Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema

KATI YA BATILDA NA LEMA YUPI ATIBUKA KIDEDEA?


  • Total voters
    52
Tunajua Mama Batilda anauzoefu wa kuwazuia wabunge wasijadili hoja ya RICHMOND.Ukiniuliza sababu za Omarlyas kumtetea Mama Batilda nashindwa kuelewa na pengine hii ni sababu tosha ufisadi unaendelea kutamalaki Tanzania.

Mtu yuko tayari kumtetea fisadi kwasababu ni ndugu yake,rafiki yake,jirani yake,kabila lake,dini yake,shangazi yake au mjomba.baba au chama chake.Omarlyas anaangukia katika kundi moja wapo niliyoyataja.Sina haja ya kubishana / ligi ya kipuuzi.


Na hili neno UFISADI nalo mnaelekea kulimaza makali yake na lisiwe na impact yoyote kwa mtanzania. Iweje utekelezai wa majukumu kama CHIEF WHIP likiwemo lile la kuhakikisha nidhamu miongoni mwa wabunge wa chama chake na pia lile la uwaziri ikiwemo kukubaliana na maamuzi ya pamoja ambayo Rais wake ameyatolea kauli ikawa UFISADI??? This shows kwamba hamna la kusema dhidi ya huyu mama ispokuwa kujaribu kutumia cheap propaganda na ubaguzi wa kijinsia kufanikisha maslahi yenu......Na inaonyesha ni jinsi gani mlivyo shallow katika masuala ya majukumu na maadili ya uongozi...
 
Inaonyesha wazi usivyojua hata hiyo kazi ya ubunge ama uwaziri ilivyo. Kabla kujaongelea suala la batilda alipokuwa Chief Whip ni muhimu ukatambua nini maana ya chief whip katika mabunge yetu. Na pia jaribu kuulizia nini maana ya uwaziri na prnciple ya collective responsibility katika governance of any society ndio uanze kutoa shallow critics kama unazozitoa hapa.

Pili kama wewe umeamua kumpigia debe LYIMO kwa ukabila wako usidhani kila mtu anamitazamo kama yako. Mimi sina undugu wala ujamaa na Batilda na wala hajawahi kunipa kitu wala sijawahi kufikiria kutaka kitu chochote kutoka kwake. Lakini nimefuatilia harakati zake kisiasa na kiuongozi ikiwemo hata kabla hajawa waziri na pia katika nafasi yake kama Chief Whip na najua perfomance yake lakini zaidi haiba ya heshima kwa watu ni moja ya nguzo kuu za uwezo wake kiuongozi na hicho ndicho kinafanyacho nimuone kuwa chaguo bora kuliko hao jamaa zako LEMA na LYIMO (ambaye naamini yaweza kuwa ndiye wewe).

Lakini pia ni siasa hovyohovyo kama zenu hapa ambazo nikilinganisha na ustaarabu na heshima ya Batilda ndio inanipelekea kujitoa mstari wa mbele kumpigania dhidi ya siasa chafu zenu??

Zaidi ni huu mtazamo hasi dhidi ya wanawake ambao mnao uonyesha hapa na katika kampeni zenu ndizo zinanitia moyo zaidi ya kusimama naye kwani to me male chauvinist and corrupt buffoon are all the same and have to be stopped from dominating our political arena...


Wewe unayejua zaidi maana ya Chief Whip mbona ujatueleza badala yake unakuja na utetezi wa kijinga.

Nani kakwambia nawapigia debe Lyimo na Lema ?.Hivi mtu unayemopigia debe ningeweza kusema ana elimu mbovu,ningeweza kusema alihusika pasipo shaka kumrubuni diwani wa Sombeti Bwana mawazo,ningeweza kusema alilipwa kitu kidogo kuondoa kesi mahakani dhidi ya Mhe F Mrema au ningeweza kusema mgombea wa TLP anatoka chama kilichogubikwa na mgogoro tena hajulikani vizuri kwa wapiga kura.Ningeweza kusema Mama Batilda ana elimu nzuri !.


Madhumuni ya kuanzisha mjadala ilikuwa kuwachambua wagombea wote kadri unavyowajua pia kutoa taarifa za mikutano ya kampeni ya wagombea wote ili wapiga kura wa Arusha waweze kuwachagua wagombea baada ya kuwa na taarifa sahihi.kwa masikitiko makubwa wamejitokeza wachangiaji wenye hoja dhaifu tena wanaotetea mambo yaliyo wazi kabisa.
 

Wewe unayejua zaidi maana ya Chief Whip mbona ujatueleza badala yake unakuja na utetezi wa kijinga.

Nani kakwambia nawapigia debe Lyimo na Lema ?.Hivi mtu unayemopigia debe ningeweza kusema ana elimu mbovu,ningeweza kusema alihusika pasipo shaka kumrubuni diwani wa Sombeti Bwana mawazo,ningeweza kusema alilipwa kitu kidogo kuondoa kesi mahakani dhidi ya Mhe F Mrema au ningeweza kusema mgombea wa TLP anatoka chama kilichogubikwa na mgogoro tena hajulikani vizuri kwa wapiga kura.Ningeweza kusema Mama Batilda ana elimu nzuri !.


Madhumuni ya kuanzisha mjadala ilikuwa kuwachambua wagombea wote kadri unavyowajua pia kutoa taarifa za mikutano ya kampeni ya wagombea wote ili wapiga kura wa Arusha waweze kuwachagua wagombea baada ya kuwa na taarifa sahihi.kwa masikitiko makubwa wamejitokeza wachangiaji wenye hoja dhaifu tena wanaotetea mambo yaliyo wazi kabisa.

Nafatilia mabandiko yako, hebu badili hiyo font Lucida Console haiko poa!
 
Waziri Burian adaiwa kuitenga CCM wilaya




Na Cynthia Mwilolezi



3rd September 2010


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni




headline_bullet.jpg
Ni katika mikakati ya kampeni
headline_bullet.jpg
Ameunda kikosi nje ya chama



Batilda%20Burian%287%29.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian



Kampeni za Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian, zinadaiwa kukigawa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya ya Arusha mkoani hapa.
Dk. Burian ambaye ni mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM, anadaiwa kutowashirikisha viongozi wa chama hicho wilayani humo katika kampeni zake.
Kampeni hizo zilizinduliwa na Mwenyekiti wa kampeni kitaifa wa CCM, Abdulrahaman Kinana.
Taarifa zinadai kuwa Dk. Burian aliteua kamati iliyohusika katika uzinduzi wa kampeni zake, huku akiwaweka kando viongozi hao.
Tukio hilo limetafsiriwa na wachunguzi wa mambo ya kisiasa mjini hapa, kwamba ni kielelezo kuwa hali si shwari ndani ya chama hicho, kutokana na hofu ya kuhujumiana.
Dk. Burian alipotafutwa na NIPASHE ili kuzungumzia suala hilo, hakupatikana na simu yake ya mkononi iliita pasipo kupokewa.
NIPASHE ilijaribu kumuandikia ujumbe mfupi wa maneno (sms) ulioonyesha kupokewa, lakini hadi tunakwenda mitamboni hakujibu, badala yake simu yake ilizimika.
Taarifa za ndani ya CCM wilaya ya Arusha zinadai kuwa Dk. Burian hakuwashirikisha viongozi wa CCM katika ya kampeni ikiwemo upangaji wa ratiba.
Kiongozi mmoja wa CCM wilayani humo alidai: "Mimi na wenzangu hatujui kitu chochote katika uzinduzi huu, pamoja na kuwa ni viongozi wa chama."
Kiongozi huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake kutajwa gazetini, alidai kuwa Dk. Burian aliiweka kando ratiba iliyoandaliwa na uongozi wa CCM wilayani humo, kupitia kwa Katibu wake, Salum Mpamba.
Kwa upande wake, Mpamba, alipoulizwa juu ya hali hiyo alisema ni mitazamo ya watu na kwamba chama hicho kipo pamoja na Dk. Burian katika kampeni hizo.
Alipoulizwa kuhusu ratiba ya uzinduzi wa kampeni hizo, Mpamba, alithibitisha kuwa shughuli hizo zilifanywa (kwa kiwango kikubwa ) na kamati maalumu ya Dk. Burian.
Kwa mujibu wa Mpamba kamati hiyo iliongozwa na mmoja wa wafanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha (jina tunalo).
"Huyu ndiye aliyekuwa akiratibu shughuli hizo, kwa asilimia mia na hata katika kura za maoni alikuwa mstari wa mbele," alisema.
Tukio jingine lililoonyesha dalili za kukosekana kwa umoja kwa CCM wilayani Arusha, ni pale Dk. Burian alipofanya ziara za viwandani pasipo kufuatana na viongozi hao, licha ya kwamba walikuwa na taarifa.
Lakini Mpamba alisema, "tuko pamoja na mgombea kwa kila kitu na katika kampeni za muda huu, mgombea anafanya vikao vya ndani na wananchi kabla ya kupanda majukwani kunadi sera za chama."
Mgombea wa CCM tangu alipozindua kampeni zake wiki mbili zilizopita, bado hajapanda tena jukwaani kunadi sera zake, kwa maelezo ya viongozi wa chama kuwa anafanya kampeni zake nyumba kwa nyumba.



CHANZO: NIPASHE

My take.

Huyu Mama Batilda kaonyesha jinsi alivyombinafsi hataki kushirikiana na uongozi wa CCM wilaya anayotaka kuwa mwakilishi wake.Kaamua kuunda timu yake ya kampeni nje ya utaratibu wa chama chake.Nilishangaa sana uzinduzi wa kampeni zake ulikuwa umekaa kifiesta fiesta muziki kwa wingi badala ya kunadi sera zake !.
 
TLP wilaya ya Arusha wamlalamikia mgombea wa CHADEMA Bwana G Lema na wafuasi wake kwa vitendo vya kubandua picha za mgombea ubunge wa TLP Bwana M E Lyimo.

Bwana Lema na wafuasi wake wamekuwa wakifanya zoezi la kubandua picha za mgombea wa TLP wakati wa usiku ili kutoa picha kwa wapiga kura ushindani ni baina yake na mgombea wa CCM Mama Batilda Buriani.

Bwana Lema na CHADEMA wamekuwa na hofu kubwa ya kugawana kura na mgombea wa TLP na kutoa mwanya mgombea wa CCM kushinda.

Tangu mgombea wa TLP alipozindua kampeni zake kwenye uwanja wa soko la kilombero viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakihaha kutafuata ushirikiano ili kunusuru jimbo la Arusha mjini lisichukuliwa na CCM.

Wagombea wote watatu wa CHADEMA waliowahi kushindania ubunge wametokea TLP lakini mara zote CHADEMA wamekuwa wakishika nafasi ya tatu huku TLP ikiambulia nafasi ya pili na CCM ikiibuka na ushindi mwembamba kwasababu ya kugawa kura.Tayari CHADEMA wamebaini hawawezi kushinda iwapo TLP imemsimamisha mgombea wake alianza kampeni kwa kishindo cha ajabu.

Bwana M E Lyimo ameshafanya kampeni katika kata tatu kwa mafanikio makubwa kuliko ilivyotarajiwa.

Mama Batilda Buriani tangu alipozindua kampeni zake kwenye kiwanja cha NMC amesitisha kampeni za majukwaani na ameamua kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba,hata hivyo wapiga kura wengi wanamshagaa kwasababu mji wa Arusha ni mkubwa mno sirahisi kumaliza kata kubwa kama Sokoni au sombeti.
 
Wakuu nimepata taarifa ambazo si rasmi kesho Jumapili muda wa kuanzia saa 2.30 usiku wagombea ubunge jimbo la Arusha watakuwa na mdahalo utakaorusha moja kwa moja bila zengwe wala chenga na TBC1.

Tafadhali wakaazi wa Arusha na watanzania wote kesho msikose kuangalia TBC1 ili tuweze kuwajua na kuwachambua wabunge wetu watarajiwa.
 
Dr Batilda Buriani akimbia[akacha] mdahalo wa wagombea ubunge Arusha mjini baada ya kuhisi atakumbana na maswali magumu na yanayoweza kumharibia nafasi ya kushinda ubunge.Wagombea ubunge wa vyama vinne walishiriki kwenye mdahalo huo uliofanyika Golden Rose jijini Arusha.
Bwana Godbless Lema wa CHADEMA, Bwana Macmillan Lyimo wa TLP , Bwana Gharib wa CUF na Mfyata Demokrasia Makini.
 
TLP wilaya ya Arusha wamlalamikia mgombea wa CHADEMA Bwana G Lema na wafuasi wake kwa vitendo vya kubandua picha za mgombea ubunge wa TLP Bwana M E Lyimo.

Bwana Lema na wafuasi wake wamekuwa wakifanya zoezi la kubandua picha za mgombea wa TLP wakati wa usiku ili kutoa picha kwa wapiga kura ushindani ni baina yake na mgombea wa CCM Mama Batilda Buriani.

Bwana Lema na CHADEMA wamekuwa na hofu kubwa ya kugawana kura na mgombea wa TLP na kutoa mwanya mgombea wa CCM kushinda.

Tangu mgombea wa TLP alipozindua kampeni zake kwenye uwanja wa soko la kilombero viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakihaha kutafuata ushirikiano ili kunusuru jimbo la Arusha mjini lisichukuliwa na CCM.

Wagombea wote watatu wa CHADEMA waliowahi kushindania ubunge wametokea TLP lakini mara zote CHADEMA wamekuwa wakishika nafasi ya tatu huku TLP ikiambulia nafasi ya pili na CCM ikiibuka na ushindi mwembamba kwasababu ya kugawa kura.Tayari CHADEMA wamebaini hawawezi kushinda iwapo TLP imemsimamisha mgombea wake alianza kampeni kwa kishindo cha ajabu.

Bwana M E Lyimo ameshafanya kampeni katika kata tatu kwa mafanikio makubwa kuliko ilivyotarajiwa.

Mama Batilda Buriani tangu alipozindua kampeni zake kwenye kiwanja cha NMC amesitisha kampeni za majukwaani na ameamua kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba,hata hivyo wapiga kura wengi wanamshagaa kwasababu mji wa Arusha ni mkubwa mno sirahisi kumaliza kata kubwa kama Sokoni au sombeti.

Hivi unadhani JF ni jukwaa la maimuna? Kama hii sio propaganda ya LYIMO sasa itakuwa nini? Jjiandae na maumivu kama waliyoyapata wenzako kule Kyela kutokana na kujidanganya kwao na strategy za kilaghai......wanadanganya hadi wanaamini udanganyifu wao..
 
Hivi unadhani JF ni jukwaa la maimuna? Kama hii sio propaganda ya LYIMO sasa itakuwa nini? Jjiandae na maumivu kama waliyoyapata wenzako kule Kyela kutokana na kujidanganya kwao na strategy za kilaghai......wanadanganya hadi wanaamini udanganyifu wao..



Omarilys sina shaka yoyote wewe ni maimuna wakutupwa nadhani ungekaa kimya nisingejua.

Ukisoma post zote na hata post uliyokimbia kuijibu utagundua kitu kimoja kikubwa.Nimenukuu maneno ya viongozi wa TLP waliokuwa wakilalamika nikaongeza na yangu jinsi CHADEMA na TLP wasivyoweza kushinda ubunge Arusha bila kuungana.Fuatilia takwimu utagundua CCM kwenye chaguzi zote imekuwa ikipata ushindi mdogo sana kwasababu hivi vyama viwili vimekataa kukaa pamoja na kumsimamisha mgombea mmoja.

Uchaguzi wa mwaka 2005 kura za wagombea wa TLP na CHADEMA zilikuwa nyingi sana kupita mgombea wa CCM aliyeshinda kwa mizengwe.Wapiga kura wa Arusha mara zote wamekuwa wakiangushwa na vyama vya upinzani kwasababu ya maslahi ya vyama vyao.

Mama Batlda tangu alipozindua kampeni zake NMC aliacha kufanya kampeni mpaka majuzi alianza na kata ya Sombetini ambayo ni kata yenye wapiga kura wengi sana na pengine ndiyo yenye kuamua mshindi wa kiti cha ubunge Arusha.

Kusema kwamba Lyimo kafanya kampeni katika kata tatu kwa mafaniko makubwa si kuwa mpiga debe bali kukuarifu wewe na wasomaji wote.

Nilitegemea ungeanza kujibu post # 82 & 84.
 
Batilda, Lema watafutana Arusha


maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 15 September 2010

buriani_206.jpg



KINYANGANYIRO cha ubunge katika jimbo la Arusha Mjini, kimepamba moto. Wagombea watano kutoka vyama tofauti wanachuana kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Felex Mrema (CCM).
Mrema aliyeongoza jimbo hilo kwa zaidi ya miaka minane, alishindwa kupenya kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyemwangusha kigogo huyo wa siasa za Arusha, ni Batilda Burian, waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais (mazingira).
Kati ya wagombea hao watano, mchuano mkali upo kwa wagombea wawili, Godbless Lema – mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Batilda anayewania nafasi hiyo kupitia CCM.
Wagombea wengine watatu, Mc Milian Lyimo aliyejitosa katika kinyang’anyiro hicho kupitia Tanzania Lebour Party (TLP), Mohamed Balawi anayegombea kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na Joseph Mafatwa wa Demokrasia Makini, wanaonekana kama wasindikizaji.
Tayari msimamizi wa uchaguzi Arusha mjini Rafael Mbunda ameshamwandikia barua Lema kumwonya kwa kile alichodai, “kutumia lugha chafu dhidi ya Batilda.”
Mbunda anasema katika barua yake kuwa Lema alitoa maneno yaliyokatazwa na maadili ya uchaguzi. Hakutaja maneno hayo.
Hata hivyo, kujitosa kwa Lyimo katika kinyang’anyiro hiki kunaweza kumpa ahueni Baltida, ingawa kunaweza kumwangamiza pia.
Kwa mfano, watu ambao hawamtaki Lema wanaweza kumpa kura Batilda.
Lakini Batilda anakabiliwa na kibarua kigumu cha kujieleza mbele ya wananchi kuhusu uzawa wake na kile kinachoitwa, “mahusiano yake na mumewe.”
Wapinzani wa Batilda wanadai kuwa mwanasiasa huyo, si mzaliwa wa mkoa wa Arusha na wala haishi mkoani humo. Wanamwita wakuja.
Wanasema ameolewa Zanzibar na anaishi Zanzibar, na kwamba mumewe Othumani Masoud, ambaye ni mkurugenzi wa mashitaka Zanzibar (DPP), ni mwenyeji wa kisiwa cha Pemba.
Changamoto nyingine ni ule utamaduni wa watu wa Arusha kumweka mwanamke katika nafasi ya pili. Tangu jimbo la Arusha lianzishwe miaka zaidi ya 40 iliyopita, halijawahi kuongozwa na mwanamke.
Wapinzani wa Batilda wanafika mbali zaidi.
Wanasema mgombea huyo wa CCM ameletwa maalum na kundi la watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini ili kufanikisha mkakati wa kundi hilo “kushika dola mwaka 2015.”
Lakini mwenyewe amekana baadhi ya madai hayo. Kwanza, anasema yeye si wakuja kama ambavyo wapinzani wake wa nje na ndani ya chama wanavyosema.
Katika kukabiliana na madai hayo, Batilda ameamua kutembea na mama yake mzazi, Hawa Mairo ambaye inadaiwa kuwa aliwahi kuwania ubunge katika jimbo hilo huko nyuma. Hakufanikiwa kushinda.
Katika baadhi ya mikutano yake aliyoifanya amekuwa akikana kuwa yeye ni wakuja. Anasema amezaliwa mkoani Arusha na kupata elimu yake ya msingi na sekondari mkoani humo.
Pili, Batilda anakana madai kuwa anaishi Zanzibar, ingawa anakiri kwamba ameolewa huko. Anasema anaishi Arusha.
Tatu, Batilda anakiri kuwa mume wake ni Othumani Masoud, mwajiriwa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), lakini anasema mume wake ndiye huwa anamfuata yeye.
Hata hivyo, utetezi huu mpya umezua mjadala mwingine. Kwamba haiwezekani Othumani kumfuata Batilda Arusha, wakati mume wake huyo ana mke mwingine Zanzibar.
Pamoja na kwamba katika maeneo mengine hoja kwamba Baltida kuolewa Zanzibar inaweza kuwa dhaifu, lakini kwa wenyeji wa mikoa hii ya Kaskazini, hili si jambo la kulipuuza hata kidogo.
Wengi wanaona kuwa hatua yake ya kuolewa Zanzibar, inamwondolea sifa ya kuwa sehemu ya kizazi cha Arusha; kutokana na kuwa na familia Zanzibar alipaswa kubaki Zanzibar na kufanya siasa zake visiwani.
Jingine ambalo wapinzani wake wanamtwisha ni kule kuzunguka katika wizara tano katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Wanasema, mzunguuko huo ni kielelezo cha kushindwa kazi hivyo anabebwa tu.
Hoja nyingine ambayo inaonekana kumtafuna, ni udini. Katika siku za karibuni wametokeza watu wasiofahamika wakipita na kusambaza ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) unaotaka waislamu kumchagua Batilda kwa kuwa ni muislamu mwenzao.
Hata hivyo, Batilda anaonekana kupata nguvu hasa baada ya ushindi wake mkubwa katika kura za maoni.
Tayari mgombea huyo amesimikwa cheo cha kabila la Kimasai anachopewa mwanamke (Leigwanaki), kama dalili za kukubalika na wazee wa kabila hilo. Cheo kama hiki amewahi kupewa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.
Naye Lema anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, baada ya kushindwa kwa mizengwe mwaka 2005, hayuko salama.
Katika kinyang’anyiro cha mwaka 2005, Lema aligombea kupitia chama cha TLP; alitangazwa kupata kura 47,000 dhidi ya 51,000 za mpinzani wake, Felex Mrema.
Hadi sasa, wengi wanaamini kuwa Lema ndiye aliyeshinda uchaguzi huo, bali CCM walitumia hila kumtangaza Mrema.
Wanasema kabla ya matangazo ya jumla kutolewa, Lema alikuwa amemwacha Mrema mbali. Wanasema alikuwa mbele kwa zaidi ya asilimia 10.
Chanzo cha tuhuma dhidi ya Lema kinatokana na kushindwa kwa uongozi wa TLP kuendesha kesi iliyofunguliwa mahakamani.
Lema anasema kushindwa huko kumetokana na mahakama kutaka chama chake kuweka dhamana ya Sh. 5 milioni kama sheria inavyotaka na Sh. 27 milioni alizotaka kulipwa wakili.
“Tulishindwa kuendesha kesi hii baada ya chama kushindwa kumlipa mwanasheria na kuweka dhamana ya Sh. 5 milioni iliyotakiwa na mahakama,” anaeleza. Anasema wakili wao alitaka kulipwa nusu ya fedha hizo.
Anasema, “Tukaamua kuitisha mkutano wa hadhara ili kuomba fedha kutoka kwa wananchi, lakini mkutano uliohudhuriwa na watu zaidi ya 5,000 ulichanga Sh. 80,000 tu.
Hiyo ndiyo sura nzima ilivyokuwa,” anasema Lema kwa sauti ya masikitiko.
Pamoja na Lema kukana madai hayo, bado wapinzani wake wa kisiasa jimboni humo wanaendelea kumtuhumu kuwa aliuza jimbo.
Bahati mbaya, baadhi ya wanaotuhumu sasa, ni viongozi wa TLP ambao wanaonekana kufunga ndoa na CCM kuhakikisha kuwa Lema hashindi ubunge wa jimbo hilo.
Tuhuma nyingine ambazo wapinzani wake wamekuwa wakimtwisha wakati alipokuwa TLP ni kupigia debe mgombea udiwani wa CCM katika kata ya Sombetini, Alfonce Mawazo.
Awali Mawazo alikuwa diwani wa TLP. Lakini aliondoka katika chama hicho kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi wake wa mkoa.
Lema anajitetea kwamba alifanya hivyo si kwa maslahi binafsi, bali ni kutokana na uhusiano wake wa karibu na Mawazo.
Pamoja na hayo bado Lema anaweza kushinda. Katika baadhi ya mikutano yake ya kampeni, ameonyesha umahiri mkubwa wa kujenga hoja na kujibu tuhuma dhidi yake. Wengi wanamwona kuwa ndiye anayestahili kuwa mbunge wa jimbo hili.
Gazeti toleo na. 206
 
siri ya Waarusha ni kuweka mtawala atakayefanikisha sera yao ya kurudisha ardhi wanayowauzia Wachaga na wapare eti waliuza bei nafuu na sasa walipwe kwa thamani ya sasa. @Mwarusha hapewi nafasi hata iweje.
 
Mkutano wa Dr. Batilda hapa shule ya msingi ya Burka Arusha bado haujaanza ni burudani tu zimeshamiri wakisubiri watu.............

Dada yangu kukosa ule mdahalo matunda yake sasa yanaanza kujionyesha. Mdahalo ungelimpa nafasi ya kujitangaza na kujisafisha mengi ya ukweli na ya kuzuliwa lakini sasa it is too late to catch a bolted horseeeeeeeeeeeeeeeee after Mr. Makamba has left the stable looseeeeeeeeee.

Jamaa zangu wanasema baada ya uchaguzi kama JK akidondoka itabidi awajibike yeye na timu yake nzima ya kamati kuu vinginevyo watampigia kura ya kusa imani nayeeeeeeeeeeeeeeee

Hivi ile sheria ya kumaliza mkutano saa kumi na mbili sijui ni nani atakayeisimamia maana huyu kigogo wa CCM hata Takukuru na NEC wanamhara ile mbaya sijui ubavu wake unatokea wapi? Hivi sasa ni saa kumi na nusu..........Anazo saa moja na nusu awe amefungasha virago vyake vya mkutano huuuu sasa sijui itakuwajeeeeeeeeeeeeeeee

Hiki kiti cha ubunge wa Arusha mjini yalekea wapiga kura wa hapa watamchagua Godbless Lema wa Chadema ambaye mikutano yake hufurika watu.

Wengi wanaamini Godbless alishinda mwaka 2005 lakini kura zake Mrema wa CCM alizichakachua ile mbayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Sasa wapiga kura wanataka kulipiza kisasi cha maumivu ya mwaka 2005 kwa mama huyu kigogo wa CCM kwa kuhakikisha anadondoka pwaaaaaaaaaaaaaaaaa

Jamaa zangu wa CCM naona hawanichangamkii hata kidogo lakini uzalendo wa kitaifa mbele na mengineyo tutayaangalia siku za usoni.........................

Nipo hapa nasubiri kujionea mambo live sitaki kusimuliwa tenaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
BAtilda Kweishnei. Ni demu wa LE na kila mtu anajua hilo. Labda atapigiwa kura na kina mama wa hapo uswahilini lakini kwingine hamna kitu.Ajabu ni kwamba haji hata kuongea sentensi iliyonyooka.
 
CCM kupoteza jimbo la Ar. Mjini ni dhahiri na ningewashauri wasipoteze muda kupiga Kampeni. Hata wale waliolazimishwa/kupewa pesa kuweka bendera kwenye viford sasa wamezitupa na Bendera za Chadema zinashamiri. Uongozi wa Chadema Mkoa leteni vipeperushi vingi maana watu wanavihitaji.
 
Back
Top Bottom