RC Kagera aomba mkoa kuwa Kanda Maalumu ya Polisi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,830
21,460
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amemuomba Kamishna wa Polisi wa Oparasheni na Mafunzo nchini, Awadh Juma kufikisha ombi la Kagera kuwa kanda maalumu kutokana na mauaji yanayotokea kila siku wastani wa mtu mmoja na kwa mwezi watu 28 hadi 30.

Chalamila ametoa ombi hilo Mei 12, 2023 wakati Kampuni ya Tembo Nickel inayochimba madini ya Nickel Wilaya ya Ngara mkoani Kagera ilipokuwa ikisainiana mkataba wa makubaliano ya ulinzi na usalama kwa jamii na Jeshi la Polisi Tanzania mkataba uliofanyika Shule ya Msingi Bugarama wilayani Ngara.

Chalamila licha ya kuomba Kagera kuwa kanda maalumu pia ameomba kata ya Bugarama kuwa Wilaya ya Kipolisi kutokana na kata hiyo kujengwa kituo cha polisi chenye hadhi ya kituo cha mkoa na kuwa kutokana na kata hiyo kuwa mpakani yamekuwa yakijitokeza matukio mbalimbali ya uharifu.

“Niombe maombi machache kwako Kamishna wa Polisi utupelekee, najua kwa dhamana yangu ninao uwezo wa kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani lakini kabla sijazungumza naye na hii wewe uondoke nayo kwamba hapa kitajengwa kituo cha polisi chenye hadhi ya mkoa ambao atapaswa kukaa mtu mzito kidogo. Sasa niombe kwamba labda anzeni kuangalia mtu atakayekaa hapa naye aitwe mkuu wa polisi wilaya (OCD) maana yake oneni kama mnaweza kufanya wilaya maalumu ya kipolisi,” amesema.

Chalamila amekazia ombi lililotolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Wiliam Mwampagahle la kuongeza askari zaidi ya 100 katika kituo cha polisi kitakachojengwa Bugarama kutokana na kwamba askari hao watalinda maeneo ya mgodi masaa 24 pia watatakiwa kuwekwa maaskari katika mradi wa umeme Rusumo unaozihusisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi na katika benki za CRDB na NMB zinazojengwa Rulenge.

Chalamila amesisitiza ombi lililotolewa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Kagera, Wiliam Mwampagahle, la kuongeza idadi ya askari zaidi ya 100 katika kituo cha polisi kitakachojengwa Bugarama. Hii ni kwa sababu askari hao watalinda maeneo ya mgodi masaa 24 na pia watatakiwa kuwekwa katika mradi wa umeme wa Rusumo unaohusisha Tanzania, Rwanda, na Burundi, pamoja na benki za CRDB na NMB zinazojengwa Rulenge.

Kwa upande wake, Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo, Awadh Juma, ameeleza kuwa amepokea maombi ya mkuu wa mkoa kwa niaba ya Jeshi la Polisi na atayawasilisha kwa mkuu wa jeshi hilo nchini (IGP). Amesema kuwa ombi la kuanzishwa kwa wilaya ya kipolisi na kuwepo kwa idadi kubwa ya askari ni mambo yanayowezekana. Wanaweza kuyafanyia kazi haraka ili kuhakikisha usalama wa eneo hilo unakuwepo, hasa ikizingatiwa kwamba wamepata uhakika wa ujenzi wa kituo kikubwa cha polisi chenye hadhi kubwa, usafiri, na mambo mengine.

Kwa upande wake, Meneja wa Mgodi wa Tembo Nickel, Manny Ramos, ameelezea mambo ambayo wamekubaliana katika mkataba, ikiwa ni pamoja na kuboresha kituo cha polisi cha Bugarama hadi kiwango cha daraja A, kuongeza kituo kidogo cha polisi katika Kijiji cha Muganza, na kujenga nyumba za askari watakaofanya kazi katika jamii ya Tarafa ya Rulenge. Pia, wamekubaliana kutoa gari kwa jeshi hilo katika kituo kitakachojengwa, ambalo thamani yake ni zaidi ya shilingi bilioni moja. Mkataba huo utakuwa wa miaka mitatu.

kagera-pic.jpg
 
Mikoa ambayo inatakiwa iwe kanda maalum ya kipolisi ni Kagera, Geita, Songwe na Mara.

Mauaji ya raia mikoa hii ni makubwa na mengi sana

Mkoa wa Dar uondolewe kwenye kundi la Kanda Maalum.
 
Mikoa ambayo inatakiwa iwe kanda maalum ya kipolisi ni Kagera, Geita, Songwe na Mara.

Mauaji ya raia mikoa hii ni makubwa na mengi sana

Mkoa wa Dar uondolewe kwenye kundi la Kanda Maalum.
Huwezi iondoa Dar kwenye kanda maalum. Geita, Mara na Shinyanga pia ziwe kanda maalum. Kagera haina haja unless kuwe na machafuko Burundi na Rwanda
 
Back
Top Bottom