Prof J. kapuya amejitokeza tena kwa staili ya tofauti ikiwamo kumpigia simu mshtaki wake akiomba wayamalize kiaina.
Akitumia no ilele 0784993039 ambayo awali aliikana, juzi jumamosi alimpigia mshtaki wake na kumwomba wakutane ofisini kwa DPP na aseme kuwa hana haja na kesi.
ujumbe uliotumwa ulisomeka hivi, "Najua kesi ni watu wawili, sasa kwa nini hamkubali? hivi hela nitakayompa akuue si bora nikupe uanze maisha? wakili nimempa hela nyingi, magazeti pia, unaweza kukanusha taarifa hii na kufuta ushahidi halafu mm nikupe hela uende popote, bungeni sifiki na nitafukuzwa nyie mtapata nini? nakupa masaa mpaka saa sita nitakuwa nimeshatuma hela, unachukua paspoti unasepa hakuna kurudi, ukikaidi roho itakwenda kupumzika, unataka kufa kibudu? jiangalie....."
Source; Tanzania Daima Nov 20 13