tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,838
- 18,250
Kwa mujibu wa kanuni mpya za TFF, wachezaji binafsi hawapaswi kuwa na mdhamini ambaye ni mpinzani kibiashara wa mdhamini mkuu wa ligi kuu (NBC). Hili ni jambo la ajabu sana. Kwanini kanuni hii ya ajabu imepitishwa? Nionavyo mimi kanuni hii inalenga kuwarudisha nyuma wachezaji kiuchumi na kuwafanya waishi maisha ya njaa kama ilivyokuwa zamani.
Hii kanuni inawabana wachezaji tu, huku ikiwa haigusi timu shiriki. Kwa mfano Yanga na Simba wanadhaminiwa na benki ya NMB lakini hawajaguswa. Pia Simba wanadhaminiwa na kampuni ya m-bet na pia kuna baadhi ya timu zinadhaminiwa na sportpesa. Na hawa ni wapinzani wa kibiashara. Mbona wao hawawekewi mizengwe?
Pia huko Ulaya, kwa mfano, utakuta Real Madrid inadhaminiwa na Adidas lakini Ronaldo alikuwa anadhaminiwa na Nike na alikuwa akivaa njumu za Nike bila shida. Na pia benki ya Barclays wanadhamini ligi kuu ya Uingereza lakini wachezaji wa Liverpool wanavaa jezi zimeandikwa Standard Chartered bila tatizo.
Hawa ndio wanajua umuhimu wa udhamini kwenye ligi sio hawa TFF wanajifungia kwenye kiota kimoja na NBC na kusahau kuwa huko Ulaya wachezaji wanapiga mpunga wa kutosha kwa kudhaminiwa na wadhamini wengine mbali na mdhamini anayedhamini ligi zao.
Na kibaya zaidi, wachezaji wa ligi kuu hawaruhusiwi sio tu kuvaa jezi au njumu zenye nembo au jina la mpinzani wa NBC tu, bali hata kujihusisha kwenye matangazo (na haya hayana athari kiwanjani). Kwa mfano, mchezaji Clatus Chama anashiriki matangazo ya CRDB na kupiga mpunga mnene. Na pia mchezaji Mwamnyeto anashiriki matangazo ya NMB yanayompa mpunga mnene. Haya yote yatapaswa kukoma mara moja kwa mujibu wa kanuni mpya za TFF.
TFF kama wameshindwa kusimamia maslahi ya wachezaji ni bora TFF ibinafsishwe kwa mwekezaji kutoka nje atakayekuwa anajali maslahi ya wachezaji. Napendekeza wakati tunawauzia waarabu bandari, tuwauzie pia TFF waiendeshe.
Nawasilisha.