Kardinali Pengo: Watanzania wa dini zote mniombee

Kardinali Pengo: Watanzania wa dini zote mniombee

Tumlishe kwa sadaka bado tumuombee?
Hiv hawa viongozi wa Dini wamepatwa na nin?
Yesu alilisha watu 5000 samaki 2 na mikate 5 wakala na kusaza

Sasa hiv watu 5000 wanamlisha mtu mmoja bado wanataka tuwambee?

Imani mfu
 
Pengo anapaswa kutubu kwanza tena mbele ya waumini baada ya hapo ndio aombe kuombewa.
 
MWADHAMA Polycarp Kardinali Pengo amewaomba waumini wa dini zote nchini, waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aendelee kuwa mwaminifu katika kutenda kazi ya kumtumikia Mungu.

Kardinali Pengo alitoa ombi hilo jana baada ya kuwaongoza mapadri zaidi ya 150 wa jijini Dar es Salaam kurudia kiapo chao cha upadri. Tukio hilo lilifanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph kwenye misa maalumu, inayowakutanisha mapadri na maaskofu kwa pamoja.

Alisema, anapenda kuendelea kuwatumikia watu kwa nia moja na moyo mmoja kwa muda wote, kwa kuwa ndio kazi ambayo Mungu amleta duniani kuitekeleza.
Hatua ya uovu wa kukandamiza haki za wanyonge kwa kutetea udhalimu ata tukisema tumwombee Mungu hawezi kukubali hayo maombi,hivi mnachukuliaje Mungu ?
robot ?
Pengo atubu kisha apumzike then tutamwombea
 
MWADHAMA Polycarp Kardinali Pengo amewaomba waumini wa dini zote nchini, waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aendelee kuwa mwaminifu katika kutenda kazi ya kumtumikia Mungu.

Kardinali Pengo alitoa ombi hilo jana baada ya kuwaongoza mapadri zaidi ya 150 wa jijini Dar es Salaam kurudia kiapo chao cha upadri. Tukio hilo lilifanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph kwenye misa maalumu, inayowakutanisha mapadri na maaskofu kwa pamoja.

Alisema, anapenda kuendelea kuwatumikia watu kwa nia moja na moyo mmoja kwa muda wote, kwa kuwa ndio kazi ambayo Mungu amleta duniani kuitekeleza.
R I P
 
MWADHAMA Polycarp Kardinali Pengo amewaomba waumini wa dini zote nchini, waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aendelee kuwa mwaminifu katika kutenda kazi ya kumtumikia Mungu.
Naona dhambi za kushiriki kutesa watu anazoshirikishwa na yule mpumbavu anayemlipia matibabu na ulinzi zimeanza kumwelemea!
 
Natazama imani kwa namna ya kichunguzi kabisa, napata ili swali, je ni nani wa kumuombea mwenzake, askofu au muumini?

Pale ambapo Askofu anapoomba aombewe hii inaleta tafsiri gani?uwezo wake wa kuombea umeisha au hana imani ambayo ndiyo msingi wa shughuli yake.

Bwana wetu Yesu Kristo aliwahi kusema ikiwa kama mtakua na imani kama chembe ya aradali mnaweza mkaimbia miti itoke ardhini na ikawatii.

Ikiwa kama askofu ni balozi wa Yesu Kristu anapaswa awe na imani aliyokua nayo bwana wetu Yesu Kristu. YESU HAKUWAHI KUOMBA AOMBEWE ila aliwaombea watu na kuwaondolea madhila yao.

Askofu anayeomba aombewe huyo si askofu tena, nguvu zake zimeisha na imani yake imeisha. Akafanye kazi nyingine.

Povu linaruhusiwa.
Tena Yesu hata alipokuwa akiugulia na hatari ya mateso yaliyokuwa mbele yake alipanda kilimani kumwomba Mungu hata likamtoka jasho la damu, hakuwashangaa wanafunzi wake kutomwombea bali aliwashangaa kuacha kujiombea wenyewe na badala yake wakaishia kulala usingizi!
 
Ndio maana kila mtu sasa hivi analalamika mambo si shwari. Muda mwingi tunawaombea wengine badala ya kujiombea wenyewe
 
Hata ilikiletwa sala kanisani kwetu nitakaa kimya! Apumzike anakoelekea ataharibu wito wake
 
Tafsiri nini hapo, ni kujutia ama kuweka msimamo katika kauli za utatanishi alizozitoa za kupelekea kudharaulika na watu waliokuwa wakimweshimu!!!!!
Huyu ameshaambukizwa na yeye kulia lia ambewe
 
Back
Top Bottom