Kanye West alalamika wasanii kuzulumiwa mapato na platforms za Muziki

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
images (5).jpeg

Rapa na muigizaji wa Marekani Kanye West amelalamika kuhusu majukwaa ya kusambaza muziki yanavyotesa wasanii kwa kuwalipa malipo duni kutokana na kazi zao.

Kulingana naye, majukwaa ya muziki yamekuwa yakiwadhulumu wasanii kwa muda mrefu kwa kuwalipa pesa kidogo kutokana na kazi zao za sanaa.

Baadhi ya majukwaa ya kusambaza muziki ni YouTube, Apple, Amazon na Spotify.

Vilevile, alisema wasanii hulipwa asilimia 12 kutokana na kazi zao huku majukwaa hayo yakipokea asilimia kubwa

"Kwa sasa wasanii wanapata asilimia 12 tu, kutokana na kazi zao, wakati umefika kuachana na mfumo huu unaowanyanyasa wasanii, ni wakati wa kuchukua udhibiti na kujenga majukwaa yetu wenyewe,”alisema Kanye West.

Ni majuzi tu msanii wa humu nchini Vivianne alilalamikia kampuni moja ya kusambaza muziki kwa malipo duni kutokana na kazi zao.

Kanye West ameeleza mashabiki wake kuwa amefungua App mpya ambayo atakuwa anapakia muziki wake na kusambaza yeye mwenyewe bila usaidizi wa majukwaa mengine.
 
Huyu jamaa ukiachana na mapungufu yake ni mtu anayefikiria sana ! Kuna siku aliwahi kusema bloggers na makampuni ya entertainment yanatengeneza hela kutokana na picha za wasanii pamoja na maisha yao hivyo wao wakiwa sehemu kubwa ya content huku wakibughuziwa na paparazzi hawafaidiki chochote.
Hivyo akapendekeza kuwe na malipo ya wao kufaidika kutokana na mauzo yanayotokana na contentments zinazotengenezwa.
 
Ndo maana muda wote anapiga mask, ile mask ina tafsiri kubwa nyingi ukiachana na marketing ya products zake za mavazi na viatu
 
Back
Top Bottom