...na wanawake :love:
duuuh utafanyaje sasa na ni kitu muhimu tena sana as long as ana afya yake kamili.....
...na wanawake :love:
Akafundishe ale angalau laki tano, kazi bongo zipo nyingi n kitendo cha yeye kusota mwaka ni uzembe.Habarini ndugu zangu..nimeombwa ushauri na mimi pia nawaombeni ninyi ushauri...kuna binamu yangu aliyehitimu IFM 2010 fani ya accountancy...baada ya kula msoto wa muda mrefu amepata ajira atakayokuwa analipwa 120,000/- kwa mwezi kwenye kampuni moja ya kihindi..itambidi atoke dar aende morogoro kama eneo lake la kazi...anaomba ushauri wenu wazoefu wa maisha kama hiyo kazi itakuwa na maslahi kwake! asanteni...!
Mkuu kwa ushauri wangu:- kijana akubali offer na aende popote afuate haya :- 1. ajitume 2. awemwaminifu 3. aheshimu wenye mali hayo yote yatazaa yafuatayo EXPERIENCE,PROMOTION,TRUST hapo baadaye kwa mantik zake kazini atapandishwa mshahara na bonus!! Good luck for him.....blessingsHabarini ndugu zangu..nimeombwa ushauri na mimi pia nawaombeni ninyi ushauri...kuna binamu yangu aliyehitimu IFM 2010 fani ya accountancy...baada ya kula msoto wa muda mrefu amepata ajira atakayokuwa analipwa 120,000/- kwa mwezi kwenye kampuni moja ya kihindi..itambidi atoke dar aende morogoro kama eneo lake la kazi...anaomba ushauri wenu wazoefu wa maisha kama hiyo kazi itakuwa na maslahi kwake! asanteni...!
Hapa sio kijiwe cha Saisa,hata kije chama gani kama kichwa buyu ni buyu tu.Msingi ni kujituma
Jamaa we nenda kafanye kazi.
Mshahara huo lazima nyumba atakuwa amepewa kama Staff house.
We nani kakuambia ukiwa msomi usifanye kazi ya kipato kidogo,kama wewe unajiona msomi basi hizo degree siku hizi kama darasa la saba tu zilivyo mjini.
Na ndio mana hawa wenye kujiona wana Elimu ya Chuo wanazurura mjini wakidharau kazi za wenzo,wakati muuza maji wa mjini anaingiza hesabu kuliko yeye.
We muuza maji tu aningiza si chini ya Tsh:5,000 kwa siku wewe ukipishananae tu na vyeti vyako.
-Kwanza Itakusaidi kupata uzoefu na kujuana na watu
-Uaminifu ndio kitu muhim,na pia ndio sehem ya kuonyesha taalum yako.
-Kaa na wafanyakazi wenzako wote vizur bila kubagua,huwezi kujua nani mwema na nani atakuwa kuwa msaada na chanzo cha channel nyingine,ukiiishi vizuri unaweza kukuta mwenzako alietoka hapo na kwenda kwingine akakutafuta ili upate kazi yenye maslahi mazuri.Mwanzo uwe na pakushika kwanza.Wewe mwanaume na muhim ni kujituma na kufanyakazi yoyote halali,hao unaowaona waliofanikiwa wamepitia safari ndefu ila leo tunaona kama wamepata pesa juzi ila siri yao ipo moyoni.
-Pia usijifanye wewe ni msomi au mjuaji,be cool and friendly one to all staffs,hapo utaona njia ya mafanikio.Usifanye tu tamaa ya kutaka utajiri wa mapema wa kupanga wizi,hapo ni kwamba mungu hatokuwa pamoja na wewe.
-Mwisho ni kwamba Mshirikishe mungu katika kila nyendo yako ya maisha ili akupe ustahamilivu,subra na njia.
acha anasa,na kama ni mlevi acha kabisa kitu hicho.
Ni Bora upate kidogo lakini ni chako na chenye Kheir na baraka za Mungu ili mwisho wa maisha pia uwe mwema kwako.
nisameheni ila me nisingeenda. Tena wahindi? Afadhali watu wengne. Mh kama hali ndo hii ngoja niendelee kugangamala na kasaluni kangu kuliko utumwa wa wazi hivi mh.
Duh japokuwa ajira ngumu but 120 jamani, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu, nyumba atalipa kodi bei gani, nauli bei gani, chakula bei gani na mavazi bei gani.