Naongezea Wasifu: Kuhusu Lema ni ukweli kabisa wala bwana/bibi Ngongo haujakosea, kwa kweli ni mtu wa bla bla, hapa Arusha kuna wakati alianzisha ki-organization sijui Positive kitu gani kinaendelea hapo mbele lakini sikumbuki vizuri hayo maneno mengine. Kwa kweli anaushawishi mkubwa sana kwani alifanikiwa kuwavuta vijana wengi wakiwemo wasomi, lakini baada ya muda kilichotokea hapo sijajuwa ni nini, hila chama kilisambaratika. Biashara yake nyingine anamiliki min-supermarket maeneo ya mianzini, arusha. Kwa sasa pia anajishughurisha na uandishi wa vitabu vya dini, sijui kama mnajua kwamba anajifanyaga mtu wa dini sana yaani kama mlokole flani hivi. Na mitaa ya kijiwe ni pale Sinka Hotel watu wa ARusha nadhani mnaifahamu hii mitaa ni ya mabroker wa mawe. Nawakilisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Kuhusu siasa: Yale mambo ya Sombetini yalitokea, ni kweli ana bla bala, lakini siasa si ndo bla bla jamani, kwani kuna uabaya gani? Kama anaweza kushawishi wapiga kura wakamchagua yeye na chama chetu ndivyo tunavyotaka kwani CCM tumeichoka. Mbona Jacob Zuma ana elimu ndogo na ni raisi tena wa nchi iliyoendelea kama South Africa, nini kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha. Mbona aliyetoka ni msomi tena si msomi kidogo, mwanasheria aliyewahi kushika nyadhifa serikalini ametufanyia nini? Kwa miaka yote ambayo amekuwa Mbunge wa ARusha Mjini. Kwa hiyo kuwa karibu na wananchi/wapiga kura ni advantage kwa Lema na kwa chama chetu, angalau ana mambo ya kuwapelekea viongozi wa juu wa chama chetu(CHADEMA) yaani feedback kwa sababu yuko karibu hivyo cha msingi atashirikiana na kina Zitto na mpiganaji wetu Dr. Slaa wataleta maendeleo, maendeleo sio vyeti hata wasomi wanachemsha.