Boramaisha
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 820
- 18
Mie nashangaa inakuwaje watu wale wale (wasio na udhu) waliotumia fedha chafu katika uchaguzi uliopita leo hii hata bila soni wanatia sahihi mkataba huo kwa mbwembwe bila hata kuwaomba wananchi radhi kwa vitendo viovu walivyofanya katika uchaguzi uliopita. Kama kweli CCM na Serikali yake wana nia njema na hiyo sheria mpya ya uchaguzi, jambo ambalo wangelipaswa kufanya ni kutamka wazi kabisa kwamba Sisi CCM tuliwakosea wananchi katika uchaguzi uliopita kwa kutumia fedha nyingi chafu na safi ili tupate uongozi. Kwa dhambi hiyo tuliyoifanya, tunaomba radhi sana na tunatarajia wananchi watatusamehe ili tuweze kuanza ukrasa mpya.
Nina uhakika wapo Watanzania waliosonya kwa hasira kuona mbwembwe zisizo za lazima katika utiaji sahihi wa sheria hiyo.
Nina uhakika wapo Watanzania waliosonya kwa hasira kuona mbwembwe zisizo za lazima katika utiaji sahihi wa sheria hiyo.