Kangi Lugola kujiunga CHADEMA?

[QUOTE=eddy; Mtungilehi alikuwa Kyerwa Kagera na si Mwibara_Musoma, Eddy usichokijua usichangie.
 
Ccm ilikuwa ikiakilisha wananchi na wabunge wasiozidi kumi. Ester bulaya, kangi lugora, James lembeli, luhaga mpina, , deo filikunjombeo, ole sendeka, Kingwangala, nk. Wakiondoka hao ccm linabki kabila moja tu (mafisadi)

Linabaki chaka tupu wazee wa ndiooooooooo
 
Haya wanakubalika waambieni wakafanye mkutano bunda na Kahama, watu wajenge chama wao warukie tu ka chura kisimani.

Utaendelea kulia lia sana na ccm ndio inazidi kubomolewa hiyo
 
Una uhakika na ulichoandika lakini...??
Esther Bulaya hakubaliki Bunda..?? na James Lembeli hakubaliki Kahama..??
Usitumie za kuambiwa tu, changanya na zako japo unazo kidogo.

Ndio hawakubaliki na viongozi wa CCM sababu wanawakilisha wananchi na kukemea ufisadi hivyo hawaenei kwa Chama Chetu CCM
 
kinachonikwaza ni kwamba wanaojiunga au kutajwa kujiunga ni wale ambao wamepima upepo na kuona either hawakubaliki na chama au wapiga kura. yaani makapi hakuna pure grain hata mmoja. feel sad to cdm

Huwazi kwa kutumia AKILI wewe, eti "makapi". Lembeli na Bulaya ni mwiba mkali kwa lichama la wezi na mafisadi wala rushwa halafu unawaita makapi?
Kipo unachotumia kuwaza ila sio akili.
 
Mnamwona kapi baada ya kuwatosa..

mkubwa nakubaliana na wewe kabisa, coz pure grain ya ccm lazima iwe na sifa zifuatazo, ufisadi, rushwa, mtu wakupenda kusifia madudu yanayofanywa na ccm, muongo, asiyependa haki, anayejali maslahi ya mabwana zake kuliko watanzania wavuja jasho. sasa haya unayouaita makapi ni wale wenye sifa opposite na hizo nlizotaja ambayo kwa vyovyote hawez survive kwny udhalim wa ccm
 
kinachonikwaza ni kwamba wanaojiunga au kutajwa kujiunga ni wale ambao wamepima upepo na kuona either hawakubaliki na chama au wapiga kura. yaani makapi hakuna pure grain hata mmoja. feel sad to cdm

CCM imeingiwa hofu, Magufuli kuwa shughuli

KUNA hofu imetanda ndani ya CCM; hofu ambayo inajaribu kufichwa mapema kwani kama mambo hayatobadilika ndani ya miezi hii mitatu hivi iliyobakia kabla ya Uchaguzi Mkuu basi chama hiki kikongwe zaidi nchini kinaweza kujikuta kikipumzishwa kutoka madarakani kwa nguvu. Dalili ya hofu hii imeonekana baada ya kutangazwa kwa mgombea wao wa kiti cha Urais Dk. John Pombe Magufuli.

Mojawapo ya mambo ambayo yametokea baada ya Magufuli kutangazwa ni kauli za kuwa yeye “anakubalika na anachagulika”. CCM imetaka kuliaminisha taifa kuwa Magufuli siyo tu anajulikana kwa utendaji kazi wake, na kuwa wananchi wengi wanampenda na wanaweza kumchagua. Kiasi kwamba wametaka watu waamini kuwa Magufuli ni Rais anayesubiria (President in waiting). Kwamba, upinzani hauna nafasi hata kidogo ya kumnyang’anya uwezekano huo.

Ukweli ni kuwa matendo ya CCM hayaoneshi kujiamini huku. Kama kweli CCM inaamini Magufuli anajulikana na kazi zake zinakubalika nchi nzima kwa nini juhudi kubwa sana inajaribu kufanywa ya “kumtambulisha”. Unamtambulisha vipi mtu ambaye tayari unaamini anajulikana, kufahamika na kukubalika? Ukiangalia utaona kuwa CCM inataka kumtumia Magufuli kukibeba chama; tatizo ni kuwa Magufuli mwenyewe – ukiondoa kukariri kwake takwimu mbalimbali – utendaji kazi wake una shaka. Tayari wizara ambayo amekalia imeshagubikwa na kashfa lukuki na hili peke yake lingetosha hata kumchafua. Akija mgombea mzuri kutoka upinzani na akajizibu hizi takwimu za Magufuli, basi Magufuli na CCM iko matatani. Yote haya yanatosha kufanya watu wajiulize mara mbili kama kweli Magufuli hatokuwa shughuli kweli kweli.

CCM imepasuka, rekodi yake mbovu, na upinzani ukimsimamisha mgombea makini, Magufuli ataweza vipi kushinda? Njia pekee ya kushinda katika mazingira ya namna hiyo ni matumizi makubwa ya nguvu, vyombo vya dola na hata kuliingiza jeshi katika siasa kama walivyofanya chini ya Jenerali Shimbo mwaka 2010. Vyovyote vile ilivyo hata hivyo kuna hofu imetanda kwa CCM; hofu kama vile wingu zito la mvua lenye dalili ya radi na ngurumo. CCM hawajui sasa wafanye nini zaidi ya kuombea Magufuli aweze kuwaokoa. Akishindwa je Hili ndilo swali la kuogopesha zaidi kwa kila mwana CCM

Chanzo: Raia Mwema (22, July 2015)
 
huu ndo wakati mzuri wa ccm kuiteka chadema nzimanzima.
tuma makada 150 wahamie chadema na watapewa nafasi ya kugombea ubunge na wakipita wanakuwa wamo kwa maslahi ya ccm.

inaitwa infiltration

huko Mwibara chadema haipo? Hili jimbo lilikuwa la Mutungerehi nae akajichanganya akaenda TLP, yaani tabu tupu.
Fikiri Vema,
Kuanzia Karukekere Hadi Mgala, Mwisenyi Hadi Kisorya, Mchigondo Hadi Mwiruruma Chadema Inatamba Ccm Wataponea Wapi?
 
Fikiri Vema,
Kuanzia Karukekere Hadi Mgala, Mwisenyi Hadi Kisorya, Mchigondo Hadi Mwiruruma Chadema Inatamba Ccm Wataponea Wapi?

Umenikumbusha mbali haya maeneo, Nyamitwebili,mahyoro, Nansimo. Karukekere kuna watu wengi sana na upinzani una nguvu historically!!
 
huko Mwibara chadema haipo? Hili jimbo lilikuwa la Mutungerehi nae akajichanganya akaenda TLP, yaani tabu tupu.
eddy acha kuchanganya watu, Mwibara iko wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara, Mutungirehi ni Muhaya wa Kagera. Siasa za haya haya maeneo mawili ni za kikabila mno tofauti na maeneo ya miji mikubwa. Mwibara watachagua Mjita au mtu mwenye nasaba na makabila ya huko. Mkoa wa Kagera kwa wahaya kama wewe ni mtu wa kabila jingine ni vigumu sana kuchaguliwa kuwa kiongozi wao. Nenda hata Halmashauri zao, karibu wote ni wenyeji wa mkoa ule, yaani ofisini ni lugha inayotumika ni kikabila tu.

Ikizingatiwa kuwa hii ni mikoa ya watani wa jadi kama "Mnyama" na "Kandambili"
 
Last edited by a moderator:
Salam Wakuu.

Kwenye MAWIO la leo, page 2 kwenye story ya UKAWA WAMFUKUZA ZITTO kuna habari ndani ya hii story kuwa Mh Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara leo anatarajia kujiunga na Chadema pale Mwanza. Yeyote mwenye uhakika wa hii taarifa atumwagie tafadhali.

Acha uongo Mtungireh alikuwa mbunge wa Kyelwa karangwe, ambapo kwa sasa linashikiliwa na Katagira kutoka CCM. Unaropoka wakati hata data ndogo tu hiyo inakushinda.
 
Ni kweli wengi hawakuwa liking com ila kwa sabab kuu moja tu. Wamekua critical kwenye maswala yenye maslahi mapama kwa taifa eh. Lembeli... Hii sifa sio ya mwanaccm. Kwao ili uqualify ni lazma uwe mpuuz flanivi ukubali kunyonya wananchi, wizi, rushwa na upuuz mwingine. Nafurah kuona hili Coz urafiki na mwez nawe kuna sku utaqdhibiwa tu
 
huko Mwibara chadema haipo? Hili jimbo lilikuwa la Mutungerehi nae akajichanganya akaenda TLP, yaani tabu tupu.

Ndugu, niweke habari hii kwa uhakika. Ukweli ni kuwa Jimbo la MWIBARA siko aliko kuwa Mutungirehi. Mwibara iko MARA. Ukweli ni kuwa Jimbo hili liko Wilaya ya Butiama, kwa Nyrere. Mutungirehi alikuwa Mbunge wa KYERWA. Iko Mkoa wa Kagera. Sasa ni Wilaya, lakini wakati wa Benedikto, Kyerwa lilkuwa Jimbo katika Wilaya ya Karagwe.
 
huu ndo wakati mzuri wa ccm kuiteka chadema nzimanzima.
tuma makada 150 wahamie chadema na watapewa nafasi ya kugombea ubunge na wakipita wanakuwa wamo kwa maslahi ya ccm. inaitwa infiltration
Wataziona hasira za watanzania wapenda mabadiliko. Au unadhani watanzania hawawezi kuchukua maamuzi magumu? Usaliti wa aina yoyoye hauwezi kuvumiliwa mahali popote.
 
eddy- Mtungirehi alikuwa Kyerwa siyo Mwibara. Na wakati akiwa mbunge alikuwa tlp hiyo hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom