wa Mui). Wakati wa kujenga ngome ufukweni. Enzi za jadi ilikuwa na maji yenye kina kidogo hivyo ikaamuliwa kujaza sehemu hizi na kupanua eneo la mji kuingia ufuoni. Watu wenye uwezo walijenga nyumba zao kubwa na ufuo ukahimarishwa kwa ukuta.