Kama sehemu hii haikujadiliwa na bunge kwa hiyo rais alisaini kwa mbwembwe kitu ambacho hana uhakika nacho kwa lugha nyepesi alisaini kanyaboya blank cheque(a) Kwa kesi ya urais watathibitishwa na Msajili, (b) Kwa kesi ya Mbunge watathibishwa na Katibu Tawala wa Wilaya na (c) Kwa kesi ya Diwani watathibitishwa na Katibu Tarafa..., ilieleza sehemu ya sheria hiyo iliyosainiwa na Rais Kikwete ambayo nakala yake tunayo.
2: Hili lingine la kumsainisha Rais sheria ambayo haijapitishwa bungeni, ni la hatari sana. Kama vipengele fulani vya sheria vilichomekwa baada ya bunge kupitisha, ni wazi, alichosaini Rais sicho kilichopitishwa na Bunge; na hivyo alichosaini Rais ni batili!
That is why he wanted it to be part of the law so that cannot be construed as corruption!!! he is a clever chap!! But if people part of your campaign team they should be hospitalised or taken care by the campaign fund and not their own money as that will even be a dangerous situation as you have to find ways of paying back them after the elections!!!The blue bolded statement from mzee wa vijisent worries me if he is real a lawyer if he knows the meaning of corruption.
Kikwete siyo maamuma asaini asichokijua.
anajua alichosaini ndo maana akasaini kwa mbwembwe. hiyo ishu ya kudanganywa naiweka pembeni. atakuwa anajua kilichoongezwa offtrack.
Songambele kuna maoni ya kawaida hasa kwenye kanuni ambazo tunajua kila mtu anatoa ili kuboresha utekelezaji wa hiyo sheria hili la kuchomekwa kitu ambacho hakikuwepo sidhani kama liko kwenye sehemu ya maoni ni sehemu ya sheria mama ninachojua mimi sheria ilishapitishwa na bunge kwa hiyo hili la kuchomekwa vipengele haliwezi kutatuliwa na mkutano wa kujadili kanuni litatatuliwa na walioitunga hiyo sheria ambalo ni bunge zimaWajuvi wanasikiliza pande mbili kabla ya kufikia conclusion, Silaha kasema hivyo sasa tusubiri upande mwingine lakini tukirejea historia na utaratibu mzima wa maaumizi hapa bongo hilo tayari limepita labda kama kuleta utata usio na tija kama kawaida yetu.
Ukisoma between lines kama mwaandishi ametia chumvi zaidi na kufanya watu wote kuwa makomongo (vichwa maji) isipokuwa Dr. Slaa. Kitu ambacho sio kweli labda kama mwandishi wa Tanzania Daima tutaelewa anamaanisha nini. Wadau wameitwa watoe maoni manake nia ya serikali ni nzuri na kama Dr. katoa maoni poa. Cheyo katoa maoni yake na Lipumba pia katoa.
huu ni mkuki kwa upinzani na uvunjaji wa sheria za nchi (kama hii ni kweli basi sasa ikulu inatunga sheria), sasa ngoja tusikie mweshimiwa six(6) mzee wa standard na speed anasemaje kuhusu hili? Na kama ni kweli nani awajibishwe? nashauri kama ni kweli basi wapinzani wakimbilie mahakamani haraka sana.
Hata kabla ya kuchomekwa hivyo vipengele vinavyolalamikiwa, sidhani kama huu muswada ulikuwa wa kushangiliwa na wapinzani kama wanavyoonekana wamejipanga kwenye picha. Wangeweza ku-protest hata walau kwa kususia mwaliko wa kushuhudia utiaji saini muswada huo. Bado nashindwa kuamini kama hawahawa kina Slaa wanaolia leo ndio walimtuma Komu kuwakilisha chama kwenye utiaji saini muswada huo!