Kanali Muammar Gaddafi (1942 - 2011)

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,716
Sasa, unaweza kupata nakala za Kitabu changu cha "NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI".
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-

Pia waweza kupata kitabu changu cha "OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI"
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-

Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457

Au bofya link hapa chini kunitumia ujumbe moja kwa moja whatsApp


Neno la Utangulizi


Japokuwa wengi wameandika, lakini baada ya kutafiti kwa kina na kukusanya taarifa za kutosha na kujiridhisha juu ya uhalisia wa masuala kadhaa muhimu, imenipendeza nami niandike japo kwa uchache yale niliyoyasikia, kuyaona na kujifunza kuhusu moja ya binadamu muhimu kupata kuishi katika zama hizi za kizazi chetu, Kanali Muammar Gaddafi.
Moja ya watu mashuhuri zaidi aliyebadili historia ya dunia kwa namna mbali mbali.



Tafadhali fuatana nami katika mfululizo wa makala hii mpya.



909afebafe3fb58db1900246cd4b87e5.jpg





Genesis


Jina lake kamili anaitwa Muammar Mohammed Abu Minyar Gadaffi.


Alizaliwa hemani katika eneo la jangwa la Tripolitania eneo linaloitwa Qasr Abu Hadi nje kidogo ya mji wa Sirte.
Muammar anatokea kwenye kikabila kidogo kisicho na ushawishi ndani ya Libya, kinachoitwa Qadhadhfa, ambao asili ya kabila hili ni aina ya watu wajulikanao kama Bedouins.

Siko vizuri sana kwenye kiarabu lakini nijaribu tu kueleza kwa kadiri ninavyodhani, kwamba Jina hili la Bedouins linatokana na maneno ya kiarabu na kingereza.. "Badyah dwellers" ambapo neno 'Badyah' ni kiarabu yenye maana ya ardhi iliyotupu (jangwa).
Ndio kusema kwamba Bedouins ni kinyume cha neno la kiarabu "hathar" ambalo lina maana ya jamii ya watu waishio mijini.


Kwahiyo, Muammar na familia yao walikuwa wanaishi jangwani kabisa ambapo mama yake aliyeitwa Aisha alikuwa ni mama wa nyumbani na baba yake aliyeitwa Mohammed Abdul Salam bin Hamed bin Mohammad alikuwa ni mchunga mbuzi na ngamia jangwani.



Watu wenye asili ya Bedouins wanafahamika kwa sifa moja kubwa ya kutokujua kusoma wala kuandika. Hii ndio sababu kubwa kwanini mpaka leo tarehe au mwaka halisi aliozaliwa Gaddafi bado haijulikani kwa usahihi. Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe pamoja na ndugu zake, inaonyesha kwamba yawezekana Gaddafi alizaliwa mwaka 1942 au 1943. Laikini papo hapo ziko tafiti zinazopendekeza kwamba yawezekana Muammar alizaliwa mwaka 1940.


Muammar ndio mtoto pekee wa kiume kwa wazazi wake ambaye alikuwa hai lakini ana dada zake wengine watatu.



Akiwa bado Mdogo, elimu yake ya mwanzo kabisa kuipata ilikuwa ni elimu ya dini, ambayo alifundishwa na mwalimu wa madras hapo kijijini kwao.
Baadae akiwa bado na umri mdogo vivyo hivyo ikambidi ahamie mjini Sirte ili aweze kuhudhuria shule ya elimu ya kawaida kama watoto wengine.
Akiwa Sirte kutokana na kutokuwa na familia hapo, siku za katikati ya wiki alikuwa analala msikitini na ikifika weekend anatembea takribani kilometa 20 kurudi jangwani kuungana na familia yake.


Akiwa shuleni, alikuwa akichekwa sana na kuzomewa kutokana na asili yake ya Bedouins.
Watu waliosoma nae, wanaeleza kuwa badala ya Muammar kujiona mnyonge kutokana na kuchekwa na wanafunzi wenzake yeye alikuwa imara zaidi na alitumia muda mwingi kuwatia moyo vijana wenzake wenye asili ya Bedouins hapo shuleni wajivunie asili yao badala ya kujisikia aibu.


Muammar alifanikiwa kumaliza madarasa sita ya elimu ya msingi kwa miaka minne pekee.


Baadae familia yake ikahamia eneo la kibiashara la Sabha ambayo iko kwenye mji wa Fezzan kusini kati mwa Libya.

Wakiwa hapa, Muammar akaanza masomo ya sekondari na ndipo nyota yake ikaanza kung'ara mapema.





KUINGIA KATIKA HARAKATI



Katika kipindi cha makuzi ya utoto na ujana wake yalitokea matukio mengi ya kihistoria katika 'ulimwengu' wa Kiarabu ambayo yalichangia kwa kiwango kikubwa kutengeneza haiba na mitazamo ya Muammar.

Mfano mwaka 1948 kulitokea vita ya kihistoria ya Israel na Nchi za Kiarabu.
Mwaka 1952 yalitokea mapinduzi nchini Misri yakiongozwa na Gamal Abdel Nasser (alikuja kuwa 'role model' wa Muammar maisha yake yote) mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Mfalme Farouk na baadae kubadilisha katiba ya nchi na kuondoa mfumo wa kifalme kwenye katiba na baadae kuipatia Uhuru Misri na Sudan kutoka kwa Waingereza (kipindi hicho Sudan ikitawaliwa kama sehemu ya Misri)


Pia ujanani mwake Muammar mwaka 1956 alishuhudia mzozo mkubwa wa Mfereji wa Suez, na pia alishuhudia uundwaji na kuvunjika kwa muda mfupi kwa shirikisho la nchi za Kiarabu (United Arab Republic) mwaka 1958 mpaka 1961.



Hivyo basi akiwa hapo mji wa Sabha walipokuwa wakiishi sasa yeye na familia yake huku akipata masomo yake ya upili, kutokana na walimu wengi katika shule yake kuwa Wamisri, hii ilimsaidia Muammar kwa mara ya kwanza alipata fursa ya kupata na kusoma magazeti ya Kiarabu na kusikiliza vipindi vya redio vya Kiarabu.


Kipindi cha redio kilichomvutia zaidi Muammar kiliitwa Voices Of Arabs ambacho kilirushwa na redio kutoka jijini Cairo, Misri.


Muammar alikuwa akivutiwa mno na mawaidha ya mwanamapinduzi wa Misri niliyemueleza hapo awali (Gamal Abdel Nasser) ambaye alikuwa akipinga kwa nguvu zote sera za kimagharibi zinazokumbatia Ukoloni, Ukoloni mamboleo, Uzayuni na pia alikuwa anachochea nchi za Kiarabu zikatae mfumo wa kiuchumi wa Kibepari na waanzishe mifumo ya Kijamaa.


Ni katika kipindi hiki ambapo Gadaffi alitumia muda mwingi kusoma tena na tena kitabu kilichoandikwa na Gamal Abdel Nasser kuhusu falsafa ya mapinduzi (Philosophy of Revolution) ambacho kiliainisha namna ya kupanga na kutekeleza mapinduzi.


Baada ya muda kidogo akiwa bado ni mwanafunzi wa shule ya upili, mbegu ya kimapinduzi ikaanza kuchipuka ndani ya moyo wa Gadaffi.

Akaanza harakati za kuandaa maandamano na kusambaza vipeperushi kupinga utawala wa Kifalme nchini Libya.
Mwezi octoba, 1961 Gadaffi aliandaa maandamano makali kupinga kujiondoa kwa Syria katika Shirikisho la United Republic of Arabs. Maandamano haya yalikuwa makali sana na waandamanaji walivunja madirisha ya vioo vya Hoteli maarufu hapo mjini Sabha.


Serikali ya mji, ilikasirishwa sana na kitendo hiki na kama adhabu, wakamfukuza Muammar na familia yake kuhama mji wa Sabha.



Ndipo hapa ikawalazimu yeye na familia yake kuhamia mjini Misrata na kuendelea na masomo ya upili akiwa huko.


Akiwa Misrata licha ya kushawishiwa sana kujiunga na vyama vya kisiasa kama vile Arab Nationalist Movement, Arab Socialist Ba'ath Party na Muslim Brotherhood, Gadaffi alikataa katakata akishikilia msimamo kwamba vyama vya kisiasa vinaleta mtengano wa kijamii na tamanio la moyo wake ni kuona jamii nzima ya Kiarabu (nchi zote za Kiarabu) zinaungana.


Akiwa hapa Misrata Kiu yake ya uanaharakati ikaimarika zaidi na alitumia muda mwingi mno na kusoma kwa bidii sana kuhusu mwanamapinduzi Gamal Abdel Nasser.


Pia katika kipindi hiki alisoma sana na kwa bidii kubwa makala za mwanatheolojia za Siasa kutoka Syria Bw. Michael Aflaq.
Pia alisoma kazi nyingi sana za Sun Yat-sen na Mustafa Kemal Atatürk waandishi wa historia ya maisha Abraham Lincoln.



Baadae akachaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Libya (University of Libya) kilichopo mjini Benghazi akisomea masomo ya Historia.




4be22a9dada7321d083328c5e99b3ff3.jpg




Akiwa hapa chuoni alipata wazo mujarabu kabisa ambalo lilikuja kubadili kabisa maisha yake yajayo.
Gadaffi aling'amua kwamba kwa mtu ambaye anatoka kwenye familia masikini na daraja la chini kama yeye, ili aweze kuinuka na kuwa katika raia wa daraja la juu, njia nzuri na rahisi kufanikisha hilo ni kujiunga na Jeshi.



Hivyo basi, yeye na marafiki zake kadhaa waliosoma wote shule ya upili Misrata, wakaacha chuo na kujiunga na Jeshi, katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Royal Military Academy kilichopo hapo hapo Benghazi.


Katika kipindi hiki Libya ilikuwa chini ya utawala wa Mfalme Idris, na hivyo katika vyuo vya kijeshi, mafunzo yalikuwa yanatolewa na Jeshi la Uingereza.


Kitendo hiki kilimuudhi sana Gadaffi kwakuwa aliwaona Waingereza kama mabepari na wanyonyaji.

Hii ilimfanya kuwa na misimamo ya kushangaza sana.


Kwa mfano akakataa kujifunza lugha ya kingereza, lugha ambayo ilikuwa inatumika kufundishia chuoni hapo. Hii ilimsababishia kufeli mara nyingi sana kwenye mitihani yake jeshini.

Pia mara kadhaa aligoma kutii amri za maafisa na wakufunzi wa kijeshi wa Uingereza.


Mara kadhaa maafisa hawa wa Uingereza walimripoti Gaddafi kwenye Jeshi la Libya kwamba ni "mtovu" wa nidhamu lakini ripoti hizi zilipuuzwa.
Hivyo basi kwa "kuungaunga" hivyo hivyo, Gadaffi akamaliza kozi ya mafunzo ya Jeshi. Na baada ya kumaliza akapangiwa kuwa Afisa mwenye jukumu la mawasilino katika kitengo cha kijeshi cha 'Signal Corps'.


Baadae akapangiwa kwenda kwenye mafunzo zaidi ya kijeshi nchini Uingereza.
Hii ikamlazimu alipofika Uingereza kutumia miezi tisa ya kwanza katika kambi ya Beaconsfield, Buckinghamshire kujifunza Kingereza.
Baadae akaelekea Bavington Camp, Dorset kwa ajili ya kozi ya 'Signal Instructor'.
Kisha akapelekwa Hythe, Kent. kwa ajili ya kozi ya 'Infantry Signal Instructor'.


Akiwa Uingereza mara kadhaa Gadaffi aliripoti nyumbani Libya Jeshini kwamba anafanyiwa vitendo vya kibaguzi nchini humo.
Lakini maafisa wa Jeshi la Uingereza walijitetea kwamba Gaddafi anashindwa kuendana/kubadilika kuendana na tamaduni za kimagharibi.

Mfano walisema kwamba Gadaffi alikuwa anavaa kwa kujifunga mashuka kwa staili watu wavaavyo nchini Libya kisha anatembea kwa kujidai kabisa akikatiza mitaa ya London, na hiyo ilifanya watu wamshangae mno na Gadaffi alitafsiri kama ubaguzi.




Pia, Kumekuwa na uvumi mwingi ulioenea mno kwamba Gadaffi akiwa Uingereza aliwahi kuhudhuria chuo cha Royal Military Academy Sandhurst (karibu maafisa wote wa Jeshi la Uingereza hupitia chuo hiki), lakini binafsi kwa kadiri nilivyotafiti sijafanikiwa kuona nakala ya nyaraka yoyote kuthibitisha hilo, kwahiyo binafsi nashikilia msimamo wa uvumi huo kama "rumors" tu.



Marafiki wa Gadaffi wanaeleza kuwa aliporejea Libya kutoka Uingereza, alikuwa ni mtu mwenye kujiamini sana na mwenye haiba imara zaidi.


Ndipo hapa kwa kushirikia na marafiki na makada wengine waliopo jeshini wakaunda Kamati Kuu ya vuguvugu la siri waliloliita 'Free Officers Movement' (jina hili alilitoa kwa shujaa wake Gamal Abdel Nasser).

Wanachama wa vuguvugu hili walikuwa wanakutana kwa siri kubwa, na pia wakatengeneza mfumo wa siri wa wanachama wao kukutana kwenye 'vijiwe' (clandestine cell systems).


Makada na wanachama wa vuguvugu hili katika 'vijiwe' vyote walikuwa wanachangia mishahara yao kwenye mfuko/akaunti moja ili kusaidia kuendesha shughuli na harakati za vuguvugu.


Gaddafi mwenyewe alikuwa anasafiri maeneo mbali mbali ya nchi ili kukusanya Intelijensia kuhusu mwenendo wa nchi na kutengeneza "connections" na watu wanao waunga mkono.



Vyombo vya Intelijensia ya nchi vilipata taarifa kuhusu mwenendo wa Gaddafi lakini wakaampuuza wakimuona kama kijana mwenye "mihemko" ya kisiasa na hana madhara yoyote kwa nchi.!!



Walifanya kosa kubwa sana…



MAPINDUZI: LIBYA MPYA




Hadi kufikia miaka ya 1960s serikali ya Mfalme Idris ilikuwa inapingwa vikali na wananchi wa Libya.
Staili yake ya uongozi ambao alijilimbikizia madaraka makubwa mno na familia yake ili aweze kufaidi utajiri wa mafuta wa nchi iliwachukiza sana watu wa Libya.


Ilifika kipindi suala la maandamano nchini Libya likawa la kawaida. Kila kukicha kulikuwa na mahali watu wanaandamana kupinga ufalme wa Idris. Watu waliandamana na kuvamia visima vya mafuta na kufunga shughuli zilizokuwa zinaendelea.


Kosa moja kubwa ambalo Idris alilifanya ilikuwa ni kufungamana na nchi za magharibi.
Hii ilipelekea mwaka 1967 baada ya Misri kushindwa vibaya na Israel katika vita maarufu ya 'The Six Day War' wananchi wa Libya wakaelekeza hasira zao kwa utawala wa Idris wakimtuhumu kuwa ni mshirika wa Israel.


Hii ikapelekea kikundi cha vuguvugu kilichoongozwa na Gadaffi, Free Officers Movement kuzidi kuungwa mkono japokuwa ilikuwa ni kwa siri mno.
Japokuwa CIA wamekanusha sana, lakini upo ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba walikuwa wanajua nyendo za Gadaffi na vuguvugu lake la Free Officers Movement.

Wenyewe CIA wanakanusha na kusema kwamba waliyekuwa wanamfuatilia nyendo zake ni, Abdul Aziz Shelhi kiongozi wa kikundi kingine cha vuguvugu kilichoitwa Black Boots.



1384ed644f31aebb52b754f0bdaec7b6.jpg




Katikati ya mwaka 1969 nchi ikiwa bado haiko kwenye utulivu kutokana na maandamani ya kila kona, Mfalme Idris akasafiri kuelekea nchini Uturuki na Ugiriki kwa ajili ya mapumziko ya msimu wa joto.


Gadaffi na washirika wake wa Free Officers Movement ambayo sasa ilikuwa na wafuasi wengi jeshini na hata uraiani waliona hii ni fursa adhimu kutimiza matarajio yao na ya wananchi wa Libya.


Ndipo hapa Gaddafi akaongoza wafuasi wake kutekeleza oparesheni ya kijeshi ambayo aliita "Operation Jerusalem ".

Siku ya Tarehe 1, September 1969 Gadaffi alitawanya wafuasi wake kuteka sehemu zote za kimkakati kwenye miji ya Tripoli na Benghazi.
Washirika wake waliteka viwanja vya ndege, vituo vya polisi, vituo vya redio na majengo ya ofisi za serikali kwenye miji hiyo.


Yeye mwenyewe aliongoza kikosi ambacho kilienda kuteka kituo cha kijeshi cha Berka mjini Benghazi.
Rafiki yake Omar Meheisha aliongoza kikosi ambacho kilienda kuteka kituo cha kijeshi cha Tripoli. Na swahiba wake mkubwa wa tangu utotoni walipokuwa shule ya sekondari, Abdul Salam Jalloud aliongoza kikosi kilichpenda kuteka mitambo ya kijeshi ya kudungua ndege (antiaircraft battery) iliyopo Tripoli.


Pia Gadaffi alituma kikosi kilichoongozwa na rafiki yake aliyeitwa Khweldi Hameidi kilichoenda kumkamata Mwana Mfalme (crown Prince) Sayyid Hasan ar-Rida al-Mahdi as-Sanusai.
Huyu ndiye alikuwa anatarajiwa kumrithi baba yake Mfalme Idris. Baada ya kukamatwa akalazimishwa kuikana hadharanj haki yake hiyo ya kurithi ufalme kutoka kwa baba yake.


Mpaka kufikia hatua hii ya zoezi hili la mapinduzi, hakukuwa na damu yoyote iliyomwagika (hakukuwa na vifo vya watu).
Hii ndio sababu iliyopelekea mapinduzi hayo huko mbeleni kujulikana kama "White Revolution " kabla ya hapo baadae kubadilishwa jina na kuitwa " One September Revolution" ili kuakisi siku hii muhimu ambayo Mfalme Idris na utawala wake waliondolewa kutoka madarakani.


Baada ya sehemu zote hizi za kimkakati kutekwa na kuwa chini ya washirika wa Free Officers Movement, huu ukawa ni muda muafaka kabisa kufanya hatua inayoguata.


Gadaffi akaelekea moja kwa moja mpaka kwenye kituo kimoja wapo cha Radio kuwajulisha ni nini kimetokea kwenye nchi yao. Ni siku hii ya tarehe moja September 1969, kwenye Redio hii… Muammar Gadaffi akautangazia umma wa Libya kuhusu mapinduzi ya kumng'oa madarakani Mfalme Idris na kuunda 'Libya mpya' ambayo mwenyewe aliita Libyan Arab Republic.


Ifuatayo ni hotuba yake kamili kwa wananchi kupitia radio, siku ya mapinduzi, September 1, 1969.




"Watu wa Libya! Katika kuitikia matakwa yenu, matarajio ya ndani ya sakafu za mioyo yenu, kujibu mnachohitaji juu ya mabadiliko na kufanya upya kwa kizazi chetu, na kujibu kilio chenu cha siku nyingi ili kukomeshwa kwa udhalimu… hatimaye leo hii majeshi yenu ya ulinzi, yameondoa madarakani utawala wa kifedhuli uliotukandamiza sote kwa kipindi kirefu sana.! Kwa pigo moja tu na mkupuo mkoja tu majeshi yenu tumeondoa miungu watu na kuharibu sanamu zao. Kwa ligo moja tu tumeweza kuleta nuru kwenye giza nene la muda mrefu ambalo kwanza ilianza kutamalaki kwa uturuki, kisha ikaja kutawala kwa Italia, na kisha utawala huu dhalimu ambao si chochote zaidi ya wanyonyaji, watesaji, wadhalimu na wahaini.! Wananchi wa Libya leo hii Libya mpya inazaliwa.!"

- Muammar Gaddafi





Mapinduzi yalikamilika rasmi, kilichokuwa mbele yake ilikuwa ni kuijenga upya Libya kwa misingi ya tamaduni na imani yake, kuindoa kuwa kibaraka wa magharibi, na pia muhimu zaidi kuhakikisha kwamba wananchi wote wanafaidi matunda ya utajiri wa mafuta ambao nchi yao imejaaliwa.


Safari ya matumanini ya kuijenga upya Libya ikaanzia hapa.




********


UJENZI WA LIBYA MPYA



Baada ya Muammar Gaddafi kuingia madarakani mwaka 1969 alifanya mabadililo makubwa sana ya kimfumo na utawala wa Libya.


Kwanza kabisa alibadili kikundi chake cha vuguvugu cha Free Officers Movement na kuwa Revolutionary Command Council (RCC) ambayo ndiyo ikafanyika kuwa serikali mpya ya Libya.
Muammar mwenyewe ndio akawa Mqenyekoti wa RCC.
Katika kipindi hiki Muammar alikuwa na cheo cha kijeshi cha Luteni, na akajipandisha cheo kutoka Luteni mpaka Kanali.

Pia yeye ndiye akawa Mkuu wa nchi na Mkuu wa majeshi.
Pia akamchagua rafiki yake wa miaka mingi tangu utotoni Jalloud kuwa Wazoliri Mkuu.


Baraza lake la kwanza la mawaziri kama nilivyoeleza kuwa likitokana na RCC. Kwahiyo kwa kiasi fulani lilikuwa ni "la ajabu".
Katika kipindi hiki cha mapinduzi, Muammar alikuwa na miaka 28 pekee. Vivyo hivyo na marafiki zake wa RCC (ambayo ilikuwa Free Officers Movement) nao walikiwa ni vijana wadogo waliotokea familia za hali ya chini na wachache wa kipato cha kati.

Kwahiyo baraza lake la kwanza la mawaziri, liliundwa na vijana wadogo, ambao karibu wote hakuna ambaye alikuwa amemaliza chuo kikuu.


Hivyo basi mwezi May 1970, serikali ya Gaddafi ikaitisha kongamano maalumu la wasomi ili kuwashawishi kuhusika katika serikali yao mpya.


Baada ya hapo akaanza kufanya mabadiliko ya kimfumo.

Akabadili mji mkuu wa nchi kitoka al-Beida na kuuufanya mji wa Tripoli kuwa mji mkuu mpya wa Taifa la Libya.

Kwanza akabadili katiba na kufanya "Sharia" ya kiislamu kuwa ndio sheria ya nchi.
Pia akavunja vyama vyote vya wafanyabishara na wafanyakazi. Pia akapiga marufuku migomo ya aina yoyote ya wafanyakazi.
Pia magazeti mengi yakafungiwa kuchapishwa.


Mwezi September 1971 Gaddafi aliwahi kujiuzuru kwa kutokufurahishwa na kasi ya mabadiliko lakini alirejea tena madarakani mwezi mmoja baadae.
Pia mwezi February mwaka 1973 Gadaffi alijiuzuru tena na alarejea tena ndani ya mwezi mmoja.



Baadae Gaddafi akaanzisha Sera ya "Mapinduzi ya Kijani" (Green Revolution) ili kuleta mabadiliko makubwa katika sera ya kilimo na kupunguza utegemezi wa Libya katika kutegemea kuagiza chakula nje ya nchi.


Kwahiyo ikatengenezwa mifumo na miundombinu thabiti ya umwagiliaji na kuongeza ardhi kubwa ya kilimo nchini Libya.

Pia serikali ya Gaddafi ikawanyang'anya ardhi walowezi wa Kiitaliano na kuigawa kwa wananchi wa Libya huku pia serikali ikitoa ruzuku lukuki kwa wananchi.



Lakini, kwa kuwa pia nchi ya Libya inategemea mafuta kama bidhaa kuu wanayouza nchi za nje, mwaka 1970 Gaddafi akavunja mikataba hiyo yote ya mafuta na makampuni ya kigeni akieleza wazi kuwa mikataba hiyo haikuwa inainufaisha Libya.


Mwishoni mwa mwaka huo 1970 karibia nchi zote wanachama wa OPEC wakaunga mkono juhudi hizi za Muammar Gaddafi na kupelekea kupanda kwa kiwango kikubwa cha bei ya mafuta duniani.
Hii ikapekekea Libya kusaini mkataba mashuhuri uliojulikana kama "The Tripoli Agreement", ambao ulisaidia Libya kupata gawio kubwa zaidi kwenye uchimbaji wa mafuta.


Hii ikasaidia serikali ya Muammar kupata zaidi ya dola Bilioni moja kutoka kwenye biashara ya mafuta katika mwaka wake wa kwanza madarakani.


Baada ya Muammar kushuhudia makusanyo makubwa hivi ya Kodi katika mafuta, mwaka uliofuata akaanzisha mpango wa kutaifisha makampuni yote ya mafuta yaliyokuwa yanafanya kazi nchini humo. Kampuni ya kwanza shughuli zake kutaifishwa ilikuwa ni British Petroleum.
Makampuni mengine yaliyosalia na yale ambayo yalikuwa yabakusudia kwenda kufanya shughuli za uchimbaji mafuta nchini Libya, zilipewq sharti la 51% ya hisa zake kuwekwa chini serikali ya Libya.


Hii ikapelekea kukua kwa pato la mwaka kutoka dola bilioni 3.8 waliyoikuta mwaka 1969 mpaka kufikia dola bilioni 13.7 mwaka 1974 na kupaa hadi dola bilioni 24.5 mwaka 1979.


Kukua huku kwa Pato la Taifa, kuliboresha haswa kuongezeka kwa hali za maisha nchini Libya.
Mfano katika muongo wa kwanza wa utawala wa Muammar (mwaka 1979) wastani wa pato la wananchi kwa mwaka lilikuwa mpaka kufikia dola 8,170 kutoka dola 40 kwa mwaka 1951.
Kiwango hiki kilikuwa juu ya viawango vya wastani wa vipato vya wananchi katika nchi nyingi zilizoendelea mfano, UK na Italia kwa kipindi hicho.


Kadiri ambavyo Muammar aliimarisha uchumi wa Libya ndivyo ambavyo pia alijitahidi kuimarisha hali za kimaisha za wananchi wake.
Mfano akaanzisha ujunzi wa makazi ya kuishi wananchi wake na kupandisha mishahara kwa 100% (mara mbili) ambapo serikali ilikuwa inakata 40% au 30% kama kodi ya makazi.


Pia akachochea na kuenzi desturi za Libya, kwa kufanya kiarabu kuwa lugha pekee rasmi ya kiofisi nchini humo, kiasi kwamba mpaka alama za barabarani alizibadili na zikaandikwa kwa kiarabu.
Lakini pia akahamasisha uvaaji wa mavazi asili ya Kilibya.
Pia klabu zote na makanisa yakafungwa nchi nzima.


Lakini pia Gaddafi alifanya jambo ambalo wengi hawakulitegemea.
Aliweka nia ya kukomesha kabisa utamaduni uliozoeleka nchini humo wa kuwakandamiza wanawake.

Kwanza akapitisha sheria ya kuamuru usawa maeneo ya kazi kati ya wanawake na wanaume na usawa katika ujira. Lakini pia sheria hii ikapiga marufuku wanawake kuolewa chini ya miaka kumi na sita. Pia sheria hii ilipiga marufuku utamaduni wa waarabu kuwaoza watoto wao wa kike bila matakwa yao. Chini ya sheria hii binti mwenyewe alitakiwa kukubali ndoa ndipo aozwe.


Pia Gaddafi alifadhili kuanzishwa kwa Libyan General Women Federation.

Mabadiliko haya yalienda sambamba na mabadiliko katika sekta ya afya.
Mpaka kufikia mwaka 1978 idadi ya hospitali nchini Libya zilikuwa zimeongezeka kwa 50% kulinganisha na mwaka 1968. Lakini pia idadi ya madaktari ilikuwa imeongezeka kutoka madaktari mia saba mwaka 1968 mpaka kufikia madaktari zaidi ya elfu tatu mwaka 1978.


Libya pia ikafanikiwa kutokomeza magonjwa ya Malaria, trakoma na kifua kikuu ambayo yalikuwa tishio kwa kipindi hicho.


Elimu ya msingi ikaongezwa kutoka miaka sita mpaka miaka tisa.
Akajenga chuo kikuu cha Beida, na chuo kikuu cha Tripoli na Benghazi vikapanuliwa.

Lakini pia kwa miaka mingi Libya ilikuwa ikisumbuliwa na watu kubaguana kutokana na makabila na ukanda.
Hivyo basi kwanza kabisa Gadaffi akapiga marufuku viongozi wote wa kikabila nchini Libya na pia mipaka ya mikoa ikachorwa tena upya.




Ndani ya miaka kumi tangu Gaddafi kuingia madarakani aligeuka kuwa shujaa wa taifa kutokana na "miujiza" aliyoifanya kubadili mwelekea na hali ya taifa na wananchi wake.
Wananchi wakaanza kumfananisha na Omar al-Mukhtar shujaa wa taifa la Libya wa miaka ya mwanzoni mwa 1900s ambaye kwa miaka ishirini aliongoza wananchi wenzake mashariki mwa Libya kupambana na ukoloni wa Waitaliano.


2d76f2486f2b86a8a7bd908e700bcd4a.jpg

Sanamu ya Omar al-Mukhtar, shujaa ambaye wananchi walikuwa wanamfananisha na Muammar Gaddafi



Wakati ambao wananchi wa Libya walikuwa wakimuona Muammar kama shujaa na mtu pekee mwenye uwezo wa kuijenga upya Libya na kuboresha uchumi wa nchi na raia wake, watu wa magharibi wao walioba tishio na kuhatarishwa kwa maslahi yao, na hii iliwafanya waone kwamba kuna ulazima wa kitu kufanywa ili "kumdhibiti".

BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA PILI

BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TATU




The Bold - 0718 096 811
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden

bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb
 
Asante mkuu Kwa maelezo mazuri na ya kina kuhusu huyu Dikteta Gaddafi.

Uhuru wa mwanadamu yeyote ndilo jambo la msingi. Mwanadamu mfanyie hata mbingu hapa duniani bila jumps uhuru wake yote umfanyiayo ni bure na kujilisha upepo.
Maendeleo yeyote yatakayo kuja katika jina la kutunyima Uhuru wetu Kama wanadamu hatuyataki, hayatakiwi.
 
Asante mkuu Kwa maelezo mazuri na ya kina kuhusu huyu Dikteta Gaddafi.

Uhuru wa mwanadamu yeyote ndilo jambo la msingi. Mwanadamu mfanyie hata mbingu hapa duniani bila jumps uhuru wake yote umfanyiayo ni bure na kujilisha upepo.
Maendeleo yeyote yatakayo kuja katika jina la kutunyima Uhuru wetu Kama wanadamu hatuyataki, hayatakiwi.
Kabisa mkuu.. Well said
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden

bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje



MGOLOLIFINYONGE SAMBIYAGAVYWA MATINYA NDISAKWISAKWISA NKYANDWALE MWAISUPULE BABA KING'EA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom