Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 4
na Antidius Kalunde (Bukoba) na Salehe Mohamed
JINAMIZI la kashfa ya mkataba tata wa uzalishaji umeme wa Kampuni ya Richmond, bado linaendelea kuwasumbua baadhi ya viongozi, tangu lilipoibuka zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Hali hiyo inajidhihirisha kuwepo kwa tukio la aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kujitetea mbele ya wapigakura wake kuhusiana na sakata hilo, huku Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shelukindo akiishinikiza serikali kuvunja mapema mkataba huo ambazo umelisababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi.
Karamagi ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, akizungumza na wapigakura wake kwa nyakati tofauti juzi, alisema kuwa aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Nishati na Madini Oktoba 16 mwaka 2006 na kwamba mkataba huo ulisainiwa miezi mitano kabla na kuwa alikuta ushauri wa bodi ya wakurugenzi ukiwa umesainiwa Machi 13 mwaka 2006 ukipendekeza Kampuni ya Richomod kupewa zabuni hiyo.
Alisema hata yeye alishangaa maoni ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata hilo chini ya uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe kudai aliwalazimisha kusaini mkataba huo wakati kipindi hicho alikuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko.
Wananchi wangu niliingia kwenye nyumba niliyokuta imeanza kuungua na rais wangu aliniweka angalau niweze kuzima moto, nilijitahidi kumwagia maji ili ipoe, lakini ilishindikana, kwani na mimi nilihusishwa pia kwenye uunguzaji wa nyumba, alisema Karamagi.
Aidha, aliwaeleza wapigakura wake kuwa, maoni ya kamati teule ya bunge iliyodai kuwa yeye alishabikia Kampuni ya Richmond kuuza mkataba kwa Kampuni ya Dowans ni kumsingizia.
Alisema kuwa wakati Richmond inataka kuuza mkataba kwa Dowans, Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) lilikwishagundua kuwa gridi ya taifa ingezimika na kusababisha nchi kuingia gizani kwa kipindi cha wiki mbili kwa sababu ya upungufu wa kina cha maji.
Aliongeza kuwa kipindi hicho yeye alikuwa safarini nchini Canada akiwa ameambatana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kwamba akiwa huko alipokea taarifa kuwa Kampuni ya Richmond ilikuwa imepata mashine tatu zenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawatt 60 zikiwa Afrika Kusini na kwamba walitaka kuziuza kwa Kampuni ya Dowans.
Karamagi alieleza baada ya taarifa hizo aligundua kuwa Kampuni ya Richmond ilikuwa ni kampuni ya kitapeli iliyotaka kuiibia serikali, hivyo alimpigia simu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO akimueleza kutokuwa na imani na kampuni hiyo na kumueleza waziwazi kuhusu utata wa mkataba huo.
Alisema alimuagiza mwenyekiti huyo kufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia wataalam wa kuangalia uwezo wa mashine hizo, ili kuinusuru nchi kutapeliwa.
Alieleza kushangazwa na Kamati ya Bunge kutoa mapendekezo kuwa yeye (Karamagi) alishabikia Kampuni ya Dowans kuuziwa mkataba na Richmond.
Mbunge huyo alisema baada ya maoni hayo ya Kamati ya Bunge na yeye kujiuzulu, amewapelekea Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Rais Kikwete nakala za barua zinazoonyesha wakati mkataba huo unasaniwa yeye alikuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, hivyo kutohusika kabisa katika sakata hilo.
Hivi sasa Bunge limeunda kamati ya kuchunguza madai yetu na ikibanika kuwa Kamati Teule ya Bunge ilinisingizia na kunivunjia heshima, watalazimika kuniomba radhi mbele ya umma.
Wapigakura wangu inabidi muelewe kuwa mlinichagua kuwa mbunge wenu, hamkunichagua kuwa waziri, hivyo mimi ni mbunge halali mpaka mwaka 2010 na hili nalieleza kulinda heshima yangu na chama changu, alisema Karamagi.
Karamagi, Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahimu Msabaha, walitangaza kujiuzulu baada ya Kamati ya Bunge iliyochuguza sakata hilo kuwahusisha katika sakata hilo.
Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wa jimbo hilo, walisema wao kama wapigakura wanasubiri serikali itamke nini kuhusu mbunge wao na wala hawawezi kumhukumu kwa lolote kwa sababu mambo hayo yako nje ya uwezo wao, kwa sababu ndio waliomchagua na kama maelezo yake ni ya kweli, basi wataendelea kumpa nafasi ya kuwatetea bungeni.
Akizungumzia sakata hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shelukindo, alisema serikali kuchelewa kufuta mkataba huo hakuwafanyi wabunge wasahau suala hilo ambalo linaigharimu taifa sh milioni 152 kwa siku.
Alisema kamwe serikali isifikiri dawa ya kusahaulika kwa mkataba wa Dowans kwa wabunge ni kukawia kutoa majibu yake, bali itambue itafika muda mambo yatakuwa magumu zaidi pindi wabunge watakapochachamaa.
Alitoa kauli hiyo alipofunga majumuisho katika semina ya wabunge kuhusu muswada wa sheria za umeme na biashara ya mafuta ya petroli iliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam.
Huu mkataba wa Dowans uvunjwe, kuendelea kuvuta muda hakutatufanya tusahau mkataba huo unaoligharimu taifa fedha nyingi ambazo zingetumika kuboresha Tanesco, alisema Shelukindo.
Alisema hakuna sababu ya kuendelea na mkataba ambao kwanza umeingiwa kimizengwe, pili uwezo wa kampuni husika kuzalisha umeme ni mdogo.
Shelukindo alisema mkataba huo na mingine ndiyo sababu kubwa ya Tanesco kutojiendesha kwa faida, kwani hutoa fedha nyingi kwa kampuni hizo ambazo uwezo wao wa kuzalisha umeme hauridhishi.
Kauli hiyo ya Shelukindo ni msumari mwingine kwa serikali, ambayo imekuja siku chache baada ya wafanyakazi wa Tanesco kuitaka serikali kusimamisha malipo kwa Kampuni ya Dowans kuanzia mwezi huu.
Wafanyakazi hao walisema hawaoni sababu ya kuendeleza malipo kwa kampuni ambayo imerithi mkataba kutoka kwa kampuni hewa ya Richmond.
Source: Tanzania Daima