Kampuni za Wachina hebu kuweni serious

Kwema job seekers wenzangu?

Kuna mchina kani-check somewhere, kaniambia nimtumie CV yangu kuna kazi za sales zinahitaji watu, nimemtumia cv yangu fresh,In return akanitumia job description ya kazi husika ndio nikaona huo mshahara anaotaka kunilipa.

Ofcoz nina uhitaji wa kazi ila nimemjibu thank you endelea na zoezi la kutafuta mtu mwingine, me siko tayari kwa huo mshahara.
Kuna maswali nimejiuliza, haya makampuni ya wachina huwa hayana HR department wakawashauri vizuri namna ya kurecruit watu na issue nzima ya compensation mpaka General Manager mwenyewe anaingia front kuokoteza wafanyakazi, na hiyo mishahara yao wanayotoa kama sio kutafuta kuibiwa ni nini?

Eti mshahara laki 2, serious?

View attachment 2020723
Mkuu wewe unaona 200k ni ndogo unaweza kumzaliushia huyo mchina zaidi ya 200k ili akulipe unavotaka au unataka ulipwe kwa kazi hujafanya.Kama we ni mfanya kazi utaangalia hio 1% the utasema nikiuza milioni 100 comission yangu ni milioni 1 then utajua kwamba hujui.

Hio ndio fare wage.
 
Kuna siku mchina kanicheki kasema tunatafuta HR ila tutakulipa 23K per day
Nikamuuliza iyo ni meal au salary?
Akanijibu kuwa ni salary nikamuuliza ivi umeangalia wapi nafanya kazi na experience yangu
kalala mbele
hawa jamaa wajinga sana aiseee
Sio wajinga swali ni je unaweza kumpa value ya kuingiza TZS 100,000,000 kwa mwezi ili aweza kukulipa 1 M?Jibu ni hapana.So unataka yeye atoe wapi pesa ya kukulipa?THINK kama unafikiri unaweza kuwalipa watu ambao hawazalishi basi anzisha kampuni yako au baki huko uliko.
 
Hustler Mentality..

Mkuu hapo ungepambana hio % ya Sales iongezeke walau ifike 5%+++ then nenda kapige kazi..

Ajira zote za kampuni za biashara ni lazima ulipwe hela ambayo umeingiza mkuu,, siku ukiwa na kampuni yako utaelewa hili..

Halafu kama ni Jobless na umeacha hio kazi basi utakuwa unaishi kwa Wazazi... Kuna mengi ungepata huko kuliko kuendelea kukaa home.. hii sentensi ni valid Only if ni Jobless na upo kwa Shemeji
 
Mtoa mada Huna Akili,
afu nna wasiwasi na elimu yako.

Ulitakiwa ukae nae akufafanulie hizo allowance na sio kukurupuka kukataa kazi.

Bungeni mshahara Ni mil.3.7 na allowance Ni zaidi ya million 8
 
Yani mchina kolo kweli eti 1% ina maana ukiuza mzigo wa million 1 anakupa elfu 10?
Hakuna kampuni ya mambo ya ujenzi.

Eti Unaweza kuuza bidhaa za mil. 1 kwa mwezi mzima?

Kwenye makampuni Iyo Ni Oda ya catoni Moja TU ya bidhaa, Tena kwa mteja mdogo
 
Negotiations skills zako ziko Chini saana,
Anapokuambia willing salary ni 200,000 wewe ungepmba 300,000 na very possible angekupa
Then hapo kwenye 1% ungepmba 2% yeye angekupa 1.25% plus
Lastly ungeomba transport na meal allowance, si ajabu angekupa 2000-4000 per day.
Kwa kifupi hii kazi ulitakiwa uanze na salary ya laki 6, sema wewe umezembea kunegotiate.
Hapo umenena,
Uyu jamaa hajui kula na kipofu.

Vijana kibao wameajiliwa kwa wachina na wanamaisha mazuri.

Kazi sio mshahara.

Kazi za sales nazifananisha na kazi za police traffic.
Mara nyingi huwa Kuna Ela huwa hazitarajiwi zinazengea zengea TU.

Ukiwa mjanja unatoboa fasta.
 
Kwema job seekers wenzangu?

Kuna mchina kani-check somewhere, kaniambia nimtumie CV yangu kuna kazi za sales zinahitaji watu, nimemtumia cv yangu fresh,In return akanitumia job description ya kazi husika ndio nikaona huo mshahara anaotaka kunilipa.

Ofcoz nina uhitaji wa kazi ila nimemjibu thank you endelea na zoezi la kutafuta mtu mwingine, me siko tayari kwa huo mshahara.
Kuna maswali nimejiuliza, haya makampuni ya wachina huwa hayana HR department wakawashauri vizuri namna ya kurecruit watu na issue nzima ya compensation mpaka General Manager mwenyewe anaingia front kuokoteza wafanyakazi, na hiyo mishahara yao wanayotoa kama sio kutafuta kuibiwa ni nini?

Eti mshahara laki 2, serious?

View attachment 2020723
Mkuu hizo kazi zinapatikana wapi?
 
Hustler Mentality..

Mkuu hapo ungepambana hio % ya Sales iongezeke walau ifike 5%+++ then nenda kapige kazi..

Ajira zote za kampuni za biashara ni lazima ulipwe hela ambayo umeingiza mkuu,, siku ukiwa na kampuni yako utaelewa hili..

Halafu kama ni Jobless na umeacha hio kazi basi utakuwa unaishi kwa Wazazi... Kuna mengi ungepata huko kuliko kuendelea kukaa home.. hii sentensi ni valid Only if ni Jobless na upo kwa Shemeji
Tuna vijana wa hovyo Sana,
Kijana hawazi ataizalishia kampuni kiasi gani, anawaza yeye atalipwa kiasi gani.

Anataka atajiwe kiasi ambacho at hakashiriki kukizalisha
 
Tuna vijana wa hovyo Sana,
Kijana hawazi ataizalishia kampuni kiasi gani, anawaza yeye atalipwa kiasi gani.

Anataka atajiwe kiasi ambacho at hakashiriki kukizalisha

Watanzania huwa nashindwana nao hapo tu.

Watu wako obsessed na Mishahara kuliko hata uwezo wao kiutendaji.... Kama huyo mleta uzi.. kazi ya sales anataka alipwe hela kubwa bila kujua kama hata hio kazi ataiweza au Laah...

Kijana unapopata kazi sehemu,, nenda kafanye kazi,, pambana at your potential...hakuna boss atakuona potential halafu akuache uende...Room ya negotiation huwa nzuri pale ambapo nawewe umeonyesha nini unacho...(na hata sio lazima ufanye mda mrefu saaaaana,, miez kadhaa tu utakuwa ushajulikana(Msosi wa kushiba huonekana hata ukiwa kwenye sahani

Madeni kuzidi malipo ni mwiko
- FidQ
 
Watanzania huwa nashindwana nao hapo tu.

Watu wako obsessed na Mishahara kuliko hata uwezo wao kiutendaji.... Kama huyo mleta uzi.. kazi ya sales anataka alipwe hela kubwa bila kujua kama hata hio kazi ataiweza au Laah...

Kijana unapopata kazi sehemu,, nenda kafanye kazi,, pambana at your potential...hakuna boss atakuona potential halafu akuache uende...Room ya negotiation huwa nzuri pale ambapo nawewe umeonyesha nini unacho...

Madeni kuzidi malipo ni mwiko - FidQ
Kweli kabisa,
Vijana wengi wanafeli hapo TU....
 
Kweli kabisa,
Vijana wengi wanafeli hapo TU....

Mkuu aache ufaLLa,, aende akapige kazi..

Hardware ni biashara ambayo ukiifanya kama sales lazima utoboe,, na pili ni Sales ni position ambayo hata kesho anaweza kuanzisha ofisi yake kwa kutumia mtaji wa Clients aliotoka nao hapo kwa mchina....kwasabu kibiashara sales ndio kama Jikoni,, kwingine kote mbwembwe
Badala ya kufikiria hayo yeye anakazana kuangalia Sinema kwenye TV ya shemeji.

Napata hasira sana ajira zilivo ngumu halafu mtu anapata shavu halafu anaanza kuleta mahaba na kazi....
 
Kwema job seekers wenzangu?

Kuna mchina kani-check somewhere, kaniambia nimtumie CV yangu kuna kazi za sales zinahitaji watu, nimemtumia cv yangu fresh,In return akanitumia job description ya kazi husika ndio nikaona huo mshahara anaotaka kunilipa.

Ofcoz nina uhitaji wa kazi ila nimemjibu thank you endelea na zoezi la kutafuta mtu mwingine, me siko tayari kwa huo mshahara.
Kuna maswali nimejiuliza, haya makampuni ya wachina huwa hayana HR department wakawashauri vizuri namna ya kurecruit watu na issue nzima ya compensation mpaka General Manager mwenyewe anaingia front kuokoteza wafanyakazi, na hiyo mishahara yao wanayotoa kama sio kutafuta kuibiwa ni nini?

Eti mshahara laki 2, serious?

View attachment 2020723
Acha tu mkuu umenikumbusha kitu hapa😂😂😂😂😂 wakati mkataba wangu unaelekea ukingoni katika kibarua fualani nilichokua nacho, niliona ni vema kusaka kazi nyingine mapema kabla ya siku kuisha hivyo niliwashirikisha jamaa zangu kadhaa in my network.
Kayi yao kuna mmoja akanijulisha kuwa kuna nafasi zipo wazi, nikamtumia CV yangu pamoja na copy ya certificates zangu zote, ni kwenye kiwanda fulani hapo Kisemvule.
Nikaitwa interview, tulikua watu saba na nafasi zilikua 2 kwanza nikashtuka maana experienced ni mimi peke yangu na hawa wengine sita ni graduates ambapo wawili walikua na mwaka mmoja tangu wahitimu na wanne wengine ni waliokua wametoka kuhitimu hata graduation bado.

Basi nikashuka hapo nikiamini kuwa hii kazi yangu na Mungu jaalia tukafika kipengele cha salary negotiations aisee kwanza nilivyotaja hadi jamaa wakashtuka lakini nilitaja range ya kawaida kwa serikalini kwa mwenye sifa kama zangu. Tukalimaliza. Hqpo ukumbuke working hours ni 12 na siku zote saba za wiki.
Baada ya wiki moja wananitumia emali ya offer eti mshahara 350k. Aisee nilibaki nimeduwaa nikawajibu tu asanteni na kumuuliza jamaa yangu akanambia kuwa ndio mishahara yao.

Aisee niliogopa sana na kuumia, yaani usafiri kwa siku moja ni 3k hapo sijala bado sasa si mshahara wote unakauka maana HAKUNA POSHO YA AINA YOYOTE.
Wacgina wanawakamua sana watu na kulipa kidogo sanaaa
 
Negotiations skills zako ziko Chini saana,
Anapokuambia willing salary ni 200,000 wewe ungepmba 300,000 na very possible angekupa
Then hapo kwenye 1% ungepmba 2% yeye angekupa 1.25% plus
Lastly ungeomba transport na meal allowance, si ajabu angekupa 2000-4000 per day.
Kwa kifupi hii kazi ulitakiwa uanze na salary ya laki 6, sema wewe umezembea kunegotiate.
Natumaini hujawahi kukaa mezani na wachina kubargain mshahara. Mimi nilivutana nao karibu wiki, wanataka huduma yangu lakini shida ni malipo. Nikatemana nao wakawachukua madogo
 
Wachina hawanaga diplomacy,ni wabaguzi mno.Sera yao ni take it or leave it,na ukitaka negotiation wanakufukuza hapo hapo at the middle of the interview.Ni aina ya waajiri wanaochapa staff wao viboko wakikosea mpaka leo
mimi kiboko hunichapi aisee ni bora unifukuze kazi, huo ni unyanyasaji ndani ya nchi yangu.

Kuna mchina alikatwa mapanga na mmasai kwa ajili ya huo ujinga..hakurudia tena kusumbua wafanyakazi
 
Natumaini hujawahi kukaa mezani na wachina kubargain mshahara. Mimi nilivutana nao karibu wiki, wanataka huduma yangu lakini shida ni malipo. Nikatemana nao wakawachukua madogo
Kwanza kiingereza hawajui.
 
Ebu naomba mi namba zao nijipeleke mwenyewe laki mbili inanitosha kabisa mwisho wa mwezi kuliko kutokupata kitu kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom