Karibu chatroom: Uliza chochote kuhusu makaburini, mochwari na wafu

Nimeandika mengi sana kuzihusu hizo nyanja tatu kwenye mada tofauti tofauti na kwa vipindi tofauti.... Kuna maswali niliulizwa na penye ufafanuzi nilifanya hivyo.
Tuchukue muda huu kwa kujisahaulisha mambo ya siasa (yajayo hayafurahishi)... Karibu chatroom tuweze kujuzana na kuelimishana kuhusiana na hizo sekta tatu hapo juu
Nawasilisha....!!!

Jr
Je ni kweli uvutaji wa bangi unazuia kulogwa na wachawi.
 
well, nimeusoma uzi wote....


mshana kuna kitu nimenotice japo sio wote wamekiona... uzi ulipost saa sita kasoro hivi, ukaendelea kuchat na kureply na memba kadhaa walikuwa hewan mda huo mpaka saa nane na dakika kadhaa, walikuwepo memba wengine kama kina humble african bado wanachat.

muda huo saa nane na dkk kadhaa ukapotea ukarudi saa kumi na dkk kadhaa... swali, ulilala?, na hata kama ulilala ulitumia mda mfupi sana maswaa mawili hayakutimia. au kuna kazi ulikuwa unaifanya ? kulingana na story zako za mambo ya giza unatisha aisee, alafu ulishasemaga mida ya saa nane mpaka saa tisa ni mida mibaya sana izrael mtoa roho anakuwepo, ngoja niishie hapa.... nataman uelezee chochote.:(:(:(:(:(:)
Uko vizuri sana... Nakupongeza... Ni kweli kabisa nilipotea hicho kipindi ila niliaga kuwa naenda kuwahudumia wafu... Ilinichukua muda huo uliosinisha.. Muda ambao dunia huwa kimya na falme za kuzimu zikishika hatamu kwa muda....
 
kuna jamaa, juzi tu alitoka mida ya saa nane usiku kwenda msalani kushika adabu zake, lakini amemaliza, ataka kuchukua kopo kujitawaza, akasikia anatawazwa tena utawazwaji wa kibabe..hakuweza kufungua mlango, alitoka nao woote kama ulivyo, uchi..je ni kweli chooni kuna majini? na ni kwanini watu wengi wanaoanguka chooni hufikwa na umauti hukohuko
Tumeshajadili sana hili kwamba chooni ni mlango wa kuzimu na ziraili hutega pia hapo
 
Huko nyuma kuna kesi ilizuka mahakamani ya mtu kumwibia na kumtoa mwenzake uzi kwenye kanga. Ina maana yoyote kwe ulimwengu wa kishirikina. Unaweza kupotezwa maisha kwa hilo??
Ndio uzi wa kwenye nguo ni mojawapo ya malighafi za kutengeneza uchawi wa kudhuru na kuumiza vingine ni kucha, nywele, uzi wa sanda, nknk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom