CCM tayari imeshawatia ujinga watu wa kanda ya ziwa sera ya "devide and rule" imeanza kufanya kazi kwa kuwajaza ukanda poleni ila mtakuja kujitambua wakati wenzenu tuko mbali.
Mkuu Ngokongosha, japo siungi mkono aina yoyote ya ubaguzi, uwe wa kidini, jisia, ukabila, ukanda, rangi, kipato ahata umri, etc, na wengi watakuona wewe ni mbaguzi, sisi waumini wa ukweli halisi jinsi vile ulivyo, tumekuelewa!.
Tukubali tukatae, kuna udini mkubwa kwenye siasa zetu!, huu ni ubaguzi!, namna ya kuufuta sio kuunyamazia, bali kuuzungumzia wazi wazi kinaga ubaga, na ikibidi kuuzuia kwa makusudi kabisa!. Kuna watu wanadhani jina la Magufuli limeingia kwa bahati mbaya tuu!. Kuna vitu kuna watu waliviangalaia na waliisha amua kabla, hivyo wakaamua 2015 ni Magufuli. Bahati nzuri mimi ni mmoja wa watu tuliodokezwa kuhusu Magufuli, na niliwaeleza watu humu Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli!. kuna sababu zilitolewa why ni Magufuli!.
Nimefurahi ulipozungumzia kukubalika kwa Magufuli kama John Pombe Magufuli na sio eti kwa sababu anatoka Kanda ya Ziwa, kwa sababu ingekuwa watu wa Kanda ya Ziwa wanaukabila kihivyo, wangemchagua Cheyo kwa sababu amewahi kugombea urais!!, kitu ambacho ni ukweli kabisa Magufuli anakubalika kwa sababu ni Jembe la ukweli!.
Kule nyuma sii mara moja wala mbili, nimewahi kuuliza humu kuhusu mambo haya haya ya ukabila, udini na ukanda, nikaishia kunyooshewa vidole kuitwa mbaguzi, lakini huu ndio ukweli wenyewe, watu makini wanaoijua sayansi ya siasa, hili wanalijua ndio maana wakaja na jina la John Pombe Magufuli.
Kanda ya Ziwa ndio determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, kitendo cha CCM kumteua Magufuli, kitapelekea mgombea wa CCM sio tuu kupata ushindi wa kishindo cha ajabu, bali pia atayarejesha CCM, yale majimbo yote ya kanda ya Ziwa yaliyoshikwa na Wapinzani!.
Mimi kwa sababu siku zote ni muumini wa ukweli jinsi ile ile ulivyo, sipati taabu kuitwa mbaguzi kwa kuusema ukweli, wale unaopenda kuujua ukweli huu ninaozungumzia hapa, mnaweza kupitia nyuzi zangu hizi.
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real?
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!
Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Siasa za Tanzania?!.
Pasco.
Kwa kweli nawapongeza sana kuanzia Mwanza, kwasababu sasa hatimaye Chadema imejitambua na kujua kanda determinant za ushindi kwa uchaguzi wa urais Tanzania ni kanda gani, hivyo wameanzia hapa.Hatimaye kile kitendawili cha Mikutano ya hadhara sasa rasmi kimeteguliwa , hii ni baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kutoa Ratiba yake .
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Itifaki wa Chama hicho John Mrema imedai kwamba , Jiji la Mwanza limeteuliwa kuwa la Kwanza kwa Chadema kufanya mkutano wake wa Hadhara , Mkutano huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya Kitaifa ya Mikutano ya hadhara tangu kuvumbuliwa kwa Tanzania utafanyika tarehe 21/01/2023 .
Mungu ibariki Chadema
Mwaka 2012, nikapandisha uzi huuWanabodi,
Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja yenye impact ikiwemo kuyashika majiji makubwa katika mikoa the big five!, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala, ili kikabidhiwe nchi, kitawale, Chadema bado kimekaa kichama harakati, hivyo kuna wengi wanakiona kama bado hakijakomaa kiasi cha kukabidhiwa ikulu yetu!.
Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu kwa sasa japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi kuliko ki chama tawala, na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.
Kwa vile CCM imechokwa na imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu Chadema kuongeza offensive ili kuisindikiza CCM kaburini, kwa kujipanga kimkakati ili muwe na sura ya kitaifa, kwa kuonyesha Watanzania kuwa mmekomaa na mko tayari kutawala, hivyo Watanzania watawamini watawakabidhi nchi mwaka 2015.
Sehemu muhimu kabisa kwa Chadema to keep watch kuhakikisha hamuiachii ni hiyo Kanda ya Ziwa ambayo imeipokonya CCM na kuishika, hii ndio Kanda determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii. Aliyeishika Kanda ya Ziwa ndio rais wa Tanzania. Hivyo CCM imeumia sana kupoteza Kanda ya Ziwa na wataelekeza all it might powers to reclaim what it has lost, hivyo Chadema itumie uwezo wake wote kulinda what it has!.
Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.
Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, as a businessman, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanyabiashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu vya kuonekanika yaani assets kama magari, mavazi, etc
Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio ku invest kwenye vitu. Chadema must invest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come kwa kutumia reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Chadema lazima ifanye recruitment ya able people, watakaokuja kuendesha serikali ya Chadema. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, it's a loss making venture kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni in for profit making. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma technocrats. Chama kishikwe na wanasiasa watendaji sio wanasiasa wafanyabiashara. Chadema iwekeze kwenye watu na kupanua mtandao wake hadi vijijini, ili kwenda kuiongoa CCM kuanzia kule chini kabisa kwenye mizizi yake ambako ni kule kwenye mashina. Chadema imiliki media yake yenyeshe for mass mobilization na sio kutegemea mikutano na maandamano, huko ni kuendeleza uanaharakati, Chadema inatakiwa kukaa mkao wa kutawala, ikitangaza kitu, kinafika Tanzania nzima!.
Paskali
Sasa Chadema ndio wanaamka kujua nguvu ielekezwe wapi, huu ni mwanzo mzuri!, tatizo la tonge hilo, waliolishika tonge mdomoni wanajua, jee watakubali kunyang'anywa tonge mdomoni?Wanabodi,
Determinant ya Rais wa Tanzania ni Kanda ya Ziwa.
Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 10!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!, hivyo CCM kwa kulitambua hili, itatumia nguvu yake yote, all its mighty powers by all means, by hooks and crooks kuyakomboa majimbo haya matatu ya Kanda ya Ziwa, na naomba mshishangae, kama ili kujiokoa, CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa hongo kubwa kabisa ya mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Laurent Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais as long as atatoka Kanda ya Ziwa kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!, the end justifies the means.
Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana kabisa kutokea kama upinzani utajitambua kwa kushikilia kwa makini kile kilicho mkononi na kuongeza juhudi za kuimililki kanda ya Ziwa, hivyo vita kuu ya kisiasa nchini Tanzania kuelekea 2015 ni nani ataimiliki Kanda ya Ziwa. Chadema ikifanikiwa, CCM inapigwa chini, ila CCM ikifanikiwa kuikomboa Kanda ya Ziwa, then 2015 ni CCM tena, na kitakacho fuatia kwa CCM ya 2015 ni kuikomboa Kanda ya Kaskazini na kusema ukweli hii ndio itakuwa kazi ngumu kweli kweli, ila kama itatumika ile 'universal language', kuna msemo "hakuna mkate mgumu mbele ya chai", mkate hata uwe mgumu vipi ukiuchovya ndani ya chai, unalainika!
Tuache Siasa za Ukanda na Ukabila, au Tuzidumishe Ili Mtu wa Kanda/Kabila Yetu Ndie Ashinde?.
Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za Ukanda, zitajenga chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane kwa hoja huku tukipendana!.
Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Bungeni Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali sana tuu kwa dhati na kupongeza kwa ushindi, huku nikiendelea kushikamana na Sioi kwa sababu ni rafiki!.
Wito Kwa Watu wa Kanda ya Kaskazini
Wito wangu kwa nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, Kanda yenu ndio imependelewa sana, inaongoza kwa mashule na wasomi, inaongoza kwa mahospitali!, KCMC, Mawenzi, Kibongoto, Mt. Meru, Seliani, Dareda, etc, Inaongoza kwa vivutio vya utalii, Mt. Kilimanjaro, Mt. Meru, Serengeti, Ngorongoro, Seronera, Manyara, Inaongoza kwa barabara za lami hadi vijijini, inaongoza kwa umeme vijijini, inaongoza kwa maendeleo, inaongoza kwa kutoa wanawake wife material, ukioa mchagga umeoa maendeleo, hivyo msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake yote ya CCM, kulea rushwa na ufisadi na kutuletea umasikini na kulea ujinga kwa kuutumia kama mtaji wake wa ushindi, pia kuna mema na mazuri yake mengi ambayo CCM imelifanyia taifa hili ikiwemo kutuletea maendeleo japo kiduchu, lakini pia imetuletea hazina ya amani na utulivu ambazo ni tunu kubwa kuliko maendeleo, hivyo tuichukie CCM kwa mabaya yake na kupenda kwa mema na mazuri yake!.
Wito Kwa Wa Kanda ya Ziwa.
Tusikubali kutumiwa kama ngazi ya wengine kupandia kisiasa, kwa vile na mimi ni mtu wa Kanda hii na sisi ndio determinant ya nani anashinda na kukikalia kile kiti cha ikulu yetu, tusikubali kuendelea kutumika tuu kama ngazi kwa wengine kupandia, au kuendelea kuwa na upendo wa mshumaa kumulikia wengine huku kwetu kunateketea, Kanda hii ndio Kanda yenye watu wengi, ndio Kanda yenye mijitu yenye nguvu inayokula na kushiba, ndio Kanda tajiri kuliko Kanda zote, ndio yenye madini ya dhahabu na almasi, ndio wenye Ziwa Victoria lenye samaki watamu Sato, tusikubali kutumiwa kama dodoki kuwasafishia wengine au dekio baada ya deki linatupwa kule, sisi tuna kila aina ya utajiri lakini very unfortunately watu wetu ni masikini wa kutupwa!. Angalia wenzetu wa Kaskazini mbona wameweza kulibwaga hili lidubwana na wanapata maendeleo, na sisi tuamue kulibwaga unless kama 2015 atakuwa ni mmoja wetu!.
Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!
Wasalaam.
Paskali