Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,775
- 3,610
Mchezo wa kanga moja maarufu kama kanga moko, umewatisha wabunge. Hali hiyo ilitokea bungeni jana wakati wabunge hao walipokuwa wakichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Akichangia ktk mjadala huo, Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Getrude Lwakatare (CCM), alisema kuna haja Serikali kuangalia mwenendo wa muziki huo, kwa kuwa unakiuka maadili ya Kibongo.
"Hebu ngoja nizungumzie huu muziki wa kanga moja, huu ni mchezo mbaya sana, tena kanga inalowanishwa na maji halafu binti anaivaa.
"Baada ya kuivaa anaanza kufanya manenguo, hivi itakuwaje kama mwenye umbo nene akiivaa na kunengua, ni aibu tupu hapa.
"Kwa hiyo, naomba Serikali iangalie namna ya kudhibiti hii kanga moja kwa sababu inachezwa kinyume cha maadili," alisema Dk. Lwakatare.
Kwa upande wa Mbunge wa Viti Maalum, Mwanamrisho Taratibu Abama (CHADEMA)...alisema muziki huo unafaa kupigwa marufuku kwa kuwa unawadhalilishwa wachezaji.
"Huu muziki wa kanga moja haufai, nasikia mara nyingine wanauita kanga moko, huu ni udhalilishaji lazima upigwe marufuku.
"Pamoja na kwamba unakiuka maadili ya Kitanzania, wanaume wanaupenda sana kwa sababu kila unapochezwa wanajaa ukumbini, Serikali iupige marufuku huu," alisema Abama.