Kampuni inayohusika na 'wrong parking' iangaliwe vizuri

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,765
Ni hawa jamaa ambao yard yao ipo pale jirani na bohari ya msd. Utawakuta mjini wamevaa sare za suruali yeusi na shati jeupe. Wengine wana tshirt nyekundu. Na usafiri wao mkubwa ni bajaji. Kiukweli watu hawa ni janga la jiji. Kwanza wana hasira hao! Wengi ni kanda maalum.

Wakishashika gari yako yani uwe mpole tu. Hata kama wamekosea wao, kwa hasira zile na jazba zao na uelewa wao mdogo, pamoja na ubabe, huchomoki hivihivi.

Yani bora upambane tu mmalizane huko nje maana ukishaingia yard ni mengine tena . Kasoro yao kubwa ni gharama. Gari ya kazi gharama yake laki 3. Kama uloleta ubishi ikabidi ivutwe hadi yard, gharama ya kuvuta ni laki 4 na haijalishi umbali toka yard yao. Wakati mwingine bora ukutane na askari kuliko hawa manyigu. Naweza kuandika sana ila nina maoni machache;

1. Gharama zao zichunguzwe. Ni ghali mno. Kosa la juu angalau iwe ni elfu 50. Hii itassidia mno kupunguza chuki, milolongo, na kupoteza muda.

2. Wakikushika wakupe na sababu zilizo wazi badala ya kuanza kupaniki.

3. Waache kuvizia.

4. Jiji lijitathmini kwa kazi hizi wanazotoa kwa kampuni hizi. Jiji linahusika pia kuwapa kiburi

Wakuu mnaweza kuongeza yenu na kipi kifanyike
 
umenikumbusha kipindi cha makonda.. tulikamatwa kwa kutupa ticket kiholela nikafuatwa na jamaa akanambia kama una buku ten nipe yaishe kama hutak twende kituoni, nkasema sikupi hiyo hela twende tu kituoni.
Baada ya kufika huko nikakuta watu wengi sana waliokamatwa na ili ujinasue inabidi utoe elfu hamsini. Ila kila alie muita askari kwa ajili ya kutoa hela basi alisimamishwa na kwenda pembeni then ukitoa hela askari anatia mfukoni kisirisiri...
 
Serikali yetu si ya hovyo hii, wakikubamba wako tayari hata wakusababishie ajali ufe, Yani wanaweza shika usukani wa bajaji yako wakauyumbishayumbisha Kama upo unaendesha. Wanaurukia usafiri wako hata Kama uko on motion. Loh
 
Umeuma uma maneno na kuniacha kwenye mataa! ..."
Ni hawa jamaa ambao yard yao ipo pale jirani na bohari ya msd. Utawakuta mjini wamevaa sare za suruali yeusi na shati jeupe. Wengine wana tshirt nyekundu. Na usafiri wao mkubwa ni bajaji. Kiukweli watu hawa ni janga la jiji. Kwanza wana hasira hao! Wengi ni kanda maalum.

Wakishashika gari yako yani uwe mpole tu. Hata kama wamekosea wao, kwa hasira zile na jazba zao na uelewa wao mdogo, pamoja na ubabe, huchomoki hivihivi.

Yani bora upambane tu mmalizane huko nje maana ukishaingia yard ni mengine tena . Kasoro yao kubwa ni gharama. Gari ya kazi gharama yake laki 3. Kama uloleta ubishi ikabidi ivutwe hadi yard, gharama ya kuvuta ni laki 4 na haijalishi umbali toka yard yao. Wakati mwingine bora ukutane na askari kuliko hawa manyigu. Naweza kuandika sana ila nina maoni machache;

1. Gharama zao zichunguzwe. Ni ghali mno. Kosa la juu angalau iwe ni elfu 50. Hii itassidia mno kupunguza chuki, milolongo, na kupoteza muda.

2. Wakikushika wakupe na sababu zilizo wazi badala ya kuanza kupaniki.

3. Waache kuvizia.

4. Jiji lijitathmini kwa kazi hizi wanazotoa kwa kampuni hizi. Jiji linahusika pia kuwapa kiburi

Wakuu mnaweza kuongeza yenu na kipi kifanyike
Umeuma uma maneno na kuniacha kwenye mataa! ..."Wengi ni kanda maalum", kanda hiyo ndiyo wapi huko?
 
Nilisimama sehemu mtu alikuwa ananipa mzigo, sikumaliza hata sekunde 30 hao wamekuja na chain yao, sikuwa hata nimeshtuka wakafunga chain.
Hakuna hawakuwa na ubinadamu.
Mr aliwatafuta na pesa ikarudi same amount. Walitoa mifukoni mwao.
Hongera sana. Wanakera
 
Nilisimama sehemu mtu alikuwa ananipa mzigo, sikumaliza hata sekunde 30 hao wamekuja na chain yao, sikuwa hata nimeshtuka wakafunga chain.
hawakuwa na ubinadamu.
Mr aliwatafuta na pesa ikarudi same amount. Walitoa mifukoni mwao.
Atakuwa aliwapelekea moto hasa.
 
Majembe Auction walijikuta wanapigwa gharama hadi kuuzwa kwa Yard yao pale Mwenge sababu ya kuvuta gari la Mtu.

Hao unawaacha wachukue gari afu nenda mahakamani maana sehemu zote wanazokamata hakuna kibao cha No parking.
 
Serikali yetu si ya hovyo hii, wakikubamba wako tayari hata wakusababishie ajali ufe, Yani wanaweza shika usukani wa bajaji yako wakauyumbishayumbisha Kama upo unaendesha. Wanaurukia usafiri wako hata Kama uko on motion. Loh

dah
 
Back
Top Bottom