figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,662
- 59,099
Kamishna wa Intelijensia ya Jinai kutoka Makao Makuu ya Polisi CP Charles Mkumbo, wakati akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha 20 cha maafisa habari wa Serikali kilichofanyika Zanzibar Aprili 3 - 6, 2025 alisema Jeshi la Polisi limejiandaa kwaajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2025
Mkumbo alisema kwamba Mkuu wa Jeshi la Polisi ameshawaelekeza Nchi nzima watu kujiandaa kwa Uchaguzi. Kwahiyo sasa hivi wapo Timamu hata kama uchaguzi ungekuwa keshokutwa.
Amesema Polisi wana vifaa vya kutosha kutimiza majukumu kabla wakati na baada ya Uchaguzi.
Kahimiza watu kuwa Wazalendo kwa kuipenda Tanzania.
"Sisi ni watoto wa Tanzania hii, iwapo machafuko yakijitokeza tutakimbilia wapi? Hatuna Tanzania A wala N, tuna Tanzania moja tu. Tuhamasishe Uzalendo, Amani Utulivu na Usalama katika kipindi chote cha Uchaguzi". Amesema CP Charles Mkumbo.