Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema

KATI YA BATILDA NA LEMA YUPI ATIBUKA KIDEDEA?

  • Total voters
    52
Chadema wataka kumbadili Lema baada ya kupata taarifa za ndani kuwa CCM wamejiandaa kumlipua Lema wakati wa kampeni.Bwana Mallah tayari ameombwa kuokoa jahazi lisiende mrama hasa wakiaangalia muda mdogo uliobaki.Bwana Lema alifukuzwa Tlp kwa kosa la kumshawishi Mawazo kujiunga na CCM na kuondoa kesi ya kupinga ushindi wa Bwana F Mrema mahakama kuu baada ya kupewa kiwanja,nyumba na fedha alizofungulia min super market iliyoko eneo la mianzini.
 
Mama Batilda Salha Buriani muda huu anarejesha fomu na msururu mkubwa wa magari,pikipiki,baiskeli na watembea kwa miguu.Urejeshaji wa fomu umeandamana na bendera za CCM na gari lenye kupiga muziki mkubwa wa kumsifia Mama Batilda.Msafara wa Mama Batilda tayari umesababisha kero ya msongamano wa magari.

Mama Batilda yuko ndani ya gari aina ya Land cruiser anapungia wananchi mkono huku jeshi la polisi likiwa limetoa askari kibao wanoonekana wakimlinda Mama kama mkuu wa nchi.habari za uhakika baada ya kurejesha fomu kutakuwa na pilau la Nyumbu la kukata na shoka,nitajaribu kujipenyeza ili kuwaletea habari za uhakika bila chenga.
 
Mama Batilda Salha Buriani muda huu anarejesha fomu na msururu mkubwa wa magari,pikipiki,baiskeli na watembea kwa miguu.Urejeshaji wa fomu umeandamana na bendera za CCM na gari lenye kupiga muziki mkubwa wa kumsifia Mama Batilda.Msafara wa Mama Batilda tayari umesababisha kero ya msongamano wa magari.
Ngongo, asante kwa uchambuzi yakinifu kuhusu kinyanganyiro cha ubunge Arusha. Ninachokiona hapo ni kwa TLP na Chadema kugawana kura za upinzani, hivyo CCM kupita kwa ulaini. Mikoa ya Kaskazini ni mikoa yenye vuguvugu la upinzani, watu hawauzi uhuru wao kwa shibe ya siku moja 'pilau', au kwa t-shirt na kofia, lakini inapotokea wapinzani kupingana, hivi ni vita vya panzi, faida kwa kunguru.

Uongozi ni kipaji na uwezo na sio elimu, japo elimu ni just an added advantage, kama mtu ana uwezo wa uongozi hata darasa la saba, atakuwa kiongozi bora, ndio maana kuna mababu zetu hawakusoma, lakini walikuwa viongozi wazuri tuu wenye busara. Wapinzani lazima waungane, vinginevyo Arusha hiyo...CCM!.
 
Heshima kwako Pasco,

Nakubaliana na hoja yako TLP na CHADEMA wanaweza kugawana kura na kutoa mwanya mgombea wa CCM kushinda.CHADEMA walikuwa na nafasi kubwa wakati huu kutwa jimbo la Arusha kama wangemsimamisha mgombea mzuri ambao wako kibao ndani ya chama.Bwana Godbelss Lema ni mgombea wa makao makuu [Dar es Salaam],wapo wagombea wawili wazuri ambao CHADEMA mkoa na Wilaya walipanga kumsimamisha mmojawapo [Mallah & Mpinga] lakini kwa msangao wa wengi makao makuu wakamteua Bwana Lema.CHADEMA wilaya ya Arusha zipo kambi mbili moja inaunga mkono makao makuu na nyingine inapinga makao makuu kuwachomekea mgombea wasiemtaka tena wanaejua udhaifu wake nje ndani.

Nakubaliana tena na hoja yako kwamba uongozi ni kipaji na uwezo lakini pia elimu ina nafasi yake kubwa sana.Kuna mambo ya hovyo yaliyowahi kufanywa na Bwana G Lema amabayo ukiyatafakari unagundua pia ukosefu wa elimu ulichangia sana.Mkuu Pasco unaweza kuchagua wabunge wenye elimu ya darasa la saba au chini ya kiwango hicho Korogwe,Iringa,Mbeya na Rorya lakini mbunge mwenye elimu hiyo hafai kabisa Arusha hasa tukizingatia mazingira yake kama mji wenye pilika pilika za mikutano ya kimataifa,makao makuu ya EAC na mashirika mbali mbali ya kimataifa.
 
Urudisha fomu Mama Batilda umeambatana na vituko vyake.

Mtangazaji maarufu wa promosheni [Raha Promotion] hapa mjini Arusha Bwana Rama amekumbana na gharika ya hasira ya vijana waliohaidiwa kiasi cha tsh 1500/= kwa kumsindikiza Mama Batilda.Bwana Rama alijikuta akizidiwa na wingi wa vijana waliokuwa wakidai kupewa kiasi hicho cha fedha kama malipo ya kumsindikiza mgombea ubunge kurejesha fomu.Taarifa za ndani zinafichua zaidi kwamba wenye magari walipewa mafuta na tsh 20,000/=,wenye pikipiki mafuta na tsh 10,000/= wenye baiskeli 5,000/= na waenda kwa miguu 1,500/=.Pia kulikuwa wasindikizaji waliokuja na mabasi ya abiria ambao haijulikani walilipwa kiasi gani.

Heshima kwako Pasco,

Nakubaliana na hoja yako TLP na CHADEMA wanaweza kugawana kura na kutoa mwanya mgombea wa CCM kushinda.CHADEMA walikuwa na nafasi kubwa wakati huu kutwa jimbo la Arusha kama wangemsimamisha mgombea mzuri ambao wako kibao ndani ya chama.Bwana Godbelss Lema ni mgombea wa makao makuu [Dar es Salaam],wapo wagombea wawili wazuri ambao CHADEMA mkoa na Wilaya walipanga kumsimamisha mmojawapo [Mallah & Mpinga] lakini kwa msangao wa wengi makao makuu wakamteua Bwana Lema.CHADEMA wilaya ya Arusha zipo kambi mbili moja inaunga mkono makao makuu na nyingine inapinga makao makuu kuwachomekea mgombea wasiemtaka tena wanaejua udhaifu wake nje ndani.

Nakubaliana tena na hoja yako kwamba uongozi ni kipaji na uwezo lakini pia elimu ina nafasi yake kubwa sana.Kuna mambo ya hovyo yaliyowahi kufanywa na Bwana G Lema amabayo ukiyatafakari unagundua pia ukosefu wa elimu ulichangia sana.Mkuu Pasco unaweza kuchagua wabunge wenye elimu ya darasa la saba au chini ya kiwango hicho Korogwe,Iringa,Mbeya na Rorya lakini mbunge mwenye elimu hiyo hafai kabisa Arusha hasa tukizingatia mazingira yake kama mji wenye pilika pilika za mikutano ya kimataifa,makao makuu ya EAC na mashirika mbali mbali ya kimataifa.
.
Ngongo, sina ubishi kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtu yoyote na inapokuja kwa mgombea ni muhimu zaidi, kati ya majimbo yaliyoitekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100% ni jimbo la Masilingi, lakini kwenye kura za maoni, CCM wamempiga chini kisa miongoni mwa washindani wake kuna aliyekuwa nshomile zaidi, na kwa wenzetu kadri ulivyo nshomile zaidi, ndivyo unavyoheshimika zaidi.

Kwa Moshi na Arusha mjini, heshima ya mtu ni fungu ambalo hujionyesha kwa life stlye, unafanya nini, unaishi vipi, unaendesha gari gari, unakunywa wapi, na unajichanganya na kina nani. Kama kijana yuko fiti hizo idara nyingine zote, bado jimbo la Arusha lina nafasi ya kuangikia upinzani.Tatizo la huyo mgombea wa Chadema kwa upande wangu, ni ubishoo tuu wa kutaka mambo makubwa, kujifanya yuko juu ili hali ni mtu wa kawaida tuu, ila kwa kukubalika na machalii wa mjini hapo, anakubalika. Tatizo linabaki lile lile la kugawana kura za upinzani, na kumpa ushindi mwembamba mamaa wa muzee!.
Natamani sana kuona wabunge wengi wa upinzani wakiingia bungeni, lakini kwa mwendo huu wa fragmented opposition, wimbo ni ule ule uliochusha-CCM!.
 
Wakuu leo majira ya saa 3 asubuhi askari polisi FFU walikuwa wakifanya mazoezi ya jeshi mitaani kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu.Nimepeta mshtuko kidogo kuona askari wakikimbia mabarabarani na vifaa vya kijeshi huku wakisababisha foleni zisizo na maana.Nadhani jeshi la polisi limeamua kufanya mazoezi uraiani kama mkakati wa kuwatisha wananchi,mambo hayo hayakuapata kutokea kwenye chaguzi zilizopita iweje waamuae kufanya sasa.

Tayari Chadema wamezindua kampeni zake maeneo ya Arusha by Night [St Thomas Hospital] madiwani na mgombea ubunge.Mgombea ubunge kata ya Sekei Mallah anaonekana anaweza kushinda kata hiyo inayoshikiliwa na meya wa sasa.Mgombea ubunge G Lema amepwaya sana ukimlinganisha na Mallah ambae aliwahi kugombea ubunge mwaka 2000 na kudhulumiwa na aliekuwa mbunge wa Arusha F Mrema.G Lema hana hoja za maana ameshindwa kujenga hoja akipewa ubunge atawafanyia nini wananchi wa Arusha.
 
Wakaazi na wenyeji wa mji wa Arusha nchi yetu iko kwenye matayarisho ya uchaguzi mkuu October 2010.Nimeona ni vyema na haki tukawajadili wagombea ubunge wa vyama vitatu ambavyo nini hakika wataleta ushindani mkali.

Mgombea ubunge wa CCM
Mama Batilda Salha Buriani kazaliwa mwaka 1965
chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1985 – 1988 B.A [Public Admin & International Relation ]
Mwaka 1990 – 1991 alichukua shahada ya pili katika chuo kikuu Sussex M.A [Development Studies]
mwaka 1992 – 1997 alichukua shahada ya uzamivu [Phd] chuo kikuu London .
Bi Batilda mpaka sasa ni waziri wan chi makamu wa Rais mazingira.

Mapungufu yaMama Batilda Salha Buriani ni mengi lakini nitajaribu kuyatupia macho machache wengine mnaweza kuongeza kadri mnavyomfahamu.
Bi Batilda Salha Buriani wakati akiwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Bunge na uratibu [ chief Whip ]aliwahi kumlima barua ya onyo kali Mama Anna kilango Malechela kwa kosa kubwa la kuzungumzia mradi wa Richmond bungeni.Hili ni kosa kubwa sana kwani baadae ilikuja kujulikana mradi wa RICHIMOND ulikuwa wa kifisadi,kwa maneno mengine Mama Batilda ni miongoni mwa wabunge/ mawaziri waliokuwa wakitetea ufisadi ndani ya serekali,bungeni na chama .

Mama Batilda Salha Buriani kampeni zake ziligubikwa na rushwa na nguvu ya ajabu nyuma yake ilikuwa ikihakikisha anashinda tiketi ya kugombea ubunge kupitia CCM.Vyombo vya dola hasa UWT/TAKUKURU vilihakikisha hakuna wa kumzuia kushinda.Wakaazi wengi wa mji wa Arusha wanajua Mama B Salha Buriani alisaidiwa sana na Mbunge wa Monduli Bwana E N Lowassa kwa faida za kisiasa siku za usoni.Mama Batilda alihudhuria uzinduzi wa nyimbo za kwaya KKKT mwanzoni mwa mwaka huu,wengi tulijua alikuwa akijiandaa kugombea ubunge wa Arusha mjini.E N Lowassa mara nyingi amekuwa akimtumia Askofu Thomas Laizer kwa manufaa yake ya siasa kitu ambacho tayari kimeanza kulalamikiwa na waumini wengi wa KKKT.

Mradi wa ujenzi wa barabara Arusha – Musoma kupitia mbuga ya wanyama ya Serengeti ni udhaifu mkubwa wa Mama Batilda Salha Buriani kama waziri anae shughulikia mazingira.Mama Batilda kaamua kukaa kimya pengine kufunika kombe mwanaharamu apite lakini akae akijua wakaazi wengi wa mji wa Arusha wanapata mapato mengi kwasababu ya utalii.Ujenzi wa barabara kupitia mbuga ya wanyama ya Serengeti kutaharibu mazingira pia kunaweza kusababisha uhamaji wa nyumbu kukoma kabisa.Inashangaza mtu wa aina hii anataka kuwa mbunge wa mji unaongoza katika shughuli za utalii Tanzania.
Ikiwa Mama Batilda Salha Buriani atachaguliwa kuwa mbunge wa Arusha,hakika utakuwa ni ushindi mkubwa wa wanamtandao bila shaka nguvu ya wanamtandao itaongezeka maradufu.Mama Batilda atakuwa ni mbunge wa aliyempachika na wala hataweza kuwakilsha vyema wapiga kura wa Arusha mjini.

Mgombea Ubunge wa CHADEMA
Godbless Lema elimu yake haijulikani kabisa na ni moja ya mambo yaliyochangia kupunguza kura zake katika uchaguzi wa mwaka 2005.Anadai anacheti cha Computer lakini hatakia kutaja jina la chuo alichosoma wala mwaka aliomaliza.Anadai alimaliza kidato cha sita lakini hataki kutaja jina la shule aliyosoma wala mwaka na alama alizopata ??????????.
Godbless Lema haijulikani anafanyakazi gani haswa, mara nyingi anapenda kujiita mfanyabiasha za madini na wakati mwingine anadai kununua vitu mbali mbali Dubai & Japan.Hana ofisi ya biashara inayojulikana muda wake mwingi anapenda kukaa mitaani kuzungumzia mambo asiyoyajua vyema kwa kujidai anayajua kuliko mtu mwingine.

Godbless Lema ni dalali mzuri wa siasa za upinzani anajua kucheza karata zake vizuri sana huku akiyatanguliza maslahi yake binafsi.Bwana Lema anahusika bila shaka yoyote alifanikisha deal ya kumuondoa Diwani wa TLP Sombeti Bwana Mawazo na kumpeleka CCM kwa ujira wa pikipiki za mafisadi na kiwanja.Baada ya kutimuliwa TLP akakimbilia CHADEMA na amefanikwa kujinyanyua hadi akapitishwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA .wanamageuzi bado wanakumbuka jinsi alivyoiondoa kesi ya kupinga ushindi wa Mheshimiwa Felex Mrema mahakamani bila kuwashirikisha viongozi wa chama wakati chama kilitoa fedha za kugharamia kesi.Ilikuja kubainika Bwana Lema alipewa kitu kidogo ili kuiondoa kesi mahakamani.

Godbless Lema akifaniwa kuwa mbunge wa Arusha mjini ataongeza idadi wa viti vya wabunge wa upinzani jambo ambalo ni jema na afya kwa demokrasia ya Tanzania lakini hatakuwa na mchango wa maana bungeni kama akina Dr Slaa na Zitto Kabwe sana sana ataongeza idadi tu.
Godbless Lema anategemea zaidi umaarafu wa CHADEMA kuchaguliwa anatamani sana wapiga kura wasahau alivyorubuniwa na CCM mara mbili.
[1] Kumpeleka Mawazo CCM.
[2] Kufuta kesi ya kupinga ushindi wa Felex Mrema .
[3] Atapenda wapiga kura wasihoji elimu yake.
[4] Atapenda wapiga kura wasihoji kazi yake.
[5] Atapenda wapiga kura wampigie kura kwasababu ya umaarafu wa CHADEMA na Dr Slaa.

Mgombea ubunge wa TLP
Bwana Max Lyimo kazaliwa mwaka 1964
Bachelor of Science Degree Chuo kikuu cha Dar
Masters of Business Administration Chuo kikuu huria Tz

Kuingia kwa Bwana M Lyimo kugombea ubunge wa Arusha mjini ni changamoto ambayo CCM na CHADEMA hawakutarajia hasa ikizingatiwa TLP katika chaguzi zote imekuwa ikileta upinzania mkubwa kwa CCM.

Udhaifu pekee wa Bwana Lyimo ni kutojulikana na wakaazi wengi wa mji wa Arusha na vitongoji vyake,chama chake kinatakiwa kutilia mkazo mkubwa kumtambulisha hasa ikizingatiwa kuongezeka kata za Moshono,Olkeriani na nk pia cha cha TLP ambacho kilikumbwa na mgogoro tofauti na cha CHADEMA ambacho muda mwingi walikuwa wakikijenga chama kupitia operesheni Sangara.

Bwana M Lyimo akichaguliwa kuwa mbunge wa Arusha ataongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni.Bwana Lyimo hatategemea umaarufu wa chama chake ambao haupo kwasasa.Nimemsikiliza Bwana Lyimo mara moja tu katika mkutano wake wa kujitambulisha eneo la soko kuu.Ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kujenga hoja.Anaweza kuwa mpambanaji kama akina Dr Slaa na zitto Kabwe.

Nategemea michango na mijadala ya kujenga ili jimbo la Arusha mjini lipate mbunge makini,mwadilifu,mbunifu na zaidi ya yote mwenye kuangalia maslahi ya taifa bila kujali jimbo analoliwakisha.
Naomba kuwasilisha

Mnyonge mnyongeni lakin haki yake mpeni.

Dr Batilda Salha Buriani ni chaguo la wengi huko Arusha. Kila mwanadamu ana mapungufu yake na hakuna mwanadamu mkamilifu.

Buriani atapita kwa kishindo sana huko Arusha mjini. Pita pale triple A uone gari lake la campaign ujisuze na roho yake.

Moto mdundo shemeji yetu Batilda. Mtoto wa Njiro
 
Heshima kwako HM Hafif,

Mkuu nilitegemea ungesoma hoja vizuri na ungekuja na majibu ya kukataa au kuunga mkono yote niliyoandika kuhusiana na Mama Batilda Buriani badala yake unakuja na viroja kwamba ni chaguo la wengi Arusha.Mkuu hata Lowassa pamoja na madudu yake kibao bado ni chaguo la wengi Monduli vivyo hivyo Rostam ni chaguo la wengi Igunga.
 
Hii imekaaje CCM wamegawa baiskeli nyingi kwa wanachama wake kipindi hiki cha kampeni je sheria ya uchaguzi inaruhusu haya mambo kufanyika ?.TAKUKURU walikuwa wanakamata simu,fedha na cherehani wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama cha mapinduzi mbona sasa siwaoni wakiwakamata watoa rushwa za baiskeli na pikipiki.
 
Wakuu nilikuwa nikifuatilia madai ya Mama Salha Batilda dhidi ya Bwana Lema ili kujua ni matusi ya aina gapi yasiyoweza hata kutamkwa.Kwanza nikiri chanzo changu cha mwanzo kilikuwa ni jamaa mmoja ambae nilikuja kugundua ni kada wa CCM.

Matusi ambayo Mama Batilda anayodai alitukanwa na Godbless Lema ni kama ifuatavyo.

[1] Mama Batilda kaolewa Zanzibar anatakiwa akae na mume wake huko Zanzibar ili kudumisha ndoa yake, Arusha anahitajika mbunge atakaekuwa na muda wa kuwahudumia wananchi wake !.

[2] Mama Batilda ni msomali kwanini aendi Somalia kuwasaidia ndugu zake wanauana kama nzige anataka kuwa mbunge Tanzania na kuleta siasa za udini kwa kupeleka siasa kwenye misikiti kwamba waumini wasiwachague makafri.

[3] Mama Batlda amewahi kuolewa mara tatu ni kwanini hawezi kukaa na mume mmoja je mwanamke wa aina hii anafaa kuwa mbunge wetu ?.

[1] Maoni yangu ni kweli Mama Batilda kaolewa huko Zanzibar lakini tunao mfano mzuri wa Mama Anna kilango Malechela lakini ni mbunge wa Same bado sioni tatizo labda kama mumewe amekilalamikia chama cha mapinduzi kumtengenisha na mkewe.

[2] Ni kweli Mama Batilda ni msomali lakini mama yake ni mwarusha sasa sijui kama aliukana uraia wa Somalia au baba yake kabla hajamzaa alishaukana uraia wa Somalia.pia zipo tuhuma kwamba anachangiwa fedha nyingi na raia wa Tanzania wenye asili ya kisomali ambao wamepania kuhakikisha wasomali wengi zaidi wanatinga mjengoni tayari A kinana ambae ni msomali mwenzake ameshachukua jukumu la kuzindua kampeni zake siku ya Jumamosi uwanja wa NMC.

[3] Sijui kama ni kweli Mama Batilda aliwahi kuolewa mara tatu na kuachika kama ni kweli nadhani atakuwa na kibarua kikubwa sana kuwashawishi wapiga kura.
 
Pamoja na mwanzo kujitahidi kujifanya objective lakini at this point nooo. Yaani unataka kuniaminisha kuwa maneno hayo ndiyo sera wanazotaka wananchi kutoka kwa wabunge wao. Ukweli haya ni maneno mazito saana. Hata km huyu bwana akishinda uchaguzi ajue wazi kuwa amekalia kuti kavu. Haya si maneno yanayofaa kutolewa na mgombea. Hizo ndio siasa za kuchafuana na kuchafuana huwa si hivyo, bora hata angetumia watu wengine. Sasa umuhimu wa shule unaonekana. Hili ni tatizo kwakweli.
 
Heshima kwako Anfaal,

kwanza lazima uelewe kitu kimoja muhimu kwamba nimejaribu kudodosa kutoka vyanzo vingi vya hii habari na kuileta hapa jamvini.Unapaswa kufahamu kwamba kama ni kweli Mama Batilda aliwahi kuolewa mara tatu na kuachika kwa maoni yangu si matusi bali ukweli kuhusu historia ya mtu kuhusiana na maisha yake ya nyuma.Mama Batilda si mtu wa kwanza kujadiliwa maisha yake binafsi hata mgombea urais wa CHADEMA wanahabari wandodosa maisha yake na amejaribu kuyatolea ufafanuzi wa kutosha.

Kama Mama Batilda ni msomali pia sioni kosa wapo raia wengi wenye asili ya somalia tena wenye nyazifa nzito ndani ya serekali na chama tatizo litakuwa pale atakapokosana na wakubwa serekali kama ilivyotokea kwa kijana Bashe.
 
Kuolewa na kuachika kuna impact gani katika maisha ya mtu? What if she decided to walk away yeye mwenyewe? Kwani ukiolewa ukaachika inamaanisha nini? Hii ni mentality ya kizamani saana. Inamaana mtu akae kwenye ndoa anapata mateso kisa watu watasema ameachika??? Hiyo ya Kisomali ina implication gani wakati wa kampeni? Nadhani huyu bwana anasahau kwamba vyama vyote vya siasa vimetia sahihi makubaliano ya maadili. Na pia hicho ndicho atakachowafanyia watu wa Arusha. Umuhim wa elimu kwakweli umeonekana sasa. Kumjadili mtu haikatazwi hasa km maisha yake yanaathiri maendeleo ya nchi vinginevyo ni kupoteza muda. Km anadhani huyo mama ni msomali aende akaappeal immigration maana otherwise ni ubaguzi usio na haja wala tija.
 
Mkuu wangu kuolewa na kuachika mara tatu kwa mgombea ubunge ambae kama akishinda atakuwa mwakilishi wa watu zaidi ya milioni moja nadhani si jambo dogo.Mtu aliyeshindwa kuongoza familia yake kwa wanaume watatu hata kama utadai alikuwa akikimbia mateso akili yangu inakataa kukubali afadhali ingekuwa mmoja ningekuelewa kidogo.

Ndugu Anfaal nchi za wenzetu waliotangulia kuyaona maendeleo kiongozi mzuri ni yule aliyeweza kuitunza na kuiongoza familia yake kwanza,mtu huwezi kupewa uongozi ikiwa umeshindwa kuiongoza famila yako.Sisi waafrika tunajaribu sana kuignore na pengine ndiyo maana tunaishia kuchagua wezi,mafisadi,walarushwa kwasababu hatutaki kumwangalia mtu anayetaka kutuongoza chimbuko lake.
 
Hili halina ukweli hata kidogo. Kwanza mfumo wetu wa maisha na ule wa kimagharibi ni tofauti kidogo. Mtu akiwa na mkewe/mumewe anakumbana na mengi kuanzia presha za extended family, kucheat nk. Lakini pia nikutolee mfano mdogo tu wa watu waliowahi kudivorce kutoka huko unakokuita kwenye maendeleo. Kuna Reagan (USA) na Sarkozy (France) achana na yule muhun wa Italy.
 
Back
Top Bottom