Kardinali Pengo: Watanzania wa dini zote mniombee

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
MWADHAMA Polycarp Kardinali Pengo amewaomba waumini wa dini zote nchini, waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aendelee kuwa mwaminifu katika kutenda kazi ya kumtumikia Mungu.

Kardinali Pengo alitoa ombi hilo jana baada ya kuwaongoza mapadri zaidi ya 150 wa jijini Dar es Salaam kurudia kiapo chao cha upadri. Tukio hilo lilifanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph kwenye misa maalumu, inayowakutanisha mapadri na maaskofu kwa pamoja.

Alisema, anapenda kuendelea kuwatumikia watu kwa nia moja na moyo mmoja kwa muda wote, kwa kuwa ndio kazi ambayo Mungu amleta duniani kuitekeleza.
 
Mr Pengo kadata.
badala ya yeye kuombea watu, anataka aombewe.
pigo kutoka kwa Mungu hilooo limeanza tartiiibu!!
 
Tatizo ni kwa huyo Mungu maana kda!! tuna myungu wengi kulingana na imani zetu, na kila mtu anajua mungu wa dini yake ndio sahihi, anyway mawazo yangu tu ... aombewe ...why not
 
Natazama imani kwa namna ya kichunguzi kabisa, napata ili swali, je ni nani wa kumuombea mwenzake, askofu au muumini?

Pale ambapo Askofu anapoomba aombewe hii inaleta tafsiri gani?uwezo wake wa kuombea umeisha au hana imani ambayo ndiyo msingi wa shughuli yake.

Bwana wetu Yesu Kristo aliwahi kusema ikiwa kama mtakua na imani kama chembe ya aradali mnaweza mkaimbia miti itoke ardhini na ikawatii.

Ikiwa kama askofu ni balozi wa Yesu Kristu anapaswa awe na imani aliyokua nayo bwana wetu Yesu Kristu. YESU HAKUWAHI KUOMBA AOMBEWE ila aliwaombea watu na kuwaondolea madhila yao.

Askofu anayeomba aombewe huyo si askofu tena, nguvu zake zimeisha na imani yake imeisha. Akafanye kazi nyingine.

Povu linaruhusiwa.
 
Back
Top Bottom