Kanisa katoliki wamwibia mjane

Kanisa katoliki wamwibia mjane

Bigjahman

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
911
Reaction score
523
Kanisa katoliki jimbo kuu la Moshi pamoja na shule yake ya sekondari Marangu bila aibu wala hofu ya Mungu wamuhubiriaye maana hi ni taasisi ya kidini wamemnyang'anya mjane shamba aliloachiwa na marehemu doctor Geovan Balletto.

Shamba hilo ambalo lina liz lipo jirani kabisa na shule ya Marangu inayomilikiwa na kanisa Katoliki, limekuwa likikaliwa na marehemu na familia yake na baada ya kifo chake mnamo 1972 alimuacha hapo mjane na mtoto wao.

Ndani ya shamba hilo kulikuwa na hospitali ambapo doctor huyo aliyekuwa mzungu raia wa Italy alikuwa akiwatibu na kuwasaidia sana wanakijiji wa Marangu na vijiji vya karibu akisaidiana na mjane huyu ambaye alikuwa nesi.

Pia kulikuwa na mazao pamoja na miti mingi na nyumba kubwa ya kuishi ambayo mpaka leo familia inaishi hapo,bila haya kanisa na taasisi yake bila ruhusa ya mjane huyo waliingiingia kwa nguvu kwenye shamba hilo na kukata miti mingi tuu na kujenga kisima.

Waliharibu mazao na kutandaza mabomba ya kupeleka maji shuleni kwao,kana kwamba hiyo haitoshi kanisa lilijitwalia eneo la ekari tatu hivi na kuanza ujenzi,mjane huyo alipouliza aliwekwa ndani kituo cha polisi HIMO.

Imekuwa kawaida kila hila na uonevu dhidi ya mama huyu mjane kutumika kwa polisi wa himo{RUSHWA KANISANI?}.

Hivi sasa kanisa linatumia nguvu kubwa ya fedha {sadaka} na hila ili wataifishe shamba hili ambalo lina liz na uhalali wote uliochwa na marehemu kwa familia yake,kanisa linafanya haya kupitia mawakala wake wakuu askofu mkuu Moshi pamoja na mwalimu mkuu Marangu sekondari ambaye kila kikicha anamtishia mama huyu maisha.

Je ni lini kanisa katoliki litaacha kuonea walalahoi na kwa kutumia sadaka zetu wenyewe?

Kupitia hapa tunaamini mama huyu atapata msaada kutoka kwa serikali,wanasheria,wanaharakati na watu mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na ushahuri.
 
Napita nitarudi kujua Thread kam itapoteza mwelekeo au itakapofikia.................

:bolt:
 
Unaonekana ni mwenye kuongea kwa ushabiki ukiomba public sympathy bila kujali kwamba unaweza kugundulika.

Uzoefu unanionesha kwamba wengi wa wanaoitwa wajane si watu wa kuwasikiliza upande mmoja na kufanya maamuzi. Ikiwa unahusika kwa kiasi hicho na hilo shauri, bila shaka ungetuwekea Lease ya hilo shamba (sio Liz) ili tujionee na si kuropoka km mama wa kiswahili.
 
sitafuti public sympathy mzee,hili swala linajulikana marangu nzima,iyo lease nitaiweka apa
 
sitafuti public sympathy mzee,hili swala linajulikana marangu nzima,iyo lease nitaiweka apa

nijuavyo mimi hayo mashamba au hilo eneo la shamba kanisa linalimiliki tangu mwaka 1890. mara nyingi wanaolalamika unaweza kukuta walikuja hapo kama wafanyakaz au walipokelewa kama watoto yatima flan au watu waliokuwa na mahusiano mazur na uongoz uliokuwepo wakati huo. sasa tatizo hawa watu kama walipewa wangetakiwa wawe na maandishi halis na kama yapo cdhan kama kanisa linaweza kufanya chochote. pamoja na yote mimi ningeliomba kanisa kama huyu mtu alikuwa mtumish wao kweli wampe angalau eka 3 tu kibinadamu.
 
sitafuti public sympathy mzee,hili swala linajulikana marangu nzima,iyo lease nitaiweka apa

Hata kama lingejulikana DUNIA NZIMA achilia mbali Marangu nzima... inachotakiwa ni uhalali wa umiliki na si ujane au umaarufu wa kesi. Kuna cases nyingi za aina hii (na mara nyingi zinahusisha watu wanaojiita 'wajane'' (labda kutafuta sympathy?)) lakini ukichunguza kwa undani unakuta wanaosema wanaonewa ni watu walioishi sehemu muda mrefu na wenye umiliki halali wanapoamua kuiendeleza wanadai wanadhulumiwa!
 
Nadhani kabla ya kuandika comments za namna mtu anavyojisikia kuhusu kanisa katoliki ingetafutwa story ya upande wa pili. Mtoa mada ameeleza kama kulishtaki kanisa dhidi ya mama mjane, lakini binafsi naamini nae ni mwanadamu mwenye hulka na mitazamo yake.
 
sitafuti public sympathy mzee,hili swala linajulikana marangu nzima,iyo lease nitaiweka apa

Mshauri aende mahakamani. Nina wasiwasi kama kanisa katoliki linaweza kufanya kitu kama hicho. Nadhani kuna utata ambao unahitaji suluhisho la mahakama.
 
kama sio dini ni nini?!! waisilamu acheni kuingilia mambo msioyajua. Mnatokwa povu mdomoni kutetea kitu ambacho huna ushahidi nacho. shame on you
Nani kakwambia ni dini hebu nipe maandiko kwenye hiyo biblia yanayosema christianity is a religion kwa taarifa yako
Hni kampuni na wanaojua kutumia fursa wamefaidika sana rejea gwajima, mzee wa upako na wengine na bidhaa za
hhii kampuni ni nyingi kama sda, jehova witness, pentecostal, catholic among many so choice ni yako
 
Mama mjane anayo lease, na kama kanisa nalo linaamini wanayo lease yao hiyo ni double allocation.
Before the eyes of law wote tunajua the justice should be done and seen to be done.
Wote tunaelewa samaki mkubwa huwa anaamini kuwa anayo haki ya kummeza samaki mdogo ila kwa huyu mama hatuna budi kufatilia mashauri husika kwa karibu ili kuiweka wazi jamii ya wale wenye kujali haki,utu na ubinadamu wajue jinsi kanisa husika kama linatenda haki ama halitendi haki kwa mama husika.
Itakuwa ni aibu sana kama mabavu yatatumika ila naamini vyombo husika kuanzia land tribunal hadi mahakama vitazingatia haki ya huyu mama na pia vitazingatia kuwa kesi hii inatazamwa na level ya dunia na sio kijiji tena kama walidhani ni siri basi nawasihi tu wajue kuwa kesi hii itakwenda kuliabisha kanisa kama ubabe na outlaw acts zinazofanywa na kanisa zitaendelea dhidi ya mama huyu.
 
Naona ungeeleweka zaidi kama ungetuambia huyo mjane na Huyo dokta walinunua ilo eneo au walikua wakiishi baada ya kupewa!!?na je nani aliwapa??je huoni kama dokta RAIA Wa Italy alipewa hifadhi tu na kanisa ili aweze kuhudumia wanamarangu???yaan unaleta bandiko LA kichonganishi hivi hapa..ivi mzima wewe???kama kipedo kimekubana vua na uvae Della pambavu kbisa.
 
Hakuna ukweli hapa, hakuna kanisa lenye heshima na ukarimu kama katoliki, mleta mada tambua katoliki sio serikali kama mjane ameachiawa eneo basi atakuwa na vielelezo kamili hakuna kiongozi wa katoliki anaeweza kutoa rushwa kwa eneo dogo ikiwa katoliki linamiliki maeneo
 
Hakuna ukweli hapa, hakuna kanisa lenye heshima na ukarimu kama katoliki, mleta mada tambua katoliki sio serikali kama mjane ameachiawa eneo basi atakuwa na vielelezo kamili hakuna kiongozi wa katoliki anaeweza kutoa rushwa kwa eneo dogo ikiwa katoliki linamiliki maeneo makubwa kuliko unavyo fikiri, hiyo serikali sio ya kanisa tamwa sio ya kanisa
 
mkuu umezungumza kitu nyeti sana, lakini je, vyombo vya sheria havikufuatwa kushugulikia hilo suala?,

wewe una uthibitisho gani?,

na mbona umelihusisha kanisa zima, ikiwa ni moja ya taasisi zake ndo zimrhusika?,

lengo lako haswa ni nini, kama siyo kuchafua kanisa?.

mi nikushauri kitu, kama umelileta hili suala hapa JF, basi anika ushahidi wote, na mwenendo mzima wa hilo suala.

pia jua, mimi sipo upande wowote, ila sijapenda, vile umeli present hapa, ni kama umelichafua, maana jukumu lake ni kulinda na kutetea haki za wanadam wote, pia kukemea maovu kama hayo.

sasa nashangazwa na hii taarifa, usilipake matope kama siyo kweli.
 
mkuu umezungumza kitu nyeti sana, lakini je, vyombo vya sheria havikufuatwa kushugulikia hilo suala?,

wewe una uthibitisho gani?,

na mbona umelihusisha kanisa zima, ikiwa ni moja ya taasisi zake ndo zimrhusika?,

lengo lako haswa ni nini, kama siyo kuchafua kanisa?.

mi nikushauri kitu, kama umelileta hili suala hapa JF, basi anika ushahidi wote, na mwenendo mzima wa hilo suala.

pia jua, mimi sipo upande wowote, ila sijapenda, vile umeli present hapa, ni kama umelichafua, maana jukumu lake ni kulinda na kutetea haki za wanadam wote, pia kukemea maovu kama hayo.

sasa nashangazwa na hii taarifa, usilipake matope kama siyo kweli.
Kesho nitakuja na ushahidi mzima, nimelihusisha kanisa lote maana haya malalamiko kanisa katoliki Tanzania bara wanayo,hii kesi aridhi kilimanjaro na polisi wanaizungushwa sana danadana nyingi hiyo ni dalili tosha ya mazingira ya rushwa
 
Hapo Kanisa Katoriki Lilikuwa Linamiliki Eneo Hl,mzungu Alikuwa Akifanya Kazi Na Hvy Aliazimwa Akae Hapo Ili Aweze Kuwah Kazini.Baada Ya Kifo,ndo Mjane Anadai Eneo Ni Lake!!
 
Nina wasiwasi mkubwa na taarifa ya huyu jamaa aidha ni ushabiki au ni umbea wake tu! Miw sidhani kama ni kweli hebu tusikilize upande wa pili wa shilingi.
 
Back
Top Bottom