Kanuni mpya za fedha: Dr Mpango

Kanuni mpya za fedha: Dr Mpango

CCM mbele kwa mbele tutanyooka
Hivi siku hizi madokta wanapatikanaje kwani?
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati
 
Nchi hii ni masikini ya kutupwa,sijui hawa jamaa wakikaa kwenye hayo ma V8, na milolongo ya ving'ora huwa wanadhani hii nchi ina neema kama walizonazo wao?.

Wanaleta siasa za enzi za Nyerere mtu ukitaka dola ukaombe Benki kuu kwa maelezo kibao, Ukitaka kusafiri nje ukaombe kibali cha Ikulu, Yaani hawa jamaa wanaturudisha enzi za uchumi uliofeli wa Julius Nyerere.

Hawa jamaa watasababisha umasikini uliokithiri wa wananchi
 
These people are communists, hawa jamaa ni wakomunisti, na wakomunisti hupenda sana mambo ya control, kwao hii huwahakikishia kuthibiti madaraka lakini at the exponse ya maisha ya kimasikini ya watu huku wao watawala wakiishi katika neema.

Chini ya dr Mpango na serikali hii kiukweli tunapiga U-turn kwa kasi kubwa kurudi katika maisha ya kinyongenyonge ya kuvaa midabwada ambayo tulishaacha.

Hii serikali ya Kikomunisti iambiwe kuwa sera zake za uchumi ni Muflisi itatupa umasikini wa kutisha kwa sera zake za kupenda kuthibitithibiti.

Uchumi siyo siasa, Siasa unaweza kuthibitithibiti na kutokana na watu kuwa busy kutafuta ugali wa watoto wao wakakuacha tu, Lakini ukijifanya kuthibiti thibiti natural flow ya uchumi unavuruga juhudi za watu kupata ugali!. Ikifikia watu wanakosa ugali wao kwa sababu ya sera mbovu hakuna magari ya washawasha yatawarudisha nyuma, hawa jamaa hawajifunzi huko Sudan na nchi nyingine?
 
Kanuni ya 11 inasema miamala miwili au zaidi ikifanywa ndani ya saa 24 na kufikia dola 10,000 za Marekani au zaidi, itachukuliwa kuwa ni muamala mmoja na hivyo itatakiwa kutolewa taarifa.

Mpango: "mtu anayefanya muamala wa fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 10,000 au zaidi, kutoa taarifa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU)"

Me on Monday: 'Muamala wa $ 7800"

Me on Tuesday: 'Muamala wa $ 9500"

hapo nani mjanja?
😉😉😉😉
 
Ukipata Dhahabu kwa mkupuo moja itakuweje ukitaka kuuza, hizo sheria za nchi za magharibi tuziangalie vizuri zinatuhabia uchumi, pia usumbufu mkubwa
 
Kwa waliowahi kufika Ethiopia watakubaliana nami kuwa tunaelekea Ethiopia sasa. Kama walivyo Waethiopia, tutaanza kuikimbia nchi yetu katika hii miaka 10 ya hawa watu.
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati
 
Maskini wa Kigoma anapokuwa waziri wa fedha....tutaishia kufa malofa.

Hizi ni sheria za Kistalinstalin.
Sioni ni kwa namna gani nchi yenye viongozi wenye mentality za kutaka kuvuna tu kutoka kwa wananchi bila kuinvest kwao.
Kuthibiti bila kutoa nafasi
Sioni serikali ya aina hii ikiwavusha watu wake zaidi ya kuendelea kuthibiti power isiwaponyoke kwa nguvu zao zote

Hizi kanuni zitaendelea kudidimiza biashara, they are not business friendly at all
 
Kusema ukweli hata $10,000 ni ndogo kwa wafanyabiashara hata wa level ya kati.
Daaaaah
Aisee, huu ni umasikini uliokithiri. Tatizo watu waliokulia kwenye mazingira hatarishi hawawezi kuwaza nje ya makuzi yao.
Hivi unaanzaje kuwaza kuripot muamala wa dola 1000. Jamani hii si 2.3m? Yaani nusu ya mshahara wa DED
Kweli ukistaajabu ya firauni unaweza kufir
 
Madikteta wanapenda sana ku-control watu. Step kwa step wanafanya hivyo... Slowly but surely... Baada ya miaka 10, sijui Tanzania itakuwaje.
KANUNI mpya za kudhibiti utakatishaji fedha, zinatarajiwa kubana zaidi wanaofanya miamala kwa njia za kielektroniki ikiwamo benki na simu za mkononi.

Kwa mujibu wa kanuni hizo zilizosainiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Mei 7, mwaka huu na kuchapishwa kwa umma Mei 24, zinataka taarifa za mtu anayefanya muamala wa fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 10,000 (zaidi ya Sh mil. 20) au zaidi, kutoa taarifa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU).

Kanuni hizo pia zinabana wanaochezesha michezo ya kubahatisha kwa njia mbalimbali ambao nao wanatakiwa kutoa taarifa zao FIU.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, kiasi hicho kinachotakiwa kutolewa taarifa ni kile kilichofika thamani hiyo ya fedha kwa muamala uliofanyika kwa wakati mmoja.

Katika kanuni hizo, uhamishaji fedha umetafsiriwa kuwa unajumuisha “shughuli yoyote ya fedha inayohusisha amana, utoaji, kubadilisha, malipo au kupokea fedha kwa shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni.”

Kanuni ya tano inasema, “mtu anayepaswa kutoa taarifa, atapaswa kutoa taarifa zifuatazo katika Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) (a) ubadilishaji wa fedha zinazohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni ambayo thamani yake ni sawa na dola 10,000 za Marekani au zaidi kwa mara moja.

“(b) Kuhamisha fedha kwa mtandao, unaohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni sawa na Dola 1,000 za Marekani au zaidi kwa mkupuo.

“(4) Katika kutambua thamani ya fedha za kigeni sawa na Dola za Marekani 10,000 kwa madhumuni ya taarifa ya fedha au dola 1,000 kwa lengo la kutoa taarifa za uhamisho wa fedha za kwa njia ya kielektroniki, muhusika anatakiwa kutumia viwango vilivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania vinavyotumika kwa wakati huo.”

Akizungumzia kanuni hizo, Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, alisema; “kanuni zinasema mtu yeyote anayefanya muhamala wa fedha kwa njia ya mtandao ama anayesafirisha fedha kwa njia ya mtandao, atoe taarifa kwamba ‘nataka kusafirisha kiasi fulani kwa sababu fulani’.

“Kama unatuma fedha Japan kwa ajili ya kununua gari ama umepokea fedha kutoka nje, au unataka kumtumia mtu fedha zinazofika kiasi kilichotajwa kwenye kanuni, lazima utoe taarifa, hii ni kwa benki ama simu kwa sababu zote hizo ni njia za kielektroniki.

“Utaona dhumuni hapa ni kupambana na fedha haramu ama ndiyo maana ukienda kwenye mambo ya ‘cash’ kuna sheria inabana ipo kwenye viwanja vya ndege na mipaka, kwamba mtu anaweza kusafirisha kiasi gani cha fedha na azitolee taarifa.

“Kwa hiyo inahusu watu wote kama ni nje ama ndani ndiyo maana inasema ndani au nje ya nchi,” alisema.

Alisema kanuni hizo zinabana hata wale wanaochezesha michezo ya kubahatisha ambao kama wanataka kutoa fedha kama zawadi ambazo zinafika kiwango kilichotajwa na kanuni wanatakiwa kutoa taarifa hizo.

“Kwa hiyo hizi kanuni zinakubana kama unataka kutumia njia za kielektroniki kutuma fedha ama kuchukua fedha huko,” alisema.

Kanuni ya 11 inasema miamala miwili au zaidi ikifanywa ndani ya saa 24 na kufikia dola 10,000 za Marekani au zaidi, itachukuliwa kuwa ni muamala mmoja na hivyo itatakiwa kutolewa taarifa.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, ripoti za uhamisho wa fedha kielektroniki au ripoti zote za fedha zitapelekwa FIU kabla ya kumalizika kwa siku tano za kazi baada ya siku ya uhamishaji.

“Zitapelekwa kwa njia ya kielektroniki au vinginevyo inavyohitajika na FIU, kila operesheni ya shughuli za michezo ya kubahatisha atahitajika kutoa ripoti ya fedha kwa fedha zilizopatikana kutoka kwa mteja,” inasema sehemu ya kanuni hizo.

Kanuni hizo pia zimeweka adhabu mbalimbali kwa watakaoshindwa kufuata matakwa yake ikiwa ni pamoja na faini na kifungo.

Zinasema FIU au mdhibiti akiridhika kwamba mtoa ripoti ameshindwa kutoa ripoti ya fedha au uhamisho wa fedha zilizohamishwa kielektroniki au kimataifa, kitengo hicho kinaweza kutoa onyo au tahadhari ya kurudia mwenendo uliosababisha kutotii.

Mtu atakayefanya kosa hilo pia anaweza kusimamishwa kufanya shughuli yake ama biashara, kutozwa faini isiyozidi Sh milioni tano na isiyopungua Sh milioni moja kwa siku ambayo kasoro ilijitokeza.

Adhabu nyingine ni kusimamisha leseni ya biashara au kusimamishwa au kuondolewa kutoka ofisi ya mfanyakazi ambaye alisababisha kasoro hiyo.
 
Hawakurupuki, wao wanaogopa pesa ya mabeberu isiingie nchini kinyamela. Nchi zinazopata misuko suko huwa kuna donor somewhere anaingiza nguvu ya pesa, wao hapo wamebana. Vyama vya siasa wamepewa mashart magumu kuliko yenu, wao kiasi chochote wanachopewa wanahitaji kuriport serikalini, na balozi zote zimepewa masharti ya jinsi na namna ya kusaidia vyama vya siasa na NGOs, lengo lao ni kuhakikisha hakuna anayepata pesa nje serikali isifahamu, huo ndio udhibiti walioweka. Ubalozi au shirika lolote la nje likitaka kukisaidia chama cha siasa kwanza serikali inapewa taarifa za kiasi na malengo ya msaada, na ndio maana uliona ulifanyika uhakiki wa NGOs zote na kuweka masharti ya kutoa taarifa za mipango kazi yao mara kwa mara serikalini.
Walengwa siyo nyie wananchi wakawaida, nyie mmekumbwa na mtego wa panya. Kulinda madaraka siyo kazi rahisi, lazima yatengenezwe mazingira magumu kwa kila mtu ili ionekane ni kawaida, na siku wakibinywa waseme hii siyo kwao tu bali ni nchi nzima.
Hivyo msimlaumu Dr. Mpango, yeye ni mtekelezaji wa mipango iliyo kwisha ratibiwa serikalini. hata akifahamu hasara ya sera Fulani leo, hawezi kubadirisha kama imeamriwa hivyo. Nyie mnadhani Bashe anaakili sana kuliko Dr.mpango, ni kwasababu mpango hutekeleza mipoango iliyopo hatengenezi sera yeye.
That is a fact...na nimelink pia kwa kuwa tunaelekea kwenye uchaguzi....20/20
 
Unaweza kuwabinya sana watu lakini huwa kuna threshold kufikiwa. Hiyo threshold siku ikifika, watalipuka tu. Threshold ya Sudan ilifikiwa mwaka huu. Na ya Tanzania ina siku yake....
Hawakurupuki, wao wanaogopa pesa ya mabeberu isiingie nchini kinyamela. Nchi zinazopata misuko suko huwa kuna donor somewhere anaingiza nguvu ya pesa, wao hapo wamebana. Vyama vya siasa wamepewa mashart magumu kuliko yenu, wao kiasi chochote wanachopewa wanahitaji kuriport serikalini, na balozi zote zimepewa masharti ya jinsi na namna ya kusaidia vyama vya siasa na NGOs, lengo lao ni kuhakikisha hakuna anayepata pesa nje serikali isifahamu, huo ndio udhibiti walioweka. Ubalozi au shirika lolote la nje likitaka kukisaidia chama cha siasa kwanza serikali inapewa taarifa za kiasi na malengo ya msaada, na ndio maana uliona ulifanyika uhakiki wa NGOs zote na kuweka masharti ya kutoa taarifa za mipango kazi yao mara kwa mara serikalini.
Walengwa siyo nyie wananchi wakawaida, nyie mmekumbwa na mtego wa panya. Kulinda madaraka siyo kazi rahisi, lazima yatengenezwe mazingira magumu kwa kila mtu ili ionekane ni kawaida, na siku wakibinywa waseme hii siyo kwao tu bali ni nchi nzima.
Hivyo msimlaumu Dr. Mpango, yeye ni mtekelezaji wa mipango iliyo kwisha ratibiwa serikalini. hata akifahamu hasara ya sera Fulani leo, hawezi kubadirisha kama imeamriwa hivyo. Nyie mnadhani Bashe anaakili sana kuliko Dr.mpango, ni kwasababu mpango hutekeleza mipoango iliyopo hatengenezi sera yeye.
 
Ni kweli kabisa. Nchi zote zinazofuata sera za aina hii zimejikuta katika umasikini mkubwa - Korea ya Kaskazini, Ethiopia, nk. Badala ya kukopi kile kilichofanywa na nchi zilizopiga hatua, sisi tunakopi nchi zilizo fail big time. Kuondoka kwa Nyerere siyo kwa vile alizeeka. Aliona siasa zake zimeshindwa. Mwinyi, Mkapa na Kikwete wakarekebisha mambo kwenye soko. Hawa jamaa wameamua kuturudisha kwa Nyerere. Kwamba ukishikwa na noti ya dola wewe ni mhujumu uchumi! Unatupwa jela. Wakati utafika hatutaruhusiwa kuwa na $ bila kibali. Kweli lazima kila mtu aishi kama shetani.
Nchi hii ni masikini ya kutupwa,sijui hawa jamaa wakikaa kwenye hayo ma V8, na milolongo ya ving'ora huwa wanadhani hii nchi ina neema kama walizonazo wao?.

Wanaleta siasa za enzi za Nyerere mtu ukitaka dola ukaombe Benki kuu kwa maelezo kibao, Ukitaka kusafiri nje ukaombe kibali cha Ikulu, Yaani hawa jamaa wanaturudisha enzi za uchumi uliofeli wa Julius Nyerere.

Hawa jamaa watasababisha umasikini uliokithiri wa wananchi
 
Kanuni ya 11 inasema miamala miwili au zaidi ikifanywa ndani ya saa 24 na kufikia dola 10,000 za Marekani au zaidi, itachukuliwa kuwa ni muamala mmoja na hivyo itatakiwa kutolewa taarifa.
Monday saa mbili asubuhi na Tuesday Saa nne asubuhi tayari ni zaidi ya masaa 24kwa hiyo siwez kubanwa na sheria
 
Mfanya biashara ambaye mzunguko wake ni mkubwa hana haja ya kuweka pesa zake benk. Kama mtu ushafikia kasi ya 4G kurudi analog ni utumwa.
 
Back
Top Bottom