Chagga King
JF-Expert Member
- Jul 6, 2011
- 1,931
- 1,178
Chagga king, mimi si mwanasheria ila kwa upeo wangu mdg naamin kwamba ile lease itamsaidia yule mama nikirefer cases nyingi ambazo ni similar na hii hapa, juzi tu niliona kwenye vyombo vya habari mkuu mmoja wa kanisa alipojaribu kuchkua ardhi ya mjane, hati(lease) ilimsaidia yule mama na serkali ilivunja zile nyumba if am not mistaking hii issue ilitokea mbezi daresalam, ama labda unisaidie maana ya lease ni nini labda na nini kazi yake
wewe unazungumzia issue ya Getrude Lwakatare, yule mama mchungani, mbunge na mmiliki wa shule za st. marys, yeye alienda kujenga eneo siyo la kwake na hakuwa na kielelezo chochote, ndiyo maana Ardhi wakamvunjia zile nyumba na kumrudishia lile eneo yule mjane.
Lease ni mkataba wa ukodishaji wa eneo (pango au shamba) ukisema mtu ana lease, unamaanishwa amekodishwa tu, (ila kuna kitu kinaitwa government lease, ambayo kwa Tz inajulikana kama Right of Occupancy/ hati miliki) sasa kama yeye ana lease, ujue alikodishwa kwa muda fulani, na kama muda huo umekwisha basi eneo litarudi kwa muhusika.
sisi huwa tunapenda kuwa mashabiki wa mambo tusiyoyajua bila kufanya utafiti,
sasa mleta uzi ameliHUKUMU kanisa bila kutoa uthibitisho, kama anayoyasema yana ukweli, basi alete uthibitisho, mbona yupo kimya? wakati vielelezo vipo?, kama atathibitisha hata mimi nitamsaidia, maana kaamua kulileta hili suala JF basi asisite kutoa ushahidi.
na kama anaona hapa siyo mahala pa kuweka huo ushahidi basi hakutakiwa kulihukumu kanisa kiasi hicho maana yeyw siyo mahakama.
na wanavyosema huyo mama ana hati, je ana hati ya aina gani?.