Kampeni kabla ya NEC kutangaza uchaguzi ni uchuro na kuwakosea wananchi

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,538
17,467
Nawaandikia wanachama wenzangu wa ccm popote pale mlipo!

Kuna ka tabia kame zuka ka hovyo sana ka kuwapigia kampeni viongozi waliopo kabla ya muda wa uchaguzi wakati bado hawajatimiza KAZI waliotumwa na chama kupitia ilani yetu,Tabia hii huwatoa viongozi kwenye Reli na kuanza kufikiria uchaguzi badala ya KUWATUMIKIA wananchi!

Zipo kauli za makada zinasikika eti FULANI hadi 2030 SASA unajiuliza huyu anaepigiwa kampeni ameshatimiza malengo ya chama HADI 2025,yaani ilani ya chama ya 2020-2025 imetekelezwa!!?

Halafu kwa nini tusiheshimu nyakati tulizonazo,yaani tuheshim BADO yupo 2023 na 2025 ni kunako majaaliwa ya mwenyeezimungu!!

Tabia hii imefanya viongozi waliopo kujikwaa KWA KUFANYA kampeni badala ya KUWATUMIKIA wananchi na kutimiza ilani ya chama,KILA kiongozi ameingia kwenye mtego wa kampeni bila kujua hapo 2025 nini kitajiri!

Baadhi wameshaanza hata kuandaa fedha za uchaguzi ujao KWA kuendekeza upigaji na ubadhirifu na hali hii ita kigharimu chama chetu kwasababu kelele zimwshaanza kupingwa pande zote!

Turudi kwenye misingi ya kuheshim nyakati na malengo ya chama na sio malengo ya mtu binafsi!!tabia hii haiwajengi viongozi wetu bali inasababisha kujikwaa kwao kama SASA ilivyo na itasababisha viongozi wetu kuanguka kiroho,KISIASA hata kimwili kabla ya uchaguzi kufika!!

Nikimtizama kwa makini huyo anaepigiwa chapuo hadi 2030 anaonekana kachoka tayari kabla hata ya 2025 kufika yaani chawa wanamnyonya damu na kumkausha kabla hata ya mapambano!ndio maana teuzi zinamchanganya na kapoteza identity ya utawala wake unasimamiwa nini HASA!!

Makada na chawa wanamuumiza sana mpigiwa chapuo kabla ya wakati na inawezekana akafika akiwa amechoka sana coz mwili hauwezi endelea kupiga vita ambavyo havipo yaani unapoga kampeni ya uchaguzi bila kujua mpinzani wako ndani na nje ya CHAMA chako ni nani!hii ni sawa na kupiga upepo ngumi!!!

Mungu ibariki Tanzania nchi yetu niipendayo sana

Mungu wape akili makada wa chama changu ccm wasiwe machawa wanaomnyonya damu mpigiwa chapuo kabla ya wakati!!!
 
Nawaandikia wanachama wenzangu wa ccm popote pale mlipo!

Kuna ka tabia kame zuka ka hovyo sana ka kuwapigia kampeni viongozi waliopo kabla ya muda wa uchaguzi wakati bado hawajatimiza KAZI waliotumwa na chama kupitia ilani yetu,Tabia hii huwatoa viongozi kwenye Reli na kuanza kufikiria uchaguzi badala ya KUWATUMIKIA wananchi!

Zipo kauli za makada zinasikika eti FULANI hadi 2030 SASA unajiuliza huyu anaepigiwa kampeni ameshatimiza malengo ya chama HADI 2025,yaani ilani ya chama ya 2020-2025 imetekelezwa!!?

Halafu kwa nini tusiheshimu nyakati tulizonazo,yaani tuheshim BADO yupo 2023 na 2025 ni kunako majaaliwa ya mwenyeezimungu!!

Tabia hii imefanya viongozi waliopo kujikwaa KWA KUFANYA kampeni badala ya KUWATUMIKIA wananchi na kutimiza ilani ya chama,KILA kiongozi ameingia kwenye mtego wa kampeni bila kujua hapo 2025 nini kitajiri!

Baadhi wameshaanza hata kuandaa fedha za uchaguzi ujao KWA kuendekeza upigaji na ubadhirifu na hali hii ita kigharimu chama chetu kwasababu kelele zimwshaanza kupingwa pande zote!

Turudi kwenye misingi ya kuheshim nyakati na malengo ya chama na sio malengo ya mtu binafsi!!tabia hii haiwajengi viongozi wetu bali inasababisha kujikwaa kwao kama SASA ilivyo na itasababisha viongozi wetu kuanguka kiroho,KISIASA hata kimwili kabla ya uchaguzi kufika!!

Nikimtizama KWA makini huyo anaepigiwa chapuo hadi 2030 anaonekana kachoka tayari kabla hata ya 2025 kufika yaani chawa wanamnyonya damu na kumkausha kabla hata ya mapambano!ndio maana teuzi zinamchanganya na kapoteza identity ya utawala wake unasimamiwa nini HASA!!

Makada na chawa wanamuumiza sana mpigiwa chapuo kabla ya wakati na inawezekana akafika akiwa amechoka sana coz mwili hauwezi endelea kupiga vita ambavyo havipo yaani unapoga kampeni ya uchaguzi bila kujua mpinzani wako ndani na nje ya CHAMA chako ni nani!hii ni sawa na kupiga upepo ngumi!!!

Mungu ibariki Tanzania nchi yetu niipendayo sana

Mungu wape akili makada wa chama changu ccm wasiwe machawa wanaomnyonya damu mpigiwa chapuo kabla ya wakati!!!
Unaowashauri wameziba masikio, sijui itakuwaje!!
 
Back
Top Bottom