Kanisa Katoliki na uhuru wa Tanganyika

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika yanaweza kutupa sura mpya tusiokuwa tukiifahamu sote, Pengine ni kwa mara ya kwanza Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ndio kinaeleza uhusika kikamilifu wa Kanisa katoliki duniani katika uhuru wa Bara la Afrika na hasa Tanganyika chini ya shirika nguli la Ujasusi la Kanisa hilo . Utafiti wa kinyaraka na machipuzi ya nera kwa mambo anuawai, ndio yaliyonihakikishia kuhitimisha katika kitabu hiki, Tunapoadhimisha kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika tunayo sababu na ni haki yetu kutambua mchango wa kila mtu alivyoshiriki katika uhuru huo, haijalishi mapokeo, Tusipoandika historia yetu, tusilaumu tukiandikiwa.

Hebu turejee kwenye Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Kwa mfano, hali ya Tanganyika kuwa eneo ka kudhaminiwa, ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo, hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa, ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia.

Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi (Jeisuiti) kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua. Lakini, lilikumbana na kiunzi/ukinzani hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya Ukristu, kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana).

Mgogoro huo ulikuzwa kwa kuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa shirika lao la kijasusi la Fabian Society, maalumu kwa minajili ya kuwaandaa Vijana katika makoloni Uingereza hususani barani Afrika, kukabidhiwa nchi zao na kwa Tanganyika Fabian Society wao walikuwa wamemuandaa Chifu David Kidaha Makwaia huku Jeisuti ya Katoliki wakiwa wamemuandaa Julius Nyerere. Rejea kitabu cha Vatican Assassins cha Eric Jon Phelps akieleza nguvu ya Vatican katika kudhibiti ulimwengu, anakazia katika harakati za ukombozi duniani hasa Afrika na nafasi ya kanisa chini ya Jeisuti.

Barani Afrika, Jesuiti ilibadili mbinu kwa kuwa dola la Kiingereza, lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani. Haikujikita kwenye dola, bali ilisimama katika muundo wa shirika likifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri shahiri, ilikuwa lazima itimie, kama ilivyoelezwa mwanzoni kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu. Kwa hiyo, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika, chini ya Udhamini wa Shirikisho la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe. Mwaka 1927 hadi 1929, kanisa Katoliki nchini, chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi wake Tanganyika, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli. Tar. 12 Februari, mwaka 1929, Zelger alistaafu wadhifa wake kwa lazima.

Ni mwaka huohuo wa 1927, ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron, maalumu kwa minajili ya kuratibu mambo ya sherehe za watu weusi pembeni ya mji, huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na akawapa jengo la ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini, historia ya Tanganyika haiwataji kinagaubaga waasisi wa AA: Rais wa kwanza, Mwalimu, Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za Mjerumani kutoka kabila la Wayao), Katibu Mkuu wa kwanza, Klest Sykes (Mzulu, Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni kutoka Afrika Kusini), Mwekahazina, Ali Ramadhan (Mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania leo bahari ya Hindi).

Hawa ndio mwaka 1927, waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933, Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho, Bw. Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948, yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest, aliyeitwa Abdulwahid Sykes.
Abdulwahid Sykes alitoka kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia, huko Burma. Aliporudi, alikuwa na mawazo ya ujana kutoka vitani, akampindua baba yake kwa vurugu na ngumi. Mapinduzi yaliyoitwa ‘ondoa wazee’. Kisha chama cha AA kikabadilishwa jina na kuitwa TAA ambapo Rais wake wa Kwanza, akawa Daktari wa binadamu Vedasto Kyaruzi (Mhaya), aliyekuwa anafanya kazi Kingorwila Mkoani Morogoro.

Huyu ndie daktari wa binadamu wa kwanza kabisa wa Kiafrika, Tanganyika. Katibu Mkuu, akawa Abdulwahid Sykes mwenyewe na Mweka Hazina akawa Dosa Azizi. Miaka miwili tu ya chama kipya, yaani 1950, Daktari Vedasto Kyaruzi, kwa ghiriba za wakoloni, alihamishiwa Sengerema Mwanza, kama sehemu ya kumuondoa jijini Mzizima leo Dar es Salaam awe mbali na harakati. Nafasi ya rais wa TAA ikakaimiwa na Bw. Adbulwahid, mpaka mwaka 1953, uchaguzi ulipofanyika na Julius Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo (Mnazimoja ya leo).

Mnamo tar. 7 Julai, mwaka 1954, Vijana (wazee wa Kariakoo) wakiongozwa na Mwl. Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajesuiti (Askofu Maranta) na Waislamu (Sheikh Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, hekima za Sheikh huyu ziliendelea kusaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwl. Nyerere ya kwenda UNO tar. 5 Machi, mwaka 1955, kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tikiti ya ndege ya kwenda na kurudi. Lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani.

Si hivyo tu, bali katika moja ya utani wa Mwl. Nyerere wenye ukweli ndani yake, aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni mabosi wake, akikumbuka malipo ya Shilingi mia sita (600/=) angali ameacha kazi ya ualimu, akiwa kijijini Butiama. Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Nyerere kuja kuiongoza Tanganyika mpya. Barua ya lugha ya Kilatini, ya kitume, Tot Tangaeque, ya Papa wa Roma, ya tar. 8 Novemba, mwaka 1984, kwenda kwa Kanisa Katoliki Tanzania, inautangazia ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa chini ya himaya ya kanisa kwa mwavuli wa Bikira Maria Imakulata.

Miaka thelethini na mbili (32) baadae, Kanisa Katoliki Tanzania chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa, linaijibu barua hiyo kwa barua yenye kumbukumbu nambari TEC/PR/1 ya tar. 10 Novemba, mwaka 2016, likikubaliana na kuitangazia dunia kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika, tar. 9, mwezi 12 ya kila mwaka itakuwa pia siku ya kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Imakulata. MSIMAMIZI wa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA...........

Itaendelea..

Yericko Nyerere
 
Mbona jukwa liko kimya sana unaweza pita naked na watu wasikuone, endelea kushusha nondo tuflash vichwa vyetu
 
Kuna kitu hakiko sawa katika historia au watu hawajui ilikuwaje? Kinachonishangaza ilikuwaje mgeni akapewa uenyekititi? Sababu zinazotolewa hazina mashiko sana kuna kitu aidha nyuma ya pazia au kuna kurasa zimelukwa
 
Ngoja Mzee Said aje ajazie nyama historia yetu ni nzuri sana.
 
Mnanichanganyaga hili jukwaa mara utaskia kanisa la roma linaendesha dunia, akija huyu atakwambia CIA wanaendesha dunia, mwingine atakwambia Mossad, mwingine Mi6, mwingine free masons. Sasa sijui dunia zipo ngapi?
 
Umeipenda kwasababu wamesemwa wakatoliki wangesifia je?
Sasa huku si ndo wamesifiwa ,au ulitaka wasifiwe vipi?
Wametuandalia Future ya nchi yetu isije ikaangukia mikononi mwa mawakala wasio faa.Na kimsingi wamefanikiwa.
Ndo maana nchi yetu imedumu kwenye amani,kwa sababu walezi wa nchi hii ni wana Dini katoliki,watu wa Mungu.
sasa ulitakaje?
Tena mamewashirikisha na Mashehe akina Skh.Hassan bi Ameir.
 
Mzee wng Yericko Nyerere I salute u, Endelea kutupa vtu dah tuñamsherehekea Bikira Maria mh.
 
Mnanichanganyaga hili jukwaa mara utaskia kanisa la roma linaendesha dunia, akija huyu atakwambia CIA wanaendesha dunia, mwingine atakwambia Mossad, mwingine Mi6, mwingine free masons. Sasa sijui dunia zipo ngapi?
Zote ni CONSPIRACY THEORIES.
Hakuna uthibitisho wa moja kwa moja, ndio kusema ni kama stories za vijiweni.
 
Who said that?
This is not a conspiracy,
Jambo hili limeshaathiri maisha ya wengi tuu,wakati kimsingi haikutakiwa iendelee kuwa hivyo hadi leo.
Kuna kitu Tanzania kinaitwa ''memorandum of Understanding between Church an Government of tanzania''
Hii ni real, kwamba serikali italipia mishahara ya Taasisi zinazohudumia jamii ambazo ziko chini ya Kanisa,kwa kulipatia Kanisa Mamilioni ya shillingi.Huku dini nyingine zikinyimawa 'privilege' za aina hiyo .
Hi ni kutokana na ule msingi uliowekwa.
Haya si mambo ya kusema ni ya kufikirika ,yapo na yanaweza kuleta tashwish huko mbeleni.
 
Sasa mpewe mnakitu gani? Hiyo sio hisani wakristo wanaKCMC na Bugando kwa mfano ukiacha peramiho, st Francis hospitals. Ambacho zinatoa huduma kwa jamii, sasa nyie mlitaka mpewe pesa ili muendeleze au huduma gani mnayoitoa?
Kujenga misikiti kwenye sheli za mafuta au mpeleke radio imaan mkaboreshe CD za kigaidi za shehe ilunga.!!!
 
Sija sema tupewe,Nimesema huko mbele kama taifa ,inaweza kuleta manenomaneo na kusababisha uvunjifu wa amani kwa kuwa kuna kajiharufu cha upendeleo fulani hivi na Ukanisa ndani ya serikali.
Wakti nchi yetu imejiepusha na Udini.
 
Kama serikali imeshindwa kutoa hizo huduma na kanisa linatoa kwanini lilisaidie japo karuzuku ili wananchi wake wasiteseke?

Yani wananchi wapate shida kisa vimaneno vya wapuuzi wachache, waeleshwe wasipotaka kuelewa waachwe.
Mbona waislamu wamepewa majengo ya tanesco morogoro kujenga chuo kikuu lakini hakuna alieleta maneno.
 
Raia wa Tanzania hakuna wapuuzi wachache,Kama madaiyake ni ya msingi serikali ianalazimika kuyazingatia.
Taifa lenye kujali hata mashoga na Wasagaji kuwa wana haki zao na wasibaguliwe,Sembuse watu wanao Imani ya kidini tena kubwa tuu.
Hakuna cha kupuuzwa kwenye Taifa makini kama Tanzania lenye viongozi makini kama Magufuli.
 
Hapo litakapo buma ndo tutajua nini kifanyie au sio?,
Maana sisi waafrika ni kama majongoo,hatugeuzi njia mpaka tugonge ukuta.
 
Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika yanaweza kutupa sura mpya tusiokuwa tukiifahamu sote, Pengine ni kwa mara ya kwanza Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ndio kinaeleza uhusika kikamilifu wa Kanisa katoliki duniani katika uhuru wa Bara la Afrika na hasa Tanganyika chini ya shirika nguli la Ujasusi la Kanisa hilo . Utafiti wa kinyaraka na machipuzi ya nera kwa mambo anuawai, ndio yaliyonihakikishia kuhitimisha katika kitabu hiki, Tunapoadhimisha kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika tunayo sababu na ni haki yetu kutambua mchango wa kila mtu alivyoshiriki katika uhuru huo, haijalishi mapokeo, Tusipoandika historia yetu, tusilaumu tukiandikiwa.

Hebu turejee kwenye Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Kwa mfano, hali ya Tanganyika kuwa eneo ka kudhaminiwa, ilisababisha Uingereza kutokubali walowezi wengi kuja hapa. Vivyo hivyo, hali ya Afrika ya Kusini Magharibi kuwa eneo la kudhaminiwa, ilizuia sehemu hii kuwa jimbo la Afrika Kusini kuwa msingi kwa uhuru wake kama nchi ya Namibia.

Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi (Jeisuiti) kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua. Lakini, lilikumbana na kiunzi/ukinzani hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya Ukristu, kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana).

Mgogoro huo ulikuzwa kwa kuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa shirika lao la kijasusi la Fabian Society, maalumu kwa minajili ya kuwaandaa Vijana katika makoloni Uingereza hususani barani Afrika, kukabidhiwa nchi zao na kwa Tanganyika Fabian Society wao walikuwa wamemuandaa Chifu David Kidaha Makwaia huku Jeisuti ya Katoliki wakiwa wamemuandaa Julius Nyerere. Rejea kitabu cha Vatican Assassins cha Eric Jon Phelps akieleza nguvu ya Vatican katika kudhibiti ulimwengu, anakazia katika harakati za ukombozi duniani hasa Afrika na nafasi ya kanisa chini ya Jeisuti.

Barani Afrika, Jesuiti ilibadili mbinu kwa kuwa dola la Kiingereza, lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani. Haikujikita kwenye dola, bali ilisimama katika muundo wa shirika likifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri shahiri, ilikuwa lazima itimie, kama ilivyoelezwa mwanzoni kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu. Kwa hiyo, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika, chini ya Udhamini wa Shirikisho la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe. Mwaka 1927 hadi 1929, kanisa Katoliki nchini, chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi wake Tanganyika, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli. Tar. 12 Februari, mwaka 1929, Zelger alistaafu wadhifa wake kwa lazima.

Ni mwaka huohuo wa 1927, ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron, maalumu kwa minajili ya kuratibu mambo ya sherehe za watu weusi pembeni ya mji, huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na akawapa jengo la ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini, historia ya Tanganyika haiwataji kinagaubaga waasisi wa AA: Rais wa kwanza, Mwalimu, Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za Mjerumani kutoka kabila la Wayao), Katibu Mkuu wa kwanza, Klest Sykes (Mzulu, Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni kutoka Afrika Kusini), Mwekahazina, Ali Ramadhan (Mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania leo bahari ya Hindi).

Hawa ndio mwaka 1927, waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933, Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho, Bw. Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948, yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest, aliyeitwa Abdulwahid Sykes.
Abdulwahid Sykes alitoka kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia, huko Burma. Aliporudi, alikuwa na mawazo ya ujana kutoka vitani, akampindua baba yake kwa vurugu na ngumi. Mapinduzi yaliyoitwa ‘ondoa wazee’. Kisha chama cha AA kikabadilishwa jina na kuitwa TAA ambapo Rais wake wa Kwanza, akawa Daktari wa binadamu Vedasto Kyaruzi (Mhaya), aliyekuwa anafanya kazi Kingorwila Mkoani Morogoro.

Huyu ndie daktari wa binadamu wa kwanza kabisa wa Kiafrika, Tanganyika. Katibu Mkuu, akawa Abdulwahid Sykes mwenyewe na Mweka Hazina akawa Dosa Azizi. Miaka miwili tu ya chama kipya, yaani 1950, Daktari Vedasto Kyaruzi, kwa ghiriba za wakoloni, alihamishiwa Sengerema Mwanza, kama sehemu ya kumuondoa jijini Mzizima leo Dar es Salaam awe mbali na harakati. Nafasi ya rais wa TAA ikakaimiwa na Bw. Adbulwahid, mpaka mwaka 1953, uchaguzi ulipofanyika na Julius Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo (Mnazimoja ya leo).

Mnamo tar. 7 Julai, mwaka 1954, Vijana (wazee wa Kariakoo) wakiongozwa na Mwl. Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajesuiti (Askofu Maranta) na Waislamu (Sheikh Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, hekima za Sheikh huyu ziliendelea kusaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwl. Nyerere ya kwenda UNO tar. 5 Machi, mwaka 1955, kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tikiti ya ndege ya kwenda na kurudi. Lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani.

Si hivyo tu, bali katika moja ya utani wa Mwl. Nyerere wenye ukweli ndani yake, aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni mabosi wake, akikumbuka malipo ya Shilingi mia sita (600/=) angali ameacha kazi ya ualimu, akiwa kijijini Butiama. Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Nyerere kuja kuiongoza Tanganyika mpya. Barua ya lugha ya Kilatini, ya kitume, Tot Tangaeque, ya Papa wa Roma, ya tar. 8 Novemba, mwaka 1984, kwenda kwa Kanisa Katoliki Tanzania, inautangazia ulimwengu kwamba Tanzania itakuwa chini ya himaya ya kanisa kwa mwavuli wa Bikira Maria Imakulata.

Miaka thelethini na mbili (32) baadae, Kanisa Katoliki Tanzania chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa, linaijibu barua hiyo kwa barua yenye kumbukumbu nambari TEC/PR/1 ya tar. 10 Novemba, mwaka 2016, likikubaliana na kuitangazia dunia kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika, tar. 9, mwezi 12 ya kila mwaka itakuwa pia siku ya kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Imakulata. MSIMAMIZI wa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA...........

Itaendelea..

Yericko Nyerere
Asante sana kwa makala hii Yericko.This explains who Nyerere really was:he was a Jesuit,and in a way this explains it all.Mwenye akili atanielewa.

Makala yako pia inaonyesha the actual position of The Catholic Church in World Politics and what it is really,a tool for the NWO cabal.
 
Back
Top Bottom