Karasha ya Wachina wafunga milango Singida

Nairobian

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
873
2,277
Karasha ya kokoto ya Wachina hapa Singida hatimaye wamefunga kazi zao Ijumaa iliyopita wakidai kushindwa kutokana na kodi kubwa pamoja na tozo mbali mbali.

Raia hao wa Kichina, waliajiri Watanzania 47 ambao wanarudi mtaani. Tukumbuke karasha ilikuwa inatoa ajira nyingine kwa waendesha malori kwa mamia ambao walikuwa wanakuja kununua kokoto za mashine na pia ikitumiwa na mikoa ya jirani ikiwemo Dodoma, Singida, Tabora etc.
 
Kokoto kwa mujibu wa sheria mpya nadhani nayo ni madini. Sasa hapo tozo zake si mchezo.

Serikali ilipaswa kumfanya mwekezaji/ mfanyabiashara alipe kodi/tozo ya aina moja tu kwa mwaka.

Taasisi za serikali ndipp zigawane hiyo tozo.

Lakini hii tabia ya kila taasisi kugonga mlango wa mwekezaji kudai tozo inachosha.
 
Kwa hivyo ulitaka wasilipe kodi na wapore pesa za nchi yako kwenda kwao kwa kigezo cha ajira ya watu 47 ambao wanalipwa pengine laki na nusu per month? we mnajifikirisha kwanza kabla ya kuropoka.
 
Kokoto kwa mujibu wa sheria mpya nadhani nayo ni madini. Sasa hapo tozo zake si mchezo...
Mambo mengi tunayolalamika humu yangeweza kuishia bungeni Kama tungekuwa na bunge lenye majadiliano mazuri.

Sheria nyingi mbovu zimetungwa bungeni tu kwa sababu wabunge hawakuwa serious kwenye majadiliano
Kokoto kuwa Kama madini ni kichekesho kingine
 
wachina ni rafiki zetuu wasisingizie ivooo labda kuna mengineyoo

nasema ivo kwa sababu serikali ya uchina imetoa msaada kwa ujenzi wa reli ya kisasa na bwawa la kuzalisha umeme
 
Kwa hivyo ulitaka wasilipe kodi na wapore pesa za nchi yako kwenda kwao kwa kigezo cha ajira ya watu 47 ambao wanalipwa pengine laki na nusu per month?muwe mnajifikirisha kwanza kabla ya kuropoka
Swala sio kulipa kodi , swala ni kodi ngapi walitakiwa walipe .na Kama wana uwezo huo

Hakuna mahala serikali inatoa mitaji kwa wafanya biashara , taxi base kubwa inategemea utashi wa wafanyabiashara , hakuna mahala mtanzania analazimika kufanya biashara , ni utashi tu, bunge linapotunga sheria ngumu kuwabana wafanyabiashara ni hatari sana maana matokeo yake ni kama hayo mtu anafunga biashara , na tax base inapungua , utafika mahala serikali itabaiki peke yake na sheria zake na hayupo wa kumdai kodi
 
Back
Top Bottom