Ndg wanajamvi nasikitika sikuweza kuwa hapa kwa muda kdg haswa ukizingatia kama mtoa mada nilitakiwa niyajibu maswali yenj na pia kufafanua baadhi ya mambo. Nilikua namuuguza mama yangu mpendwa. Baada ya kusoma jinsi wengi wenu mliochangia ni kwamba kuna mnaodai lile eneo ni la kanisa, la hasha si la kanisa, lile eneo alimilikishwa Dr Balletto tena kisheria na hata ukienda pale ardhi wilayani ukaomba ramani utaona tu, na jirani yake ndo lilikua eneo la shule ya marangu. Ieleweke kwamba shule ile haikua mali ya kanisa katoliki hadi miaka ya 80 ilipokabidhiwa kwa jimbo katoliki la moshi, kwahiyo kanisa lilikua halina ardhi yyte pale, na baada ya kukabidhiwa shule kanisa ndo lilianza kufatilia ardhi ya jirani yani kwa mjane kama nilivyoeleza kwenye mada. Nimesoma alivyoandika mdau ngaiwoye anaesema kua ni jirani yake anavyoeleza ni sawa, nimesoma alivyoandika mdau chaga king ni kweli huyo dr Baleto kuna wkt alikua kule maua, na huskii familia yake ikiongelea maswala ya maua sababu ilibaki chini ya maua sem, mmeongelea juu ya lease na tittledeed nazan kuna waliofafanua hapo, ila napenda ieleweke document alizo nazo yule mama zinatambulika ofisi ya ardhi wilaya na ktk ramani hilo ya wilaya ilioyopo ofisi za ardhi shamba hilo lipo na linaonekana kwa jina la marehem na si kanisa wala shule. Kuna wengine wamedai kufahamu hiyo shamba na historia yake kua lilikua ni la kanisa, nawasihi waache uzushi na kubuni, ni lini kanisa lilimiliki pale wakati shule yenyewe ilikua si yao?? Kuna wengine wamemkashif mama mjane wakati hawamjui wala hawajui historia ila wameamua tu kutetea kanisa, mi mwenyewe ni mkatoliki toka kuzaliwa hadi uzee huu, sina sababu ya kulisingizia kanisa ila kwa hili kanisa ama watendaji wake hawako sawa. Kuna waliohoji uraiya wa mama mjane nazani ni ndg msingida, mama huyu ni raiya wa tanzania mzaliwa wa marangu na mwanae pia ni mtanzania maana alizaliwa hapa. Kuna mwingine alihoji kwanini raiya wa nje anamiliki shamba hapa, kuna watanzania kibao wana nyumba ughaibuni pia wana mashamba nchi za watu sioni tatizo kwa marehem kwani mkewe alikua mtanzania kabisa. Nawalongeza wale wote walioonyesha moyo wa huruma kwa mjane, MUNGU awabariki sana. Hivi sasa taarifa ambazo nimezipata ni kua mama mjane na mwanae wamefata mkondo wa sheria na hivi sasa wameshafungua shauri katika mahakama ya ardhi moshi na tayari kanisa na shule wameshapewa zuio la kuendeleza ujenzi pale huku kesi ikiendelea katika mahakama hiyo ingawa matisho ya mwalimu mkuu kwa mjane yanaendelea. Kwa maana hiyo basi nitashindwa kuweka ushahidi hapa kama nilivyoahidi kwa kua nitakua naingilia kazi za mahakama na uhuru wake. Wale wanaosema wanakaa pale ama wanapajua pale mfano benteke, ngaiwoye na wengine watakua sasa wameona barua za zuio zilivyobandikwa pale. Wasalaam mimi Bigjahman mpenda haki na muumini halali wa kanisa katoliki la roma