Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, May 1, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,600
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Kama kawaida yangu, nipatapo fursa, hupita huku na kule na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa kada tofauti. Kwa takriban siku 3 zilizopita, nimepata fursa ya kutembelea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo ndiyo inayo dorminate Kanda ya Kaskazini, kiukweli pande hizi CCM ina hali mbaya sana, huku CCC Imechokwa sana mpaka basi!.

  Kama CCM Imechokwa, Mbona Inachaguliwa na Inashinda?
  Siku zote nimekuwa nikisema humu, kuwa kuna baadhi ya maeneo CCM imechokwa ila bado CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi sio kwa sababu ya kupendwa au kukubalika sana, hapana!, CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi kwa sababu ya mazoea tuu wengi wakiichagua CCM kwa sababu ndicho chama pekee walichokifahamu tangu wamezaliwa, na wengine wakikichagua CCM kama asante ya kutuletea uhuru kupitia TANU, na idadi kubwa ya walio vijijini, wamekuwa wakiichagua CCM kwa ignorance tuu ya elimu ya uraia!. Sasa wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu kama asante ya kutupatia uhuru, kwa sasa ni oldguards, wamezeeka, wanazidi kupungua na wachache waliobakia their days are numbered!. Wale wengi waliokuwa wakiichagua CCM kwa ignorance, sasa wameanza kuerevuka na wameanza kuamka!.

  Tabia za Maeneo CCM ya Stronghold za CCM na Stronghold za Opposition.
  Stronghold ni eneo lenye nguvu ya chama fulani. Mfano CUF Stronghold yake ni Pemba, Chadema Stronghold yake ni Kanda ya Kaskazini, na CCM inamiliki maeneo mengine yote. Tabia za maeneo wanayochagua wapinzani, ni maeneo yenye maendeleo, watu wake wanajiweza kidogo kiuchumi hivyo wamesoma na kuelimika, hawawezi kudanganyika kirahisi rahisi. Kanda ya Kaskazini, ndio inayoongoza kwa high literacy levels ikifuatiwa na Bukoba, Mbeya Mwanza na Iringa, majiji yote yameshikwa na upinzani sababu watu wana nguvu ya kiuchumi hivyo wameelimika na kufuta ujinga hivyo wamechagua upinzani.

  Maeneo ya Stronghold ya CCM, ni maeneo yote yenye umasikini uliotope na low literacy levels, hivyo ni rahisi kudanganyika na kuna wanaoichagua bila kujua wanachagua nini!. Hivyo CCM itazidi kuchaguliwa as long as umasikini unaendelea.

  Majaaliwa ya CCM Kanda ya Kaskazini
  Kwa mujibu wa kada mbalimbali za wale niliozungumza nao, wamenithibitisha pasi shaka kuwa hakuna jinsi yotote wagombea wa CCM wa kanda hii kama Ole Sendeka, Ole Medeye na Ole Nang'uro wataweza kusalimika, sehemu pekee salama kwa CCM mpaka sasa ni Jimbo la Monduli tuu kwa sababu ya Lowassa!, na maeneo ya upareni nako CCM bado ni salama kwa sababu ya umasikini uliotopea, lakini kungine kote, Kanda ya Kaskazini, CCM haina chake, CCM haipati kitu!.

  Kama kasi ya upepo wa mwamko kama huu wa Kanda ya Kaskazini kuichukia CCM, utaingia kanda ya Ziwa kwa kasi hiyo hiyo, then amini usiamini, hakuna jinsi yoyote ya kuiokoa CCM isipigwe mwereka uchaguzi wa 2015, CCM inakwenda kupigwa chini!. Kwa vile hili CCM pia wanalijua, mtashuhudia juhudi za ziada kwa CCM kuelekeza nguvu nyingi na nguvu kubwa ya ziada
  kwenye kanda hii ya Ziwa na kwa vile tayari kuna majimbo matatu Kanda ya Ziwa yako chini ya Chadema, kama Chadema itaendelea kuyas
  hikilia na kuongeza kasi ya Chadema kukubalika na kupendwa kanda ya Ziwa, kiukweli kabisa, CCM itakuwa kwenye hali mbaya sana kwenye kanda hii hivyo inakwenda kuandika!.

  Determinant ya Rais wa Tanzania ni Kanda ya Ziwa.
  Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 10!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!, hivyo CCM kwa kulitambua hili, itatumia nguvu yake yote by all means, by hooks and crooks kuyakomboa majimbo haya matatu ya Kanda ya Ziwa, na mshishangae, ili kujiokoa, CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!.

  Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana kabisa kutokea kama upinzani utaimlilki kanda ya Ziwa.

  Tuache Siasa za Ukanda na Ukabila, au Tuzidumishe Ili Mtu wa Kanda/Kabila Yetu Ndie Ashinde?.
  Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane kwa hoja huku tukipendana!.

  Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Bungeni Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali sana tuu kwa dhati na kupongeza kwa ushindi, huku nikiendelea kushikamana na Sioi kwa sababu ni rafiki!.

  Wito Kwa Watu wa Kanda ya Kaskazini
  Wito wangu kwa nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake yote ya CCM, kulea rushwa na ufisadi na kutuletea umasikini na kulea ujinga kwa kuutumia kama mtaji wake wa ushindi, pia kuna mema na mazuri yake mengi ambayo CCM imelifanyia taifa hili ikiwemo kutuletea maendeleo japo kiduchu, lakini pia imetuletea hazina ya amani na utulivu ambazo ni tunu kubwa kuliko maendeleo, hivyo tuichukie CCM kwa mabaya yake na kupenda kwa mema na mazuri yake!.

  Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!

  Wasalaam.

  Paskali
  Kirua Vunjo, Moshi Vijijini
  Rejea
  Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni ...
  Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye ...
  Ni upuuzi kuwagawa watanzania kikanda,kikabila na kidini ...
  Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? | Page 7 ...
  Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...
   
 2. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Samahani mkuu tukumbushane kidogo ccm ndo chama gani.Sisi tunajua chadema na tlp tu usijekuwa unachanganya na vya nchi za jirani manake huko kidogo ndo sijui vyama vyao
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ivi pasco umenunuia jino jipya ulilopoteza ajalini? KARIBU TENA ARUSHA.
   
 4. h

  hans79 JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  chema hujuuza kibaya chajitembeza, kwa hiyo jambo na mwishowe.uwongo wa ahadi kwa kizazi hiki cha teknojia mpya ni ngumu kueleweka, tenda jema kwa wananchi uone kama utapigwa mawe.
  kama ubinafsi ndo utawala wao lazima wananchi watakuchoka na kukuchukia pia.mfano mazao yauzwe kwenye vyama vya ushirika kinachofuata ni kuzungushwa kuhusu malipo, je hapo wategemea nini ?
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hebu taja baadhi ya sehemu ulizopita na kuhojiana na hao watu.
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,812
  Likes Received: 36,903
  Trophy Points: 280
  :tape: M4C with no apology.
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Paso bwana haya kaka sina la kuongeza zaidi ya kusema nchi imefika tulipo kwa sababau ya CCM
  tungekuwa mbali zaidi kama tungekuwa na mseto kama US na UK.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Leo Pasco nadhani ulitulia wakati unazipanga point zako,
  Uchambuzi wako ni makini na ninakubaliana na wewe licha ya uswahiba wako na Lowasa sidhani kama umemdefend kuhusu jimbo la Monduli ni kweli Lowasa pale amejenga mizizi na ni yeye ndiye mwenye ushawishi mkubwa wa kumu endorse next Mp kama yeye Lowasa hatogombea tena ubunge

  Kuhusu CCM kuchokwa hili wala halihitaji uwe Political Analyst na uzuri wake hata viongozi waandamizi wanalifahamu hili na ndio maana sasa chama kinajiendesha katika mfumo wa Auto Pilot.

  Nikiangalia kuhusu kanda ya , Hii mikoa ya Mara, Shinyanga na Mara hapa somo limeshaeleweka na hasa watu wa Mara wala hawahitaji hamasa maana wao walishaamuwa siku nyingi kwamba CCM sas basi.

  Katika kanda ya Ziwa sehemu ambayo nadhani inapaswa kufanyika kazi ya ziada ni mkoa wa Tabora, hawa wanyamwezi hata siwaelewi elewi akili zao zimekaaje!!

  Ukija mkoa wa Kagera hapa napo somo limeeleweka ila bado kuna kazi inatakiwa kufanyika, mfano hai ni Jimbo la Bukoba Mjini matokeo ya Urais aliongoza Dr Slaa, lakini Ubunge akashinda wa CCM Balozi Kagasheki, kwa maono yangu Chadema inaweza kuscore vizuri sana kanda ya ziwa next Election.

  Tatizo lililopo mpaka sasa hivi ni huu ukanda wa umakondeni na uzaramoni, huku ndiko kunapaswa kuwaweka sawa wazawa wa maeneo hayo hili waunge mkono na mbaya zaidi CUF hizi ndio ngome zake, maana hakuna siri kwamba sehemu hizo wanaamini kabisa kwamba CUF ni chama cha waislamu na jamii kubwa ni waislamu katika hayo maeneo.
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Pasco hayo unayoyaona yanachagizwa na tamko la UVCCM la Pwani kuwa rais hatatoka Kaskazini. Kanda ya Kaskazini ni kama wanasema ngoja tuone, usije shangaa madiwani wengi kama si wote wa Arusha, Kilimanjaro na Manyara kuisusa CCM.
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  wanaichukia ccm kwa sababu tanzania inarudi nyuma -ve development.eg mtoto kafaulu darasa la 7 hajui reading,writting
   
 11. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu Pasco.
  Umetoa analysis nzuri na way forward.
  Sasa ni jukumu la waratibu wa M4C kuona wanaweza vipi ku-buy your ideas/opinion.
  Kwa kuwa mh. Lema na mh. Slaa wapo humu, hopeful watakuwa wasikivu na kuweza kuyafanyia kazi.
  Umetoa analysis nzuri mkuu.
   
 12. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  nafikiri kuwa na akili kwamba kanda ya ziwa pekee ndo wanaoweza kuipiga chini ccm ni akili za bata. mambo ya kuwagawa watz kikanda hayo ni ubaguzi kama ule wa wakikuyu na wajaluo tu. wewe huna tofauti na makaburu kabisa. kwanini unasema kanda ya ziwa ndo watu wengi, wakati wasukuma ni watu wazuri sana wasio na ubaguzi kikabila kabisa? wewe unataka kuwapandikiza icho kitu? kama wasukuma wangekuwa na mawazo kama yako hii nchi wangeshaisambaratisha..

  tz yote kwa pamoja yaweza kuiangusha ccm. anglaia iringa, pale mjini palishawahi kutawaliwa na NCCR mageuzi kwa term nzima, tena mbunge wake kibasa alikuwa headmaster wa secondary ya mwembetogwa. angalia sasaivi chadema ndo inatawala, angalia mbeya, chadema ndo inatawala, watu kule wako tayari hata kumpa mcheza bongo fleva alimradi tu ccm wasipate ubunge, kuna watu wameshamvurumishia mawe kikwete zaidi ya mara mbili. kusini kule songea nako ccm walishinda kwa shida, morogoro wanatawaliwa na abood na yule mwenye mabasi wa gailo. kitu cha muhimu hapa ni kufanya uamsho wa watz wote, ili ccm ikijakushindwa uchaguzi, hata mzizi tu usibaki, chama hicho kife jumla. kisijekufa ukanda wa kaskazini halafu ukanda wa kusini kikawa bado kina mizizi...kampeni tunatakiwa kufanya nchi nzima.

  kwa sasa kilimanjaro yote, mwanza, arusha yote, iringa, mbeya na miji mikubwa mingi chadema tumeshatawala, cha muhimu sasa ni kuhakikisha majimbo tuliyoshinda hayapokonywi, na twabidi tuongeze majimboi mengi zaidi. mwaka 2015 lazima tuchukue nchi tuanze kunya maziwa na asali.
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu Hute.
  Ili swala ni kama 'war game'. Katika battle kuna 'strategic points' ambazo ukimpiga adui yako, chance ya kushinda vita inakuwa kubwa (sio kwamba umeshinda vita).
  Sasa kwenye siasa, eneo la kanda ya ziwa ni strategic one.
  Ukiweza kukubalika eneo ili, chance ya kushinda uchaguzi inakuwa kubwa.
  What we are talking here, are strategic issues.
   
 14. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pamoja na haki yako ya mtazamo tu, mimi huangaliaga ndani ya mistari; ujumbe unaoutoa una taswira mbili.

  1. Hukutegemea kuwa kanda unazozitaja zinaweza kuigeuka CCM

  Jibu langu kwa hili weka kinyume CCM imewageuka watanzania kwa kuwasahau kabisa katika maisha yao ya kila siku. Kwa hiyo CCM imetoa elimu kwa makusudi isiaminiwe kwa mifano hai ya kuwapora imani na mategemeo waliyokuwa nayo watanzania. NAKUHAKIKISHIA SI UKANDA angalia Tandahimba ni kanda gani?

  2. Unatafuta suluhisho la maovu ya CCM yaliyojenga chuki.

  Hapo nawaelewa Watanzania kuwa ni wanadamu wakawaida viumbe wa Mungu waliojaliwa uelewa na hiari ya kusema SASA BASI baada ya kufanyiwa waliofanyiwa na CCM ambayo unayajua vema.

  Uchambuzi wangu

  Chaguzi zote hadi sasa kuna neno mvuto linajitokeza, mimi najifunza kuwa linahusu wajihi zaidi kuliko dhamira ya uwajibikaji. Wajihi huchujuka kama ua nadhani ndiyo yanayoipata CCM. Dhamira ya uwajibikaji inahusisha ahadi na matendo; wazungu wanasema TO WALK THE TALK. Hiki ndicho kinakosekana kwa CCM (labda na wewe) kwa sababu ukichulia kuwapa matumaini watu juu ya maisha bora halafu kila siku inakuwa afadhali ya jana nani atavumilia?

  Mifano mingi sana mishahara midogo na tofauti kati ya wafanyakazi, wakulima kuhujumiwa na wafanyabiashara wa kati kwa msaada wa utawala wa CCM huna haja ya kutambulishwa kumjua mbaya ni nani.

  Kwa kiwango CCM ilipofikia hata ukienda nyumba kwa nyumba kutoa maelezo yako utasikilizwa na sikio la kushoto yatatokea sikio la kulia kwa kukosekana WALKING THE TALK. Kusini mwa TZ wanapokudharau ni pale kauli zako zisipoendana na matendo yako.

  Kauli za CCM na hata wewe Pasco mziainishe na kuzilinganisha na matendo yenu. Hata angalau mseme mnaweza nini na hamuwezi nini maana kwa sasa mmebakia kuhodhi dola mnachoongea tofauti na mnachoweza kufanya. Wenye akili wamewagundua kuwa ni ...................
   
 15. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Njoo na kanda ya ziwa ushuhudie mwenyewe!!

  Siwezi kuisemea kanda ya nyanda za juu kusini!!

  Magamba you should eat like Gluttons for your days a deteriorating!!
   
 16. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Watu wakaskazini huwa hawapendi porojo za ccm
   
 17. s

  salisalum JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  I am sorry to say this, you seem to be discriminatory. You think change can came as a result of dividing this country into sections of tribes and regions. I am not sure which political party stands for such dirty politics as you've displayed in your thread. At no single time in history of our country we have ever conducted any census categorizing people according to their tribes. The lake zone as you have put in your thread is inhabited by a large number of tribes, probably the only country section lived by a more diverse community than any other part of our country. To say that Sukumas are 6 million is a skewed opinion made purposely to propagate your tribalistic thinking. I will be very sorry if there is any political party sympathizing with such politically corrupt inclinations nor strategies to effect change in this country by dividing it on tribal sections. Any political party thinking this way will be hastening its demise.

  True political change in this country will only came through independent voters (who are more in numbers than a total sum of all citizens with membership in the existing political parties). These are people who sway instantaneously, they are strongly influenced by current issues and reality on the ground during the material time. These include the young and elderlies, men and women of all classes and ages from all geographical areas of this country. Many who voted in the recent by-election were elderlies and the opposition side won. So discriminating our population on bases of gender, age, etc. is immaterial. If a political party lacks support in certain sections of the country the reason isn't because of the predominant age or tribe residing there. Rather it may be due to the fact that the political party in question hasn't done its homework there. Ref to the Chadema Operation Sangara in Lake zone prior to 2010 election. Such and other more creative strategies will improve voters/civic education. We need to see more of that rather than your cheap tribal sentiments you have put across.
   
 18. M

  Molemo JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco uchambuzi wako umetulia.Lakini hujatutendea haki watu wa nyanda za juu kusini.Ukitaka upigwe mawe itaje ccm.
   
 19. D

  Do santos JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo maeneo ambayo chadema inaungwa mkono ni maeneo yenye wakristo wengi? Hiki chama ni ngumu sana kukitenganisha na ukristo,kwani hata mashabiki wake wanaonesha hivyo.Bila shaka waislamu hawakiungi mkono kwa sababu kama hizo,Acheni siasa za udini

  Tatizo lililopo mpaka sasa hivi ni huu ukanda wa umakondeni na uzaramoni, huku ndiko kunapaswa kuwaweka sawa wazawa wa maeneo hayo hili waunge mkono na mbaya zaidi CUF hizi ndio ngome zake, maana hakuna siri kwamba sehemu hizo wanaamini kabisa kwamba CUF ni chama cha waislamu na jamii kubwa ni waislamu katika hayo maeneo.[/QUOTE]
   
 20. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Pasco nimekusoma; embu chukuliwa kwa takwimu zako hizo kanda mbili zinatosheleza kumpitisha Raisi toka chama "A"; Kanda hizo mbili labda idada ya Wabunge wake hawazidi 50 kati ya 350 bado huyo Raisi ataweza kuongoza nchi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...