Qixima mQiqa
Senior Member
- May 18, 2012
- 178
- 20
Kila la kheri Bashaija
cv yako haitufai chochote hamna jipya kiutendaji, tunahitaji safaricom/safaritel yetu
Kamugisha kazaura...aka MUGI...hongera kaka, wewe pamoja na Peter Ulanga(CEO-Mfuko wa Mawasiliano) mnawakilisha "timu ile" ya KIBAHA SECONDARY SCHOOL
Mwl. Kazibure(RIP) na Mkuu wa Shule Mwampaja hakika walifanya sehemu yao...
na SISI TUNAKUJA MUGI...hakuna wa kutuzuia......go Kibaha...go...
Daaaaaah nshomileee !
...Wote tunaoitakia Mema TTCL tumuombee Hivyo lakini ni Ngumu Sana.
Anaweza Kuishia kwenye Vicious Circle ya 'Busines as Usual' tu.
Amefungwa Mikono.
Hawezi kuvunja Mkataba wa Ovyo wa TTCL na Celtel/Zain/Airtel Unaoivunja mbavu TTCL wa kutumia Minara na Mitambo ya TTCL bila Kuilipia.
Hawezi kuisambaza itakiwavyo Huduma rahisi ya Simu za Mkononi ya TTCL 073 ambayo ingeweza kuwapiga bao hawa Wahuni wote lakini kwa Vile Wazito wetu wengi wana Hisa kwenye Makampuni haya basi TTCL inabanwa Mbavu ili isisambaze sawa sawa tekinolojia yake ya simu ya Huaiwei kwa visingizio hivi na Vile.
Kuna Mdai amechangia vyema hapo juu. Aitishe ajira mpya na kuzipa kampuni za akina Deloitte kupata wafanyakazi wa aina yake wanaoweza kuipeleka Kampuni yetu ya Taifa.
Kuna Vijeba ndani ya TTCL ambavyo havikubali mabadiliko.
Ninawafahamu watu wawili watatu ambao wameishia Darasa la Saba na Form 4 (potelea mbali kwamba ni ya zamani!) lakini Meza wanazokalia, utazimia mwenyewe.
Ni hawa hawa ambao mteja Mzungu akiingia hawajua waongee nini naye na wanawasukumizia wenzao kwa sababu Lugha haipandi!
Kuna Mengi yanayoweza kumkwamisha Msomi huyu lakini kwa leo niishie hapa na kuwapa nafasi wengine Kuchangia...
kielimu,kiupeo na kiutendaji anastahili kuwa full CEO na sio kukaimu