Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Watu Wenye Ulemavu

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20210227_114645_0000.png


KANUNI ZA UTOAJI NA USIMAMIZI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU (MAREKEBISHO) ZA MWAKA 2021

Kufungu 6A (1)

Mtu mwenye ulemavu atakuwa na sifa ya kupata mkopo kama kikundi cha watu wenye ulemavu endapo:

(a) Kamati ya Kudumu ya Fedha, Mipango na Uongozi itajiridhisha kuwa mtu huyo amekosa mtu mwingine mwenye ulemavu na sifa ya kuwa mwanakikundi wa kikundi cha watu wenye ulemavu;

(b) Anajishughulisha na ujasiriamali au anakusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati;

(c) Ana akaunti ya benki iliyofunguliwa kwa jina lake kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kiujasiriamali;

(d) Ni raia wa Tanzania mwenye akili timamu na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea;

(e) Hana ajira rasmi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom