Kamishna Chagonja aruhusu polisi washughulikiwe

Jun 14, 2011
58
18
Friday, 26 August 2011
Na Waitara Meng'anyi, Tarime

KAMISHNA wa Operesheni za Jeshi la Polisi Nchini, Paul Chagonja, amewaruhusu wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka Mgodi wa North Mara, kuwapiga kama wezi, askari wakorofi wanaowavamia na kuwanyanyasa kinyume na taratibu za jeshi hilo.

Ruhusa hiyo ilikuja kufutia tukio la Jumanne wiki hii, la askari walioendesha operesheni ya kamata watu na kulipua mabomu ya machozi, kwa maelezo kuwa walikuwa wanadhibiti walioingia mgodini kinyume cha taratibu.

"Nasema, ikiwa askari atakuja kukukamata wakati akiwa hana namba Inayoambatana na jina lake, apewe kipigo hadharani na msimhurumie. Huyo si mwenzetu," alisema Chagonja wakati akizungumza na wakazi wanaozunguka mgodi huo jana.
 
Kimsingi hakupaswa kutoa kauli hiyo kwani huu ni ukiukwaji wa good governance. Kwa kauli hii ni mauti kwa polisi hususani kwa kipindi hiki ambapo hakuna mahusiano mazuri kati ya wachimbaji wadogo na polisi huko Mgodini. Alipasa kuagiza wao kuwakamata na kuripotia polisi na si kupiga hatimaye kifo.
 
Naona sijaelewa, hivi anamaanisha washughulikiwe kama vibaka Kariakoo? Yaani wavalishwe na tairi la gari kisha wachomwe moto? Ndo kusema ameruhusu mob justice? Naomba aliyeelewa anifahamishe.
 
Msije tu kusema ohh watu wa Tarime wakorofi mara wameua polisi!!! nyie wenyewe mmetoa rungu na mawe na nyumba yenyewe ya vioo...
 
Siamini kama anachosema ndio anamaanisha,ktk zama hz za polisi jamii kamishna wa operesheni
kutoa kauli kama hiyo ni kutokuwa na weledi na kwenda kinyume na philosophy ya bosi wake!
 
Mh!hapa kamishna amechemka mbayaa....so anatupasha kuwa kupiga mpaka kuua mtuhumiwa sio kosa kisheria?
 
Huyo kamanda si ndie alikuakilalamika wapinzani wana haribu amani yetu? Mbona wapinzani walikuwa wanatoa elimu kwa wananchi kujua haki zao. Sasa yeye mbona anavunja sheria moja kwa moja? Au Tarime wakishatekeleza maelezo yake ndio atakataa ili tume iundwe kuchunguza kauli yake?
 
Jaman huyu anawafahamu wakulya ama anawaskia tu. Ametangaza vita ya polis na raia. Kweli nchi haina kiongozi. Kila mwenye nafasi ya kusema anajipa majukumu. Luhanjo sasa Chagonja
 
Alikuwa anatafuta sifa kwa Wananchi. Nchi imekwsha, hatutafika salama.
 
Alikuwa anatafuta sifa kwa Wananchi. Nchi imekwsha, hatutafika salama.

Kweli kabisa huyu chagonja atakuwa anatafuta umaarufu wa bei nafuu kwa wananchi wa nyamongo. Anafahamu kabisa ni kwa kiasi gani polisi wanaolinda mgodi wamekuwa wakiua raia wasio na hatia kwa visingizio mbalimbali. Na anafahamu kwamba hakuna mahusiano mazuri kati ya polisi na wananchi halafu yeye anawaambia wananchi wawashughulikie polisi wasio na namba wala majina.

Hapa ninachokiona, chagonja anataka raia wengi zaidi wafe, kwani anachofanya ni kuchochea ugomvi uliopo kati ya polisi na wananchi. anawawekea mtego wananchi, pindi watakapomshughulikia askari polisi basi wapate nafasi ya kupora mali za watu na kujitajirisha.
 
Chagonja usije kuikana kauli yako,,,,,sisi wengine bwana tuna hasira sana na hao vibaraka wenzako
 
Kimsingi hakupaswa kutoa kauli hiyo kwani huu ni ukiukwaji wa good governance. Kwa kauli hii ni mauti kwa polisi hususani kwa kipindi hiki ambapo hakuna mahusiano mazuri kati ya wachimbaji wadogo na polisi huko Mgodini. Alipasa kuagiza wao kuwakamata na kuripotia polisi na si kupiga hatimaye kifo.

hii ndio itawatia akili wanapokwenda kuonea wananchi na kuwapola wewe unaona sawa
 
Kimsingi hayupo sahihi, anachotaka ni kuleta vurugu ambayo inaigharimu polisi kuirejesha tena.
 
Naona sijaelewa, hivi anamaanisha washughulikiwe kama vibaka Kariakoo? Yaani wavalishwe na tairi la gari kisha wachomwe moto? Ndo kusema ameruhusu mob justice? Naomba aliyeelewa anifahamishe.

Ndo maana yake,Polisi na vibaka wote ni dugu moja wachomwe moto tu.
 
Ni kweli hayuko sahihi lakini kwa nini polisi aende kukamata watu namba kaacha nyumbani na hana kitambulisho? Anaogopa nini? Kifupi amesema: muwafanye kama mnavyoyafanya majambazi mengine.
Hata hivyo si sahihi!
 
Kimsingi hayupo sahihi, anachotaka ni kuleta vurugu ambayo inaigharimu polisi kuirejesha tena.

Kama Polisi mwenye uniform na akakosa namba amesema tumuue, naomba atufafanulie wale CID ambao hawana hata yuniform. tukiwaua si tuwazike moja kwa moja?
 
Kimsingi hakupaswa kutoa kauli hiyo kwani huu ni ukiukwaji wa good governance. Kwa kauli hii ni mauti kwa polisi hususani kwa kipindi hiki ambapo hakuna mahusiano mazuri kati ya wachimbaji wadogo na polisi huko Mgodini. Alipasa kuagiza wao kuwakamata na kuripotia polisi na si kupiga hatimaye kifo.
Kwani wao wameua raia wangapi?si ni wengi tu dawa ya moto ni moto.
 
Back
Top Bottom