Kanga - Matumizi yake, Misemo na Vijembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanga - Matumizi yake, Misemo na Vijembe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tausi Mzalendo, May 31, 2011.

 1. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asante MKJJ,
  Khanga zina matumizi mengi sana.Yafaa tuanzishe thread ya "Matumizi ya Khanga"
  Baadhi ya matumizi ni:
  1.Kutoa jumbe mbalimbali
  2.Ni ishara ya mambo mbalimbali hasa ya mapenzi
  3.Ni vazi lenye matumizi mengi ( Versatile) - huvaliwa na kina mama kama nguo bila hata kushonwa, Hushonwa, hutumika kama mbeleko kubebea watoto, hutumika kama matandiko kitandani,
  4.Ni zawadi nzuri
  etc etc!!

  Kanga siku hizi zinatumiwa sana hata na wanasiasa na imekuwa kama sehemu ya zile Takrima. Lakini pia kanga mitaani pia ni kama sms zenye kutuma ujumbe mfupi uwe wa kheri au wa shari. Labda tuulizane ni jumbe gani tumewahi kuziona au kuzituma hasa sisi kina mama kwa kutumia kanga. Rangi gani tunapenda, n.k Na kwanini wakati mwingine tunanunua kanga ambazo hatuzivai alimradi tunaweka kwenye "collection" zetu za kanga?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka moja niliwahi kusoma zamani "Umeyataka Mwenyewe"..

  Sasa hadi leo sijui ujumbe huo ulikuwa unamhusu nani, kwanini na kwa vipi. Nilitaka hata kuuliza "imekuwaje"? Kwa kweli kanga nyingine huacha maswali bila kujibu wala kujaribu kujibu.

  TM umepotea saaaaaaana assante kwa hii ya kuunga mkono ile. Ngoja tusubiri Khangaologists waje kutupa elimu hapa.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Raha ya raha ni kupata raha zaidi

  Wachome wachomeke
   
 4. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asante NN, unadhani misemo hiyo ina maana gani?

  "Shanuo baya pale linapokuchoma" - huu ni ujumbe na kijembe kwamba kitu ni chema hadi pale kitakapokudhuru
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Tafsiri ni jinsi wewe msomaji utakavyotafsiri. Hiyo ya raha ya raha ni kupata raha zaidi nadhani inamaanisha ukiamua kula raha basi kula kikwelikweli na usisaze kitu.

  Wewe umeitafsiri vipi kwani?
   
 6. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Nipo MKJJ ila majukumu tu yamenizidia.
  Ujumbe kama huu utapata maana tu endapo utaweza kujua huyo mvaaji kamvalia nani.Jumbe nyingine ni za jumlajumla kwa watu wote lakini kama huu uliouweka hao juu una mlengwa.Laiti ungelikuwa na "ujasiri" kumpeleleza mvaaji ungejua kamlenga nani na kwanini.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  duh.. hii ya kweli au umejitungia tu mbele ya safari.. inabidi nikushtukie hapa kwa kweli.
   
 8. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na tafsiri uliyoitoa.Ule msemo mwingine wa "wachome wachomeke" - Hii ni rusha roho hakika!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nadhani kati ya messages zoote ambazo nimewahi kuona hii inakumbukwa sana; sijui kama ina "double meaning" au ina "reverse meaning"..
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hehehehee Mwanakijiji bana. Kwani hizo zingine hazitungwi? Na kwa nini unishtukie? Ni kwamba huamini au?
   
 11. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hapo zamani na inawezekana bado yanaendelea ni kwamba jirani wakigombana basi mmoja hwenda kutafuta kanga yenye ujumbe maalumu wa kumfumba jirani yake. Jioni mwenyewe huzivaa zile kanga na kukaa kibarazani nje, na huhakikisha kwamba ule ujumbe jirani anausoma.

  Jirani naye akitaka kujibu mapigo basi na yeye hutafuta kanga yenye msemo wa kujibu na yeye hufanya vile vile. Basi inakuwa malumbano tu kwa misemo ya kanga.

  Kanga niliyovaa leo imeandikwa 'hata na wewe nawe' nilipewa kama ujumbe kwamba nilisahau kumwalika mtu kwenye arusi basi nikaletewa zawadi hiyo. Baadae ilibidi niombe radhi.
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ndo maanake! Khanga na rusha roho ni pete na kidole.
   
 13. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hivi mnakumbuka kuna ule msemo wa kwenye kanga "ALAA,KUMBE" kwa kweli mpaka leo sijawahi kuelewa maana yake
   
 14. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maneno ya kwenye kanga huzaliwa kila kunapokucha kuendana na matukio kwenye jamii. Hivyo kama NN katunga basi ni sawa kabisa na pengine wengine nao waje na misemo mipya - nani anajua itaweza kujikuta kwenye kanga karibuni/

  Asante BM- nadhani huu mtindo wa kuvaa na kuvaliwa, kutoa ujumbe na kujibiwa husaidia kufanya biashara ya kanga iwe nzuri sana.Wafanya biashara wanafaidika na vijembe hivi! Lakini nasikia kwenye familia nyingine kanga zimepelekea watoto kupata utapia mlo maana mama akiachiwa pesa, zinaishia kununua kanga badala ya chakula! Kanga zina mambo kweli.

  Khanga na taarabu ni njia nzuri sana ya kupeleka jumbe za vijembe a.k.a rusha roho!
   
Loading...