Elections 2010 Kanuni za Uchaguzi 2010 na mgogoro wa Sheria ya Gharama

Status
Not open for further replies.
Ndio maana wabunge walikuwa wanaipinga hii sheria!
 
MMJ,
Njia pekee ya kutibu (redress hiyo situation) ni kwa Serikali kuleta Bunge la April Miscelaneous Amendment.

Hilo linawezekana lakini linawezekana kiasi kwamba CCM wawe wameona matatizo kwenye sheria yenyewe. HOfu yangu ni kuwa wakati mchakato umeanza ndio watu wataona ugumu wa sheria na taratibu zake zilivyo. Hivi Waziri anayeshughulikia masuala haya ndiyo nani?
 
Dr Slaa,
Naheshimu saaana michango yako ktk siasa za nchi na hasa kuelekea kutatua matatizo ya wananchi.

Lakini nahisi kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya muelekeo wako na wa hiki chama Tawala, CCM. Hii inayoitwa serikali ya CCM haina niya njema na inanifanya nitie mashaka kwa kila wanalolifanya. Hili la sheria ya gharama za uchaguzi, Wananchi wanadhani serikali ya CCM ina lengo zuri lakini siamini kama ni hivyo.

Kwa mtiririko wa matukio ya kampeni zilizopita, hisia zangu ni kwamba sheria hii imekuja kwa sababu ya mwenendo wa CHADEMA ktk kampeni. CCM walidhani ni peke yao wenye uwezo wa kuzunguka nchi nzima kwa gari na nyimbo za John Komba. Sasa wamejikuta hata CHADEMA wakiweza kufanya hivyo kwa kutumia helikopa. Ikimaanisha kwamba kama ni misuri sasa hata wengine wanayo.

Kwa ufupi sheria hii imeletwa ili kuwadhibiti wengine wasionyeshe uwezo wao kifedha. Nina maana kwamba sasa ndo tutaona matumizi yasiyolingana ya sheria hii. Usione ajabu CCM wakaendelea kuzidisha hizo gharama na vyama vingine vikijaribu tu, ndo utaona sheria ikitumika. Nahisi hata ndani ya CCM wengine watabanwa na wengine hasa wanaotaka wapite wataachiwa. Kumbuka jinsi wabunge kama akina Chitalilo walivyodanganya viwango vya elimu yao na bado wameachwa kwa miaka 5 ktk ubunge wakati kuna watu walishaenguliwa.

Hii ni kuwazuia wasiotakiwa kutumia pesa na wengine watatumia watakavyo.
 
Dr Slaa , Heshima yako Mkuu!
Kama kweli kuna kifungu kimechomekwa na ushahidi upo basi hiyo sheria ni batili.Swala la msingi si kuongea na spika tu na kuishia hapo bali ni kwenda Mahakama kuu na kuomba kuifuta hiyo sheria kwa msingi wa kwamba kifungu 7(3) HAKIKUJADILIWA BUNGENI hasa ukizingatia bunge ndiyo chombo cha kutunga sheria. sasa imekuwaje kuwe na kipengele ambacho hakikujadiliwa na bunge ndani ya sheria mama na kumpelekea Mh. Rais kusaini kitu batili,je Rais kabla ya kusaini sheria tarajiwa mbali mbali kuwa sheria kamili, pamoja na kuisoma sheria tarajiwa husika Je anapitia Hansard za bunge kujiridhisha kwamba anacho saini ndicho kilichopitishwa na bunge au ndiyo bora twende?
 

I have to admit it.. kurudi kwako kumenichangamsha. Karibu na kokote ulikokuwa umepotolea natumaini wote wazima na mmesalimika!
 
  • Adai mchezo mchafu umefanyika sheria ya uchaguzi
na Irene Mark

KWA mara nyingine, Rais Jakaya Kikwete, amepotoshwa ukweli kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi aliyoisaini hivi karibuni katika Ikulu yake jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kuwa baadhi ya vipengele vimeingizwa kinyemela nje ya Bunge, Tanzania Daima Jumatano, imebaini.

Kipengele kilichoingizwa kinyemela bila kujadiliwa na kupitishwa na Bunge mjini Dodoma, ni kile kinachohusu uthibitishwaji wa wajumbe wanaounda timu za kampeni kwa ajili ya wagombea wa urais, ubunge na udiwani.

Wakati Bunge linajadili na kupitisha sheria ya gharama za uchaguzi, sehemu inayohusu uthibitishaji wa timu za wagombea ilijadiliwa na wabunge wote, lakini haikueleza nani anayepaswa kukagua timu za kampeni za wagombea wa nafasi mbalimbali, lakini katika sheria aliyosaini rais, inafafanua watu wanaostahili kukagua timu za kampeni.

Kwa mujibu wa sheria iliyosainiwa kwa mbwembwe na Rais Kikwete, kipengele kinachodaiwa kuchomekwa bila ridhaa ya Bunge, kinaonyesha kuwa timu za kampeni za wagombea urais, zitathibitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, timu za kampeni za wagombea ubunge, zitathibitishwa na Makatibu Tawala wa Wilaya wakati timu za kampeni za wagombea wa udiwani, zitakaguliwa na kuthibitishwa na Makatibu Tarafa.

Akizungumzia utata wa sheria hiyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, alisema anashangazwa na kilichotokea Ikulu siku ya kusaini mkataba huo, huku akitaka kujua nani aliyehusika kuongeza vipengere hivyo bila idhini ya Bunge.

Dk. Slaa alitoa ufafanuzi wa kasoro hiyo jana wakati wa semina ya kujadili kanuni zinazofafanua Sheria ya Gharama za Uchaguzi, iliyoandaliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa.

Dk. Slaa, ambaye pia ni Mbunge wa Karatu, alionyesha kitabu cha kumbukumbu za Bunge ‘Hansard’ ambacho haikuonyesha viongozi wanaopaswa kufanya uhakiki wa timu za kampeni za wagombea.

“Katika sheria aliyosaini rais kuna kifungu cha 7 (3), ambacho hakikuwepo kabisa kwenye muswada uliojadiliwa na kupitishwa bungeni. Kwa kweli nimeshangazwa sana kwa sababu rais amedanganywa katika hili.

“Bungeni hatukusema nani anatakiwa kukagua timu ya kampeni ya nani, lakini kwenye kipengele ambacho kimo kwenye sheria iliyosainiwa na rais inaonyesha kwamba timu za kampeni za mgombea urais zinatakiwa kuhakikiwa na Msajili.

“Timu za kampeni za mgombea ubunge, zinaonyesha zinapaswa kuhakikiwa na Makatibu Tawala wa Wilaya na kwa kesi ya wagombea udiwani, timu zao kampeni zinapaswa kukaguliwa na Makatibu Tarafa,” nani kaichomeka hii?” alihoji Dk. Slaa, huku wajumbe wengi wakipigwa na butwaa.

Alisema, haiwezekani timu za kampeni ambazo ndiyo kikosi cha ushindi cha mgombea yeyote, kukaguliwa na mtu wa nje ya chama chake, hususan anayetoka chama tawala, yaani Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katibu huyo wa CHADEMA ambaye alikuwa mbogo wakati wa kujadili utata huo wa sheria hiyo, alisema kuna mchezo mchafu uliofanyika kwa lengo la kufifisha kambi ya upinzani nchini.

Dk. Slaa alifafanua kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa ni nafasi ya kuteuliwa na rais, hivyo kambi ya upinzani haitakuwa na imani kwa timu zake za kampeni za mgombea wao wa urais, zikaguliwe na mtu huyo.

Alisema si sahihi pia kwa Makatibu Tawala wa Wilaya au Makatibu Tarafa, kuzikagua timu za kampeni ya wagombea ubunge ama madiwani kwa vyama vya upinzani kwa kuwa watendaji hao ni makada wa CCM, hivyo haki haitatendeka.

“Hawa wenzetu wana mbinu nyingi hasa za kuwanunua wafuasi wa upinzani, hivyo kesho nikikubali timu yangu ya kampeni ikaguliwe na DAS (Katibu Tawala wa Wialaya), ni rahisi kwake kuniingizia mamluki...

“Unatakiwa kujua kwamba timu ya kampeni, ndiyo yenye mbinu zote za ushindi hivyo yanaweza kutokea kama yaliyonitokea mimi mwaka 2005, ambapo mmoja wa watu wangu wa kampeni aliyekuwa anaingia kwenye vikao vya siri alirubuniwa na CCM akanikimbia wakati tunakaribia uchaguzi,” alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa alisema kwa mchezo mchafu huo uliofanywa na serikali, anakusudia kuchukua hatua za kisheria ili kumbaini aliyeingiza kipengele hicho kinachofinya uhai wa demokrasia kwa vyama vya upinzani nchini.

Machi 17 mwaka huu, taifa liliandika historia pale wabunge, wawakilishi wa vyama vya siasa, mabalozi, viongozi wa dini na wasomi mbalimbali walipokutana Ikulu ya Dar es Salaam kushuhudia utiwaji saini wa sheria ya gharama za uchaguzi uliofanywa na Rais Kikwete. Sheria hiyo itaanza kutumika kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, kifungu kidogo cha pili, kinaeleza maana ya timu ya kampeni kuwa ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa zoezi la uteuzi lenye madhumuni ya kumwakilisha au kumsaidia mgombea kwenye kampeni za uchaguzi ambaye amepitishwa kuwania.

“(a) Kwa kesi ya urais watathibitishwa na Msajili, (b) Kwa kesi ya Mbunge watathibishwa na Katibu Tawala wa Wilaya na (c) Kwa kesi ya Diwani watathibitishwa na Katibu Tarafa...,” ilieleza sehemu ya sheria hiyo iliyosainiwa na Rais Kikwete ambayo nakala yake tunayo.

Muswaada huo wa sheria ulioasisiwa na Rais Kikwete mwenyewe, ulipitishwa kwa mbinde Februali 12 mjini Dodoma huku ukiibua malumbano makubwa baina ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, pamoja na wabunge wengine kuhusu vipengele mbalimbali vya muswada huo.

Mwanasheria Mkuu wa serikali alipingana waziwazi na Chenge aliyekuwa mwanasheria mkuu wa zamani hali iliyomlazimu Naibu Spika kuingilia kati mara kwa mara.

Muswada huo ulimlazimisha Mwanasheria wa Serikali kusimama kwa zaidi ya mara 11 kwa ajili ya kutoa ufafanuzi huku akitahadharisha kuwa yeye ni jaji, hivyo kuwataka wabunge kuwa watulivu baada ya kubaini kuwa baadhi yao walikuwa wakizungumza kwa sauti za juu wakati mwanasheria huyo aliposimama.

Wanasheria hao pamoja na wengine walikuwa wakibishania kifungu cha saba ambacho hakikuwa na ufafanuzi kuhusu gharama za watu wanaosaidia katika kampeni ambapo Chenge alitaka baadhi ya mambo yaongezwe ili kupanua wigo kwa wapiga kampeni hao katika kugharamiwa baadhi ya mambo ikiwemo chakula na malazi.

Chenge alitaka kifungu hicho kiwekwe kwani kwa mtazamo wake ni halali kwa mgombea kuwalisha na kuwagharamia watu ambao wanamsaidia katika kampeni jambo lililotafsiriwa vibaya na baadhi ya wabunge. Wabunge wengine ambao walikuwa moto na muswada huo ni pamoja na Halima Mdee, Dk Slaa, na Peter Serukamba.


The blue bolded statement from mzee wa vijisent worries me if he is real a lawyer if he knows the meaning of corruption.
 
Dr Slaa, ubarikiwe. Tanzania ya leo na kesho inakuhitaji mno.
 
a) Kwa kesi ya urais watathibitishwa na Msajili, (b) Kwa kesi ya Mbunge watathibishwa na Katibu Tawala wa Wilaya na (c) Kwa kesi ya Diwani watathibitishwa na Katibu Tarafa...," ilieleza sehemu ya sheria hiyo iliyosainiwa na Rais Kikwete
bado naishangaa nguvu ya serikali katika utungaji wa sheria ambazo zimepitishwa na bunge, naungana na Slaa kushangaa namna watawala wanavyolipuuza Bunge kwa kuingiza vitu vyao nnje ya sheria iliyopitishwa na Bunge.
 
NINYI WATU,
hakukuwa na sababu ya ku-paste magazeti wakati muhusika mwenyewe alianzia humu kulielezea hilo swala.i mean,hata aliyeandika hilo gazeti ametoa humu humu jf!
 
Nampenda sana Dk.Slaa, anajituma, anasoma sana na kutufundisha alichosoma bila kudai malipo. Nampenda sana kwa anafanya tafiti kabla hajasema! Kwa kweli anatujuza Watanzania madudu yanayofanyika nyuma ya Pazia hasa anapokuwa bungeni.

Haka ka mchezo kaliko fanyika ka kuchomekea kanadhihirisha kuwa the whole process has a hidden agenda! Kwa nini in the first place mswaada huo ulikuwa wa kulazimisha lazimisha vile? Kwa nini ulisainiwa kwa mbwembwe kubwa kinyume na miswada yote iliyopita tangu tupate uhuru?

Tutayaona mengi mwaka huu!
 
Huu ni Mkuki kwa Upinzani na uvunjaji wa Sheria za nchi (Kama hii ni kweli basi Sasa ikulu inatunga sheria), Sasa ngoja tusikie Mweshimiwa Six(6) Mzee wa Standard na Speed anasemaje kuhusu hili? Na kama ni kweli nani awajibishwe? Nashauri kama ni kweli basi wapinzani wakimbilie mahakamani haraka sana.
 
inawezekana kile ki babu kinachoitwa philip malmo, naona kina powers za ajabu siku hizi
 
Umefika wakati sasa CCM na serikali yao waache kufanya mambo kwa mazoea na pia wakumbuke kwamba pamoja na hii michezo michafu wanayocheza hawatakuwepo madarakani milele hivyo wanapaswa kuwa fair ili kamba wanazozitayarisha zije ziwanusuru na wao pia.

Uchunguzi wa kina ufanyike na yeyote aliyehusika na uhuni huu ana kesi ya kujibu mahakamani, huwezi kuwa unacheza na sheria za nchi halafu ukategemea tunaendelea kukuchekea. We have to be serious on this.

I support Dr Slaa, to me he is a real Tanzanian.
 
2: Kifungu cha 5(2) Kinatamka kuwa "….. the nominating organ shall be …(b) in the case of a Member of Parliament, the members of the Political Party within the District…and (c) in the case of a Councilor, the members of the political party within the ward…"
Kifungu cha 6(2) kinaweka "Regional Women organ" kuwa chombo cha kufanya Short listing ya Wagombea wa viti maalum.

Huu ni uCCM ndani ya kanuni. Hivi huyu anayetunga kanuni hizi anajua anachokifanya au anafikiri Watanzania wote ni wajinga? Kama ni waziri, basi ni wazi hafai kabisa!
Hili lingine la kumsainisha Rais sheria ambayo haijapitishwa bungeni, ni la hatari sana. Kama vipengele fulani vya sheria vilichomekwa baada ya bunge kupitisha, ni wazi, alichosaini Rais sicho kilichopitishwa na Bunge; na hivyo alichosaini Rais ni batili!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…