Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 370,974
- 858,957
Wakati wa kazi zinazoendelea sasa za kupanua barabara ya eneo la Darajani, Zanzibar, wakandarasi wamechimba ardhini na kuligundua daraja la zamani lililokuwa limefukiwa kwa miaka mingi.
Chini ya beams za daraja hilo wamekutwa maji meusi yaliyochanganyika na mafuta machafu.
Lakini kabla hatujaanza kugawana vitalu vya mafuta, tukumbuke historia.
Eneo la Darajani zamani lilikuwa mkondo wa bahari uliotenganisha Mji Mkongwe na Ngambo. Ukitaka kwenda Kikwajuni, ilibidi uvuke kwenye daraja hilo ndiyo maana eneo hilo likaitwa Darajani na upande wa pili uliitwa Ngambo .
Wakati wa Serikali ya Sultan Seyyid Khalifa, ilifanyika reclamation ya eneo hilo. Kwa mujibu wa wazee, daraja halikuvunjwa. Lilifukiwa pamoja na mkondo wa bahari kwa kutumia mawe, mchanga na hata takataka za aina mbalimbali.
Leo, wakati barabara inapanuliwa, daraja hilo la zamani limegunduliwa tena.
Chini yake kuna maji machafu yaliyochanganyika na mafuta. Huenda huo ni uchafu unaotokana na takataka zilizotumika kuufukia mkondo huo wa bahari miaka mingi iliyopita.
Lakini kichekesho kikubwa zaidi si daraja wala hayo “mafuta.”
Maafisa wa Manispaa, Ofisi ya Meya na taasisi nyingine walipofika eneo hilo, wakasema kwa mshangao:
“Hatuna kumbukumbu zozote kuhusu daraja hili!”
Kweli?
Eneo linaitwa Darajani, lakini taasisi zetu hazina kumbukumbu ya daraja! Hii ni sawa na kwenda Uwanja wa Ndege halafu kuuliza: “Ndege zilianza lini kufika hapa?”
Badala ya kuwaita wanahistoria, wataalamu wa mambo ya kale na wahandisi kuchunguza ugunduzi huu, hatua ya haraka ikawa
kuweka ulinzi watu wasiibe yale “mafuta”! 😂
Hongereni Zanzibar!
Tumepoteza kumbukumbu za daraja, lakini tumelinda mafuta yake.
Sasa tunasubiri taarifa rasmi:
“Zanzibar yagundua mafuta Darajani; uzalishaji waanza chini ya daraja la Sultan!”
Hili si jambo la kuchekesha pekee. Ni aibu kwa taasisi za umma kutokuwa na kumbukumbu za historia ya eneo maarufu kiasi hiki. Daraja hilo linaweza kuwa sehemu muhimu ya urithi wetu na ushahidi wa namna Stone Town ilivyokuwa imetenganishwa na Ngambo kabla ya kufanyika reclamation.
Tusije tukaliharakia kulifukia tena kabla halijachunguzwa na kuhifadhiwa kihistoria halafu vizazi vijavyo vikaja kuligundua kwa mara ya tatu na kutangaza kuwa vimepata gesi! 😂
Credit: Abuu Shani Ally Saleh Farid Himid Omar Said Shaaban