Kanuni za Uchaguzi 2010 na mgogoro wa Sheria ya Gharama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanuni za Uchaguzi 2010 na mgogoro wa Sheria ya Gharama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dr Willibrod Slaa, Mar 21, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #1
  Mar 21, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Wanajamii Forums,

  Natumaini hamjambo. Nilikuwa napitia Kanuni za ku operationalize Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ( Elections Expenses Act, 2010), No. 4 of 2010 REGULATIONS, (made under section 31 ).ambazo kwa bahati mbaya sinayo Electronically. Iwapo kuna mtu anazo nitaomba aziweke hapa. Hata hivyo, nimeona kuna matatizo makubwa na vipengele kadhaa. Ni imani yangu kwa kuzijadili tunaweza kutoa mchango mkubwa kwa Wahusika. Ifuatayo ni analysis yangu. Nawashukuru sana.

  DR.WILLIBROD PETER SLAA (MP)
  The Office of the Member of Parliament,
  KARATU CONSTITUENCY
  P.O BOX 119, KARATU,
  TEL. (027) 2534247(Karatu)

  + 255-22-2460 485( DAR)
  FAX:+255-22-266 8866
  Mobile: +255-784-666995

  E-Mail: slaa@chadema.or.tz
  Web: www.chadema.or.tz


  Our Ref Bass/01/01/2…….

  Your Ref………………………  RE: ELECTION EXPENSES ACT (2010):

  REGULATIONS (GN No……..);

  1: Utangulizi:

  Pamoja na kuwa Watu wengi, wakiwemo wana Siasa wa vyama vya Siasa walikuwa wakipenda sana itungwe Sheria kudhibiti matendo ya Rushwa katika uchaguzi, lakini nia hiyo njema hata siku mmoja haikulenga itungwe "Sheria mbaya". Sheria ya Gharama ya uchaguzi pamoja na kuwa imekarabatiwa sana, bado ina maeneo mengi tu ambayo bado yanaweza kutumika vibaya na bado yakazalisha matendo ya Rushwa, na wakati huo huo ina nia ya kudhibiti vya Upinzani.

  Kanuni zinazotungwa kutokana na Sheria hiyo bado ina vipengele ambavyo vina madhara sana. Mifano ya Vipengele hivyo vibovu ni kama ifuatavyo:


  1: Kifungu cha 4(1) Kinamtaka "Mgombea wa nafasi ya Urais, Ubunge au Udiwani "…. Shall make an application..". Kifungu hicho kinaleta jambo ambalo halizingatii matakwa ya ya vyama. Mathalan Katiba ya Chadema inamtaka Mgombea yeyote kati ya waliotajwa " kujaza Fomu.." Kujaza Fomu na kufanya "Application" bila kufafanua muundo wa "Application" hiyo kutaleta mgongano. Application ya kawaida inatakiwa iwe katika umbo la Barua. Kwa uzoefu wa nyuma, wagombea wengi watakataliwa na Wasimamizi wasaidizi kwa kutokufanya "Application" hata kama wamejaza Fomu. Kanuni zozote zinazotungwa ni lazima itoe nafasi kwa taratibu mbalimbali zilizowekwa na Katiba za Vyama. Takwa hili la Kanuni:-


  a) Kanuni zinazotungwa leo hazitakiwi kwenda kinyume na Katiba ya Vyama kwa vile siyo utawala bora kutunga Sheria/Kanuni isiyo zingatia mazingira yaliyokwisha kubaliwa. Isitoshe, kati ya sasa na utekelezaji wa Kanuni hizo vyama havina tena nafasi ya kurekebisha Katiba zao.

  b) Kufanya "application", yaani kupeleka maombi ambayo yanatakiwa kuzingatia masharti yaliyoko katika Kanuni ya 4(2) (a-g) ina maana ya kuwa iwapo sharti lolote halikutimizwa basi mfanya "application" anaweza kukataliwa ndiyo maana Kanuni inatumia "shall" badala ya "may" ambayo pia ingeliruhusu vyama kutumia njia mbalimbali za wagombea kuomba kuomba nafasi hizo kwa mujibu wa Katiba zao. Kifungu cha 4(3) kinatamka wazi kuwa "Katibu Mkuu hatapokea Maombi ..(shall not accept) ambayo hayatimizi masharti yaliyowekwa katika kifungu cha 4(2)(a-g) yaani Jina na anuani, umri, jinsia, kazi, elimu, uraia, na jina la Chama. Kimsingi kumnyima mtu haki ya kugombea kwa sababu ya kutokuandika umri, jinsia, kazi, elimu ni kuweka masharti yanayoenda kinyume na Katiba. Kanuni haziwezi kuweka masharti ambayo yanaenda kinyume na Katiba ya nchi. Haina maana ya kuwa taarifa hizo siyo muhimu. Lakini ni mambo yanayosahihishika tu, na badala ya Katibu Mkuu kumnyima haki mgombea aliyesahau kuandika mambo hayo ampe nafasi ya kusahihisha. Kanuni ziepuke jambo lolote linaloweza kutafsiriwa vibaya wakati wa utekelezaji.

  c) Kwa maoni yangu, badala ya "shall make an application" itamke " shall make an application in the manner provided for in the constitution of his party respective party". Kwa mfumo huo Katiba za vyama zitakuwa zimeheshimiwa pia, Katiba ya nchi imeheshimiwa, na hapatakuwa na tafsiri potofu kwa yeyote anayetaka tu kupotosha kama ilivyotokea huko nyuma.

  2: Kifungu cha 5(2) Kinatamka kuwa "….. the nominating organ shall be …(b) in the case of a Member of Parliament, the members of the Political Party within the District…and (c) in the case of a Councilor, the members of the political party within the ward…" Hapa:-


  a) Ni dhahiri kabisa, Kanuni zinataka kushinikiza kwa vyama vingine utaratibu wa CCM bila kujali masharti na taratibu zilizoko kwenye Katiba ya Vyama hivyo. CCM inajulikana kuwa kwa zaidi ya miaka mitano imekuwa ikiandaa utaratibu huu. Kimsingi imekuwa na muda wa kutosha kuandaa Katiba yake kuendana na utaratibu huu, na hata Kamati maalum iliundwa kwa lengo hili. Si haki, kuhamisha utaratibu huu kwa vyama vyote, bila navyo kupewa muda wa kutosha kujiandaa na kurekebisha Katiba yake. Hapa ni dhahiri kuwa lengo la Kanuni hii si nzuri, bali kudhibiti vyama vya Upinzani.

  b) Itakapotokea kuwa Vyama vya Upinzani havijafuata utaratibu huu, ambao ni wa CCM itakuwa kigezo kubatilisha na au kuwawekea pingamizi wagombea wa Upinzani. Kifungu cha 5(5) kinatoa msingi wa disqualification hiyo pale kinaposema, "where the registrar asks a political party that an applicant has during the nomination process committed an act which renders that applicant liable for disqualification from participating in the election, a political party concerned may opt to nominate another applicant. Kifungu hiki ni dhahiri hakina nia njema hasa kwa vyama vya upinzani. Vyama vingi Katiba zao havina kipengele cha kura ya awali kwa wananchi wote katika Wilaya, au katika Kata. Pili vyama vingi vya Upinzani havina uwezo wa kifedha, na hasa ikizingatiwa kuwa havijajiandaa kwa zoezi hili wakati CCM walikuwa walikuwa wamejiandaa kwa muda mrefu kama nilivyosema hapo juu. Hivyo, yeyote ambaye hataweza kutimiza sharti hili ataondolewa. Ikumbukwe kuwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tulipoteza nafasi zaidi ya 20,000 kutokana na kifungu kibovu cha "mwongozo" kama hiki. Kifungu hiki hakikubaliki kabisa kwani havitendei haki vyama vya upinzani. Iwapo kipengele hiki kitaruhusiwa kupita, Wagombea wengi sana wa upinzani wataondolewa kwa pingamizi inayozungumziwa katika kipengele cha 5(5) na vyama havitakuwa na nafasi wala uwezo wa kuweka wagombea wengine.

  c) Serikali inayofuata utawala wa Sheria, inapaswa kulinda Katiba za Vyama zinatekelezwa na siyo kuvifanya vyama vivunje Katiba zao wenyewe kutokana na maelekezo ya Serikali. Kanuni hii inaenda kinyume na Katiba ya Jamhuri inayotoa mamlaka kwa vyama vya Siasa kujiendesha kwa utaratibu wanaojipangia alimradi hauendi kinyume na sheria iliyoko. Katiba za vyama ziko tayari muda mrefu, hivyo kwa utaratibu wa kawaida wa Sheria, Kanuni hizi hazipaswi pia kuwa Retrospective, kwa maana ya kuathiri katiba zilizoko za vyama.

  d) Kifungu cha 5(5) kinaenda kinyume na principles of Natural Justice na Katiba Jamhuri ya Muungano, kwa kutokutoa "Right to be heard", yaani "mgombea kuondolewa bila kusikilizwa" nah ii ni kinyume kabisa na Spirit ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi kama ilivyopitishwa na Bunge. Kanuni haziwezi kuwa na masharti au vipengele vigumu zaidi kuliko sheria yenyewe.

  3: Kifungu cha 6 nacho kina matatizo. Kimsingi Kanuni zinapaswa kuzingatia katiba za Vyama kwa kadiri inavyowezekana. Pale ambako kuna vacuum ndiyo Kanuni hizi zitumike. Kanuni zisifunge vyama kutumia Katiba zao, bali pale ambapo hakuna utaratibu ndio Kanuni ziweke utaratibu wa kiserikali. Kwa mfano siyo kila chama kina District Party Secretary of the women organ. Serikali isifike mahali ikalazimisha vyeo vya CCM kwa vyama vya vingine na wala visilazimishe vyama kuiga mfano wa CCM bila utashi wao jambo ambalo haiwezekani kwa kuwa vyama vina historia tofauti, viwango vinavyotofautiana vya rasilimali na kadhalika. Pamoja na maelezo haya:-


  a)Kifungu cha 6(2) kinaweka "Regional Women organ" kuwa chombo cha kufanya Short listing ya Wagombea wa viti maalum. Si kila chama kina Regional Women organ. Mathalan, katika ngazi ya Mkoa Chadema haina Regional Women Organ. Mkoa kwa Chadema ni chombo cha Uratibu tu, Tazama Katiba ya Chadema, Toleo la 2007, na "Mwongozo wa Mabaraza ya Chadema," (ambayo ndiyo katiba ya Mabaraza hayo). Kwa mfano kwa Chadema uteuzi wa awali unafanywa na Mkutano Mkuu wa Wilaya Wanawake,, na uteuzi kufanywa na Halmashauri Kuu ya Taifa wanawake kabla ya kuthibitishwa na Kamati Kuu ya Chama. Kifungu cha 6 cha Kanuni kinavunja kabisa utaratibu huo wa kikatiba ndani ya chama.

  4: Kifungu cha 7 cha Kanuni kinatunga Forms mbalimbali zitakazotumika katika Uchaguzi huo. Hata hivyo:-


  a) Kifungu cha 7(3) ( a) hakitekelezeki. Kifungu hiki kinazungumzia "Projected amount and sources of funds" Kama kingeliishia hapo hakuna tatizo. Lakini (b) inazungumzia " ….. date or period during which the funds are expected to be received.." Kwa ccm inawezekana tarehe na kipindi kikajulikana. Hali si hivyo kwa vyama vya upinzani, kwa kuwa Vyama vya Upinzani havina uwezo wa kulazimisha watu kufanya fund raising kama ilivyo kwa ccm. Hivyo, swala la tarehe liachiwe kuwa katika "Taarifa ya mwisho" baada ya uchaguzi ambayo itaonyesha lini fedha zimepokelewa na kutoka kwa nani. Lakini katika projection siyo realistic kuweka takwa hilo ambalo linaweza kutumika kama ukiukwaji wa Kanuni na likalazimisha mtu kuondolewa katika kugombea. Hivyo Form EE1 isiwe na hitaji la jina la mtoa fedha na wala Tarehe. Itakuwa mwujiza kujua zaidi ya miezi 3 kabla kujua nani atakuchangia mafuta, gari ( matumizi ya gari lake). We have to be realistic. Tusitunge sheria/Kanuni ambayo itawaondoa kwenye kugombea au itawapeleka watu mahakamani . Hivyo Fom EE1 iandaliwe upya kabisa kama nia ni njema.

  b) Kifungu cha 8 kinachoanzisha Form EE2 nacho kinahitaji kufanyiwa kazi upya kama ilivyo kwa ( a) hapo juu, vinginevyo nayo haitekelezeki kwa vyama vingi.` Nayo pia iandikwe upya na Taarifa ya Nani katoa fedha, na tarehe iwe katika taarifa ya mwisho ya Chama. Lengo la Kanuni ni kudhibiti vitendo vya Rushwa, na haina maana kuweka taarifa ambazo hazitasaidia, chama, mgombea wala Taifa katika kudhibiti vitendo vya Rushwa. Form hii ikiachwa hivi ilivyo ni un realistic na haitekelezeki. Form iwe tu na Projections za Fedha ambazo Chama inatememea kupata iwe ni mkopo, msaada na kadhalika. Lakini siyo jina la nani atatoa au kiasi kwa mtu au tarehe ya kutoa. Hata deni lako mwenyewe una uhakika wa siku ya kupewa sembuse mchango unaotegemea kwa mtu. Itakuwa maajabu. Sheria isiyotekelezeka ni kichekesho.

  5: Kifungu cha 9 (2) siyo realistic kumtaka mgombea hasa wa Kata kupeleka nakala ya copy ya Disclosure siyo chini ya siku 5 kabla ya Nomination day ni un realistic. Kata ngapi zitakuwa na Posta( maeneo mengi kwenda kwenye mji wenye posta ni safari ya siku nzima ni kipindi hiki muhimu mgombea anahitaji kutumia muda wake kwa mambo muhimu ya kugombea kuliko legal requirements ambazo hazina tija katika kushinda uchaguzi. Katika kifungu cha 9(3) kinachoweka Form EE4 nayo haina maana. Mikopo inaweza kuendelea hadi siku mmoja kabla ya uchaguzi alimradi inakuwa ndani ya kiwango cha fedha kilichotangazwa kutumika na chama. Vivyo hivyo majina ya watoa mikopo, misaada au na "zawadi" nayo ni vema yaonekane kwenye taarifa ya mwisho badala ya kuonekana kabla ya Nomination Day ambayo ni siku zisizopungua takriban 90 kabla ya uchaguzi. Hilo linawezekana tu kwa chama ambacho kilijua kuwa Regulation hii inakuja na hivyo imekwisha kujiandaa kupata fedha za uchaguzi mapema. Vinginevyo, kama tulivyosema toka awali, Sheria na Kanuni hii hazina nia ya kujenga Fair and Level Play Ground. Hivyo Kifungu hiki pamoja na Form EE4 zinahitaji kuandaliwa upya. Kimsingi hizi Forms zinapaswa kujazwa "Progressively, yaani kila mchango, Donation, loan, Gift inapopokelewa. Na ikiwa lazima kwa Vyama vya Siasa, kila mkopo au donation au loan ya kiwango fulani inapopokelewa inaweza kupelekewa Taarifa kwa Chama na Chama kihamishe kwa Msajili. Hii itakuwa na maana kuliko ilivyo sasa, na nia na lengo la kudhibiti matendo ya rushwa litakuwa limetimia kwani ni rahisi kusimamia matumizi ya fedha hizo. Kimsingi Forms EE8,9 and 10 zinaweza tu kuwa na details za nani katoa baada ya uchaguzi au iwapo itakuwa inajazwa "progressively" as received during the campaign lakini kuzitaka zijazwe kabla ni kutokutengeneza kwa "Fair Play Ground" kwa vyama vyote. Na hasa Rulling na non Rulling parties.

  6:Kifungu cha 14(e) kinaongeza Sharti jipya ambayo haliko katika Sheria. Fedha za mgombea mmoja hazitakiwi ziwe Audited. Sharti hili halitekelezeki. Sheria inamtaka CAG afanye kazi hii, na wakati wa mjadala tulikataa kifungu hiki kwa vile hakitekelezeki kwa kuwa CAG hatakuwa na uwezo. Hivyo, si halali kuweka kwenye Kanuni kifungu ambacho hakiko kwenye Sheria. Kazi ya Kanuni ni ku "operationalize sheria na siyo kuweka masharti mapya. Kifungu hiki kifutwe. Sheria inatamka kuwa Mgombea ataandaa Taarifa, siyo awasilishe Taarifa iliyo kaguliwa.


  Kifungu cha 14(3) kinachosema, "on completion of the report… na kisha baada ya (b) kinasema, " …..within 30 days following the date of notification by political party of the amount apportioned to that candidate" kifungu hiki ni contradiction. i) Notification inapelekwa kwa mujibu wa Form EE3. Form hii ni " intention" tu. Siku 30 itakuwa bado katikati ya uchaguzi, hivyo, si haki kumtegemea candidate kutoa Taarifa ya fedha siku 30 tangu apewe intention. Kwa kuwa ni intention inawezekana kabisa hata siku hizo 30 fedha hizo bado zitakuwa hazijamfikia, pili, hata kama zimemfikia, si jambo la kawaida kutoa taarifa ya fedha katikati ya shughuli nzito kama Kampeni ya uchaguzi. Kifungu hiki kirekebishwe na kuwa siku 30 baada ya uchaguzi. Na hii ndiyo mantiki ya Form EE10.


  7: Kifungu cha 15(1) Kinachomtaka "candidate"…to which the provisions of these regulations apply "SHALL" required to apply expertise of persons who profess knowledge in accountancy…" Kipengele ni kipya, hakipo kwenye sheria, na kitawanyanyasa wagombea. Kipengele hiki kifutwe. Mgombea atakiwe tu kutunza kumbukumbu kwa kadiri inavyowezekana, na asitakiwe kwa lazima kuwatafuta wataalamu wa fedha. Hii ni kumwongezea mgombea gharama zisizo za lazima ( tena kama shindwa uchaguzi), Tena kiepngele kimetumia neon SHALL badala ya MAY. Hii ni hatari na watu wanaweza kufungwa au kushitakiwa bila sababu yeyote kwa vile kutokutekeleza vipengele hivi ni "offence" yaani ni "Kosa" chini ya Sheria.


  15(3) Kifungu hiki ni kishekesho. Ni mgombea gani au msaidizi gani wa mgombea ubunge labda aliyekuwa waziri, au mfanyi biashara mkubwa, au mtumishi wa Serikali wa ngazi ya juu, ambaye anaweza kuweka kumbukumbu yake kwenye "Electronic Form". Hitaji hili ni jipya na haliko kwenye Sheria yenyewe hivyo lifutwe. Kanuni haipaswi kama nilivyosema awali kuweka masharti mapya ambayo hayako kwenye Sheria yenyewe. Ikumbukwe kuwa Sheria inakubali kuwa hata badala ya receipts "statement iliyosainiwa inakubalika kulingana na mazingira halisi ya nchi yetu ambapo hata matumizi mengine yanaweza kufanyika ambako hata receipts hazipo. Kanuni imesahau Sheria hii inatungwa kwa wagombea wote, wakiwemo madiwani, tena katika nchi ambayo hitaji kubwa la Kikatiba/kisheria ni " kusoma na kuandika"… na haya yote yanakwenda kinyume kabisa na Katiba ya nchi. Kifungu hiki kinatikiwa kufutwa.

  8: Kifungu cha 16(1) kifungu hiki kinatakiwa kiwe re phrased. Campaign Team inayozungumziwa ni ile ambayo mgombea anatembea nayo. Lakini kila anapofika kwenye eneo Viongozi wote wa Chama ni Campaign Team wa mgombea wao. Itakuwa ajabu kufika kwenye eneo na kisha viongozi wa Chama katika eneo husika wanatengwa. Hawa kimsingi wanajulikana, na katiba za vyama zinafafanua.


  Kifungu cha 16(2) na (3) kinazungumzia "…to the authority stipulated in section 7" Section hiyo inazungumzia "Disclosure of Funds" . Hivyo kipengele hicho kiangaliwe upya. Na hitaji hilo linaweza kuangaliwa pamoja na kifngu cha 17(2)(a-e) ili kiweze kupanuliwa inavyohitajika kwa kushirikisha viongozi wa vyama kwenye maeneo yao.

  9) Kifungu cha 18 kinaweka misingi ya Malalamiko yanayoweza kupelekwa kwa msajili ambavyo vinaweza kumwondoa Mgombea katikati ya Kampeni, na au hata mahakamani baadaye. Matendo yanayoweza kulalamikiwa yameainishwa katika kifungu cha 18(2) (a-e). Hivyo kama tuko makini kuepukana na malalamiko hayo ni lazima tufanye marekebisho makubwa kwenye vifungu nilivyovitaja hapo juu, mathalan "kushiriki kwa mtu asiyidhinishwa katika Kampeni Team" kama ilivyo kwenye namba 8 hapo juu. Hivi ni vifungu muhimu sana katika kujenga Free and Fair Election, na hasa Fair and Level Play Ground kwa wagombea na vyama vyote.


  10) Kifungu cha 19 kinatumia neno "may" badala ya "shall" ni vizuri neno "shall" litumike ili kuwa na uhakika kuwa haki ya wagombea inalindwa na hasa "right to be heard:" ambayo inatolewa na sheria. Hatuwezi kuiondoa haki hiyo kwa Kanuni.


  11) Katika kifungu cha 25 neno "Shall" liondolewe na neno "May" itumike. Si haki kulazimisha vyama kufanya kitu kama hawataki kufanya hivyo. Iwapo "candidate na chama chake hawataki kutumia fedha zao kwenye matangazo na badala yake wakatumia

  kwa kitu kingine ni uamuzi wao sio wa Serikali.


  Ni imani yangu vipengele husika vitarekebishwa kwa manufaa ya Uchaguzi ulio huru na wa haki katika nchi yetu.


  Natanguliza shukrani za dhati


  ………………………………………..

  Dr. Willibrod Peter Slaa,(MB)
  MBUNGE WA KARATU,
  KATIBU MKUU-CHADEMA.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  asante Dr. Slaa.. hii sheria ni mkuki tu; imeandikwa kwa kukurupuka bila kuangalia the unintended consequences. Na ukiangalia itaumiza sana demokrasia, uhuru wa vyama kuendesha mambo yao na ninaamini inaingia kwa kiasi kikubwa uhuru wa kujieleza kuliko sheria nyingine nyingi.
   
 3. m

  mtemi Member

  #3
  Mar 21, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AHSANTE DK. willy,tungekuwa na watu hata watano wa aina yako ambao wanapenda kuisadia nchiii hii kama wewe tusingelia na umasikini kihivyo.

  mungu akubariki,na akulinde dhidi ya njama za mafisadi
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Mar 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Dkt Slaa tunaomba hiyo nakala (hard copy) ui-scan na uiweke hapa kama attachment! Mimi nashindwa kuchangia kuhusu point ulizotoa kwa kuwa umetaja baadhi ya vifungu au sehemu za vifungu! Otherwise, asante kwa mchango wako!
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Dr. Slaa,

  Fanyeni petition Uchaguzi Mkuu uahirishwe hata ikiwezekana ufanyike December au Sheria hii mpya isitumike kabisa mwaka huu, na ianze kupitiwa upya na kufanyiwa kazi.

  Je Bunge na Bungeni hamuwezi kupiga kura kusitisha muswaada huu kuwa Sheria?
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  .

  Rev K, ni kweli mahakamani ndipo mahali pa kupatikana haki, ila kwa mahakama zetu, tuna viwango tofauti vya haki hizo, miongoni mwa vitu vugumu kabisa kabisa kabisa kwa mahakama kuamua, ni kuusimamisha Uchaguzi Mkuu.

  Otherwise, Dr. Slaa, asante.

  Nasikitika hapa nchini, hakuna programu yoyote ya uelimishaji umma kuhusu sheria mpya mpya tuzazozipitisha zina maana gani kwa nchi yetu na mwananchi wa kawaida.
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  dk slaa,
  mbona umetujuza so late?
   
 8. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,994
  Trophy Points: 280
  Iko Cream saana hii sema tu imekuja late sana
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nadhani kuna wakati simuuelewi Dr. Slaa mpiganaji wetu!

  Lakini wakati mwingine pia watu tunatofautiana, kuna wale wanalenga IMPACT/RESULT na wale wanalenga kupata upinzani tu na kubisha tu ili kupata media airtime... hata pale ambapo unawezakutumia njia fulani sio public sana lakini pia malengo yako yakatimia bado njia hizo hazitumiki... Ndio maana kuna wabunge wengi bungeni hawaongei sana lakini result majimboni mwao ni awesome.

  Sasa Dr. Slaa, hizo ni kanuni na nijuavyo mimi hizi hazihitaji kurudi mbungeni kujadiliwa, mawaziri wanaotunga etc.,. unawamudu. Je umefanya lolote kabla ya kuleta hapa!

  Hata hivyo kila mahali umekuwa unatabiri tu ndio mbaya, wakati mwingine sio lazima hiyo nia mbaya iwepo pia. Ila ni sahihi kweli kuweka kila neno sawa, but it is clear maneno yatakuwa sawa kwa nani kwa kila mtu, la hasha, ukiwa madarakani uta-ji-behave almost more than50% ya CCM wanavyoji-be-have leo...

  Ndio maana sisi wananchi wengine hatuwasikilizi kwa100%... tunachuja sana kutoka kwa wanasiasa.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hivi mahakama zetu huwa zinatoa haki ya kweli?
  Au haki ni kwa wenye nazo na maskini wanaendelea kutaabika kwa kukosa haki.!
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kanuni zenyewe ndo zipo jikoni zinaandaliwa, hata hazijawa published bado
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nimesikia baadhi ya wasimamizi wakuu wa sheria hii wakisema kwamba hii ilikuwa ni ahadi ya JK alioitoa wakati analihutubia Bunge kwa mara ya kwanza December 2005.

  Tujiulize ni kwa nini ahadi hii imechelewa kuletwa Bungeni kwa karibu miaka mitano sasa. Kwa nini imeletwa kwa hii ya zima moto sasa?


  Naamini hofu ya JK na wenzake walioko madarakani kwa sasa kwa wenzao walioondolewa madarakani ni kubwa zaidi. JK anajua akina EL, RA, Mramba, Yona, Karamagi,.....wanazo pesa na wanaweza kuzitumia kumwondoa kama walivyozitumia kumweka madarakani.

  Ndio maana sheria hii ikashinikizwa haraka bila kuangalia madhara mengine kama ulivyoyainisha hapo Dr Slaa pamoja na yale alioyabaini Mwanakijiji kwenye ile thread nyingine.


  Jaribuni kutafuta wanasheria wazuri ambao wako juu zaidi ya siasa za vyama wawasaidie. Wengi tunajua kwamba wenye mapesa ya kumwaga kwenye chaguzi hizi wako CCM.
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Hatujachelewa sana. Baada ya sheria kupitishwa sasa kanuni ndio zinatungwa ili kusaidia utekelezaji wa hiyo sheria. Kanuni zipo mikononi mwa waziri, hivyo kama zina mapungufu naamini zinaweza kubadilishwa kirahisi tofauti na sheria ambayo mabadiliko mara nyingi ni lazima yapitie bungeni.
   
 14. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza Dk Slaa nakushukuru kwa hii post muhimu sana, hasa kwa wana JF.

  Kuna dalili za wazi kuwa hata kama serikali ina dhamira njema kwa taifa juu ya rushwa wapo watendaji ambao waegemea zaidi kwenye chama tawala ama KWA KUJUA AU KUTOKUJUA lakini wakijipendekeza.

  WITO.
  Hili ni taifa letu WALIOKO MADARAKANI NA WALE AMBAO SIYO WATAWALA. kwenye mambo muhimu kama haya tuweke utaifa wetu mbele kwanza.

  Mimi nawashauri watungaji wa hizi kanuni kuweka kizazi chao mbele ya fikara za utunzi wa kanuni.
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Dr. Slaa,

  Asante sana kwa uchambuzi wa kina. Kila sheria hapa duniani inakuwa na mapungufu yake. Muhimu ni kuangalia kama faida ni kubwa kuliko matatizo na kisha kuanza kuyapunguza matatizo kwa kufanya marekebisho kama ulivyoshauri kwenye ujumbe wako.

  Swali langu ni je ungelipewa uamue kama sheria hii itumike kama ilivyo kwa mwaka 2010 au isitumike kabisa, ungechagua nini?

  Mimi naona pamoja na mapungufu yake bado hii sheria ina faida hasa kwa wanasiasa wapya na wale ambao hawana mapesa ya kumwaga. Wabunge wengi walioko madarakani wanaipinga kwasababu inawapunguzia nafasi ya kutumia mapesa kununua ubunge kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma.

  Muhimu ni kupendekeza mabadiliko mbalimbali ili kuifanya iwe bora zaidi.
   
 16. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa,
  Pamoja na mapungufu hayo uliyoyaainisha ambayo naamini utayafikisha kwa msajili (kama kifungu cha 30(2) cha sheria kinavyotaka) ni vema tukaanza mchakato wa kushinikiza mabadiliko katika sheria yenyewe.

  Kwa mfano kifungu cha 30 (2) cha sheria kinamtaka msajili wa vyama vya siasa kuvipa daft reulations vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kwa madhumuni ya kupata maoni kutoka kwa wananchi kabla ya kupeleka kanuni hizo kwa waziri. Hapa kuna shida.

  Mimi nilitegemea sheria ingeenda mbele zaidi na kumtaka msajili baada ya kupata maoni chini ya kifungu 30(2), kuyazingatia maoni hayo. Kwa sheria ilivyo sasa msajili anaweza kupata maoni na kuamua kuyatupilia mbali bila ya sababu za msingi.
   
 17. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Dk. Slaa sikuelewa hiyo barua ulikuwa unamuandikia nani. Nani hasa ametunga na anayesimamia kanuni hizo?

  Kinachotakiwa ni kwenda mahakamani kuzichallenge hizo kanuni kwa sababu kama ni kupitia bungeni CCM itatumia wingi wa wabunge na kuzipitisha kwa mabavu. Ikiwa hivyo hakutakuwa na haja ya uchaguzi kwa sababu viti vingi CCM itapita bila kupingwa kwa msaada wa hizo kanuni ambazo bila shaka CCM ndiyo mhandaaji wake. Na hili litafanya wananchi wengi kupoteza imani na mfumo mzima wa uchaguzi. Hawataenda kwenye vituo kujiandikisha wala kupiga kura. Na hilo litaifaidisha CCM kwa sababu ya uwezo wao wa kuwahamasisha wanachama wao.

  Vipi habari ya kurekebisha au kutunga Katiba mpya? Mbona hakuna harakati tena?
   
 18. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Utengenezaji wa kanuni ninavyofahamu ni processs (mchakato) na ni lazima zifikishwe kwa wadau kabla ya kutumika. Ni kiwango gani mabadiliko yanaweza kufanya inategemea na uono/uelewa wa wadau wanaoshirikishwa. kama ni hao hao mabadiliko yanaweza kuwa kidogo sana. naomba wenye moyo na uzalendo kama wa Mh dr Silaa waendelee kupigana hadi tone la mwisho ili zipatikane kanuni za kweli na zenye tija na sio kandamizi kwa ajili ya kukomoa vyama vichanga.
   
 19. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Dr. Slaa alikuwa anakuandikika wewe mwana JF, ndiyo maana ameeleza katika utangulizi wake soma hapa chini: Nakuwekea usome nyie ni akina Tomaso.

  Wanajamii Forums,

  Natumaini hamjambo. Nilikuwa napitia Kanuni za ku operationalize Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ( Elections Expenses Act, 2010), No. 4 of 2010 REGULATIONS, (made under section 31 ).ambazo kwa bahati mbaya sinayo Electronically. Iwapo kuna mtu anazo nitaomba aziweke hapa. Hata hivyo, nimeona kuna matatizo makubwa na vipengele kadhaa. Ni imani yangu kwa kuzijadili tunaweza kutoa mchango mkubwa kwa Wahusika. Ifuatayo ni analysis yangu. Nawashukuru sana.
   
 20. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  jambo la msingi ni kusoma na kuyaelewa vyema mawazo ya Dr.
  kiukweli tunahitaji kuwa na mawazo na hoja mbadala katika hili
  ni rahisi san ku-challenge pasipo evidence, ndio maana Dr katoa quotes kadhaa kwa ajili reference
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...