Sagini: Wenye vikundi muandae miradi itayowawezesha kukopa pesa ndefu nawapigia debe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amewataka Wananchi waliopo kwenye Vikundi kuandaa miradi mikubwa itakayowawezesha kukopa kiwango kikubwa cha fedha za Serikali isiyokuwa na riba.
qq.png

q.png
Akizungumza Februari 21, 2024 katika hafla fupi ya kuvunja kikundi cha Amka Mwanamke kilichopo Kitongoji cha Kyamakerya Kijiji cha Nyabange Kata ya Nyankanga Mhe. Sagini amesema mikopo inayotokana na Serikali hususan Serikali za Mitaa inalenga kuwasaidia Wananchi walio kwenye Vikundi wanaoweza kurejesha.

"Lakini twende mbele hivi Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu vinanufaika na mikopo isiyokuwa na riba na tumekubaliana kukopa laki tano au milioni hiyo ni hela ndogo mno hivyo andaeni mradi ambao mkopo mtakaoomba usipungue milioni tano sisi Viongozi tutawaunga mkono"

Pia Mhe. Sagini amesema kuwa mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe lakini mtaji mkubwa kuliko wote ni umoja ambapo wanyonge wakiungana watainuka Kiuchumi kwani Serikali ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira mazuri ya kisera na kisheria yanayoruhusu vikundi kwa kijamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Butiama Ndg. Christopher Siagi, amewataka kina mama kuendelea kukiunga mkono na kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwa sababu mambo makubwa yote yanayofanywa na Mbunge ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Awali akisoma taarifa ya Risala kwa Mgeni Rasmi Katibu wa Kikundi cha Amka Mwanamke Bi. Rhoda Laurian, alieleza kuwa walianzisha umoja huo Machi 10, 2023 ili kuondokana na mikopo ya kausha damu inayorejeshwa kila siku.

Aidha Mwenyekiti wa Kikundi cha Amka Mwanamke Bi. Monica Mirumbe alimshuku Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini kwa kuridhia kuwa mgeni rasmi katika sherehe yao ya kuvunja kikundi na kuwachangia shilingi laki 858000/- pamoja na viti 50 mbali na maneno yaliyosambaa na kuwakatisha tamaa kuwa Mbunge hawezi kufika kwenye sherehe ya kitongoji.
 
Back
Top Bottom