Kapuya; Nihurumieni jamani

Samahani kwa kusema kuwa Tanzania daima wameonyesha udhaifu sana ktk hili suala.Hapo inaonyesha kuwa ni dhahiri wametakana kumpaka tope Kapuya.
 
Inatungwa na nani habari hii imeandikwa na gazeti la tanzania daima la Leo sasa kama anasinfiziwa si akafungue kesi kapuya ni mti mzima sana haya yanayo andikwa ni kweli mtupu na kama si kweli afungue kesi wakuu
 
Huyu Kapuya atakuwa mjinga kiasi gani kutuma ujumbe kama huu baada ya yote haya?

Kumbe hata huku nako hufikirii ! Huku hakuna kukariri ! ...labda kunamtu ame-swap line ya alhaj au alhaj amechanganyikiwa na kutuma ovyo au anatuma tu kwa makusudi ya kuvuruga upepo , kama wewe unavofikiri sasa.
 
Mawili tu hapo, ama Kapuya anafanya hivi makusudi ili stor ionekane ya uongo kwa watu wenye akili timamu bcoz for sure hutegemei kapuya kufanya upuuzi huu.
Au ni kweli kachanganyikiwa anatapatapa.
 


Binti anaserebuka pembeni ya kapuya . Jicho la kapuya linamuona anamuita wanaanza kuongea

 


Mh? Mbona umetoa mpya hii? Hivi kosa la jinai mtu unaomba msamaha na linaishia? Si wangeshauriwa akina Babu Seya wafanye hivyo? In fact kila mwenye kosa la jinai angefanya hivyo na kusamehewa.
 
Nitakuwa wa mwisho kutoa maoni yangu hadi pale itakapothibitishwa pasipo shaka kuwa tuhuma hizi ni za kweli au uwongo.
 
Sasa naanza kuamini Prof anasingiziwa. kuna mtu anatumia hiyo sim card kumchafua. Lugha gani hiyo ya kihuni hivyo atumie mzee mzima! :frusty:

Ulishakwenda msasani beach club ukaona watu wanavyojibehave??? huwezi amini wazee wa kileo bana
 
Kwa uwelewa wa std seven mtu atapambanua kiurahisi kabisa kwamba mwenye hii laini sio Profesa Kapuya.
Naanza kuutilia shaka uweledi wa hili gazeti la Tanzania Daima!
Nitasikitika zaidi ikijulikana kwamba gazeti hili limeshindwa na gazeti la udaku la uwazi na ijumaa pamoja na risasi katika kuandika habari za ukweli za kiuchunguzi!
 
Najaribu kutafakari lile igizo linaloigizwa na Ze Comedy kwa ule upande wa Le Profesor! Kama ni kweli maprofesa wanakua vile basi sina mashaka na Kapuya! Wewe ogopa profesa kama Kapuya alishawahi kuchukua ndege ya jeshi akabeba mkaa akapeleka kwao wakati ule akiwa waziri wa ulinzi! Chezea Profesa Juma Kapuya?
 
Hii sasa nimeamini inafanana na Report ya Siri toka Makao Makuu ya Chadema.
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…