Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,920
- 2,798
Ni hawa jamaa ambao yard yao ipo pale jirani na bohari ya msd. Utawakuta mjini wamevaa sare za suruali yeusi na shati jeupe. Wengine wana tshirt nyekundu. Na usafiri wao mkubwa ni bajaji. Kiukweli watu hawa ni janga la jiji. Kwanza wana hasira hao! Wengi ni kanda maalum.
Wakishashika gari yako yani uwe mpole tu. Hata kama wamekosea wao, kwa hasira zile na jazba zao na uelewa wao mdogo, pamoja na ubabe, huchomoki hivihivi.
Yani bora upambane tu mmalizane huko nje maana ukishaingia yard ni mengine tena . Kasoro yao kubwa ni gharama. Gari ya kazi gharama yake laki 3. Kama uloleta ubishi ikabidi ivutwe hadi yard, gharama ya kuvuta ni laki 4 na haijalishi umbali toka yard yao. Wakati mwingine bora ukutane na askari kuliko hawa manyigu. Naweza kuandika sana ila nina maoni machache;
1. Gharama zao zichunguzwe. Ni ghali mno. Kosa la juu angalau iwe ni elfu 50. Hii itassidia mno kupunguza chuki, milolongo, na kupoteza muda.
2. Wakikushika wakupe na sababu zilizo wazi badala ya kuanza kupaniki.
3. Waache kuvizia.
4. Jiji lijitathmini kwa kazi hizi wanazotoa kwa kampuni hizi. Jiji linahusika pia kuwapa kiburi
Wakuu mnaweza kuongeza yenu na kipi kifanyike