Simulizi nzuri mkuu, congratulations
Ninayo kadhaa ya kuongezea. Unaweza kumtazama Gadaffi katika pande zoye i.e kiongozi mzuri na pia kiongozi mbaya, kama ilivyo kwa binadam wengine
Binafsi nayakumbuka haya
1. Alikua kiongoz mzuri kwa wana Libya, kuinua uchumi na pato ta taifa. Lakini analaumiwa kwa kuendekeza "ukabila" huku akiwatesa sana makabila hasimu kwake kiasi ambacho hawakufurahia utawala wake. Huku ndiko uasi ulupoanzia dhidi yake
2. Kimataifa, wakati akijipambanua kama mtetezi wa nchi zilizoonewa, ufadhili wake kwa vikundi kadhaa ulileta maafa makubwa kwa watu wasio na hatia. Mf. Munich massacre amabapo kikundi cha Black September kiliwateka na kuwaua wanamichezo toka Israel bila huruma. Hawa walidhaminiwa na Gadaffi. Pia kutekwa kwa ndege iliyokua na abiria wa mataifa mchanganyiko kutika ulaya na israel, kisha kurushwa had Libya, Algeria na Misri hatimaue Uganda ambapo watu wengi wasio na hatia waliuawa. Pia tukio la kulipuliwa kwa ndege ya Ufaransa na magaidi kwa ufadhili wa Gadafi
3. Kwetu sisi TAnzania hatutamsahau kwa kumgadhili Idd Amini katika ile vita maarufu ya Uganda, vita ambayo hatutakaa tuisahau kwa kuharibu uchumi na ndoto za taifa letu, vota iliyoturudisha nyuma kiasi hatujaweza 'recover" hadi leo. Kw la ufadhili wa Gadafi, Idd Amini alidhamiria kutimiza "ndoto ya mchana" kujimilikisha bandari ya Tanga. Ni miujiza ya Mungu tu ndio ilituokoa