Kanitukana sana kisa nimemtongozea JF

Kanitukana sana kisa nimemtongozea JF

CONSTRUCTIVE THOUGHT

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2015
Posts
1,158
Reaction score
417
Jamani hakuna mahari maalumu pakumuona umpendae. Pia hakuna mahali maalumu palipo ainishwa pakuanzishia mausiano, bali sehemu na namna yoyote inaweza faa kuanzisha mausiano ilimradi tu umemuona umpendae.

Hivi karibuni niliona picha (profile picture) ya msichana mrembo katika akaunti ya mmoja kati ya watu waliomo humu JF. Kiukweli ile picha ilinivutia sana, hivyo nikaona ni vyema nimtafute uyo dada ili nimueleze yangu ya moyoni.

Cha kustajabisha niliambulia matusi makubwa makubwa huku akiniuliza kwa lugha ya ukali "We bwege nani kakuambia mimi ni mwanamke? au umetumwa kunifatilia?", "unikom.. mimi ni mwanaume.. sio mwanamke kama unavyofikiria"

Baada ya majibu hayo nilielewa kuwa kumbe ni mwanaume ila ameweka picha ya msichana. Nilimjibu kwa kumuambia picha ulioweka ndio iliosababisha nijue wewe ni mwanamke. Lakini sikuishia hapo nilimuomba samahani!

Jamani katika hilo mimi ninakosa gani mpaka nitukanwe kiasi hicho?
 
Mkuu,kumbuka kila mtu humu JF amelelewa na malezi yake sasa usitegeme sana positive response kutoka kwa wengine,
Na hayo matusi usidhani anakutukana wewe anatukana maisha yake na kukujulisha kua hana peace of mind...
Hana ugomvi na wewe hata kidogo anaugomnvii na maisha yake,msamehe bure na usijibishane nae..
 
We na wewe acha mambo ya ajabu unatuaibisha wanaume. Yaani ukiona picha tu akili zimekuruka? Mbona huku kitaa warembo wamejaa na hawaijui hata JF? Kwenye mtandao wa kijamii kuna drama nyingi sio sehem sahihi ya kutafuta wanawake.
Kweli mkuu mitandao ya kijamii sio ya kutongozea!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom