Kamera, Kimera, Kamari na Kukamula!

Kamera.... tangu soga ya ushirikina izuke Bungeni kuna habari za kutatanisha kuhusu matumizi ya kamera za Bunge. Kwanza taarifa zilisema Kamera zilikuwa wazi na zilimnasa bwana chenge akifanya alichokuwa anafanya. Tukaambiwa siyo tu kamera za usalama bali pia za mojawapo ya TV binafsi zinazorusha matangazo. Vyanzo vyangu vya uhakika vinasema TV hiyo binafsi kweli ilimnyaka bwana huyo na hilo usalama na bunge wanajua (halina utata). Baadaye zikaja habari kuwa hakuna Kamera iliyonasa hilo na hivyo hakuna clip ya tukio..Hata hivyo habari hizi zilizimwa mara ilipohakikishwa kuwa kweli jamaa alinaswa. Hata hivyo mwishoni hapa ikasemekana ni kamera moja tu iliyomnasa wakati zile za usalama za Bunge hazikumnasa (au ni moja iliyonasa).

Hoja ya Kamera ya Bunge kuzimwa haiingii akilini. Ukumbi wa Bunge unatakiwa kuwa na usalama kwa masaa 24. Watu wanapoingia kusafisha n.k lazima wote waonekane in camera, itakuwajee kama msafishaji alikuwa ametumiwa kupandikiza kitu? Hivyo wote wanaoingia kwenye chumba cha Bunge wanarekodiwa (wanapaswa kurekodiwa) masaa 24. Kama ni kweli kuwa Usalama wa Bunge wanazima kamera zao baada ya kikao tu na kuna muda ambao ukumbi wa Bunge haonekani "in camera" hilo ni jambo la hatari kuliko ambayo nimewahi kuyasikia na inatishia kabisa usalama wa Bunge lenyewe na wabunge wetu.

Hili linahitaji ufafanuzi, je Kamera za usalama wa Bunge zinazimwa wakati wowote ule na kwanini (kama zinazimwa)? Kama hazizimwi ni kwanini tumeambiwa kuwa kamera zilikuwa zimezimwa? Kama ilikuwa ni jitihada za kupotosha umma ni nani aliyetoa habari hizo (kuna mtu ambaye anajulikana kuwa chanzo cha upotoshaji huu na utawala wa Bunge ungemtimua kazi mara uongo huu utakapogundulikwa kwani alikuwa anajaribu kuficha uovu ambao unaweza kugharimu maisha ya viongoi wetu). Kamera zilikuwa zinawaka au zimezimwa?


Kimera..a.k.a chimera Kule kusini kuna sumu kali sana inayotumiwa na watu mbalimbali. Sumu hii hujulikana sana kama kimera na tunasimuliwa kuwa ni very potent na kiasi kidogo tu kinaweza kumdhuru mtu ndani ya muda si mrefu. Sumu hii ambayo nadhani kwa kiingereza ni arsenic inaendana pia na sumu nyingine ya kimeta (anthrax) angalia majina yanavyofanana. Enzi za mababu sumu hii ilikuwa inawekwa kwenye ulanzi, togwa n.k kwa kutumia ukucha tu ambapo mtu anaweza kuigandisha na kwa "bahati mbaya" kutumbukiza ukucha kwenye kombe la ulabu. Sumu hizi mbili zimekuwa zikitumika katika jamii mbalimbali tangu enzi za warumi na wagiriki.

Hata hivyo, chochote kilichokuwa kinafanyika Dodoma yawezekana siyo "Kimera" tunachokifahamu sisi bali kimera cha ushirikina tu. Lakini kwa mwanamazingaombwe kama mimi naamini kabisa kuwa siri ya mazingaombwe ni distraction yaani "kuzuga". Wakati unafanya hiki na watu wanakiona na kuamini lakini ukweli ni kuwa unafanya "kile" ambacho hawakioni na kukiamini. Ndio maana tangu mwanzo nimejaribu kukwepesha kabisa suala la ushirikina kwa sababu kilichotokea chawezekana siyo ushirikina na siyo kimera cha kiafrika bali distraction of what actually is happening. Itakuwaje kama Bw. Chenge ambaye hata kabla ya hapa amekuwa akitajwa kuwa ni "ntuzu" na baadhi ya watu na kuamrisha hofu ndani yao alikuwa hana lolote isipokuwa kupiga mahesabu kuwa watu wakiona anchofanya wataamini "ushirikina"?

Miaka michache iliyopita nilikuwa kwenye msiba wa babu yangu ambaye alifariki kifo cha ghafla. Imani za kichawi zilishiriki sana na aliyedaiwa kuwani "mchawi" ni mtoto mdogo wa miaka kama 10 hivi ambaye inadaiwa alirithishwa "mkoba". Kwa vile nilikuwa kijijini nilipoondoka niliambiwa niongozane na kijana huyo kunionesha njia hadi kijiji cha jirani ambako ndiko barabara kuu ipo. Hata hivyo nilionywa kuwa kamwe nisimuache awe nyuma yangu! You can only guess what happened along a wooded stretch of about 10 mile on a sunny and dry day! However by the end of the trip bwana mdogo alikuwa rafiki "yangu".... alinipa tukinga kinga (sijui kama tunafanya kazi au ilibidi nikubali tu yaishe"!

Yawezekana madai ya ushirikina ni uzugaji wa kitu halisi!


Kamari... Hata hivyo maelezo yanayoendelea sasa kutoka kwa viongozi mbalimbali ni sawa na kucheza kamari wakijaribu kuona ni kipi wananchi watakikubali na kukiamini? Kwamba halikutokea, kwamba limetiwa chumvi, kwamba ilikuwa ni "kutafuta kiti" kwamba alipoteza "vijisenti" vyakee akawa anatafuta n.k Ni Kamari kwa sababu wanatarajia kuwa maelezo yao yatafunga mjadala na kufanya jambo hili liwe la kupuuzwa.

Naamini when everything is said and done maelezo yatakayokuja ni ya kupuuzia na big misunderstanding. Chenge atasafishwa na mjadala utaziimwa kwa kutumia hekima za "supika". Mbadala mwingine ni pale Bw. Chenge atakapoweza kuona amefanya mambo ambayo ni kinyume na maadili ya chama au kukifedhehesha chama (kwa mujibu wa Katiba ya CCM). Katika mazingira hayo CCM inauchaguzi wa kumpa onyo, au karipio kali. Lakini kama kitakachothibitika ni kitendo cha uhalifu (kumbuka vitendo vya kichawi vinashtakika mahakamani) basi CCM itakuwa haina ujanja isipokuwa kuonesha kutokukubali kwake kulea, kuzoea, na kulinda vitendo vya kishirikina. Watafanyaje hilo sina uhakika, kumvua uanachama si rahisi. Hata hivyo option nyingine ni kama ataonekana kuvunja kanuni yoyote ya Bunge basi anaweza kujikuta akichukuliwa hatua za kinidhamu.

kukamula...Katika yote haya, ukweli ni kuwa hadi tumefikia mambo ya kuzungumzia ushirikina badala ya bajeti maana yake tuna matatizo... yawezekana tumeshalogwa, au tuko mbioni kulogwa! Na Taifa zima linapologwa basi huyo mchawi ana nguvu kweli! Lakini wakituloga na tusipologeka uchawi huo unamrudia nani au unapotolewa tu hewani! Je yawezekana uchawi hauko kwenye kamera, kimera au kamari bali uko kwenye kukamula! Mwenye kukamula (kushika) ndiye mwenye kujua nani ana kimera mbele ya kamera anayejaribu kucheza kamari!

Tanzania na watanzania wote tulishalogwa muda mrefu uliopita na sasa tumekuwa mazezeta. Upuuzi wote unaotokea ndani ya nchi watu tuko kimya na kuendelea kupiga domo kila siku. Hakuna cha maandamano ya kupinga na kukataa uchafu huo. China, korea na Urusi wanafanya maandamano ya kupinga upuuzi na uchafu unapotokea nchini kwao. Sisi watanzania mlogo umetupata kisawasawa, hatuoni wala kusikia. Kila kitu hewara ama rukhusa.
 
Hivi kweli hapa JF watu wamesahau SPIN za SISIEMU na Serikali yake. Spika ni yuleyule SISIEMU ambayo ni The Mother of All The Spin Mothers. Yaani sometimes hawa viongozi wawe wanafikiria kwanza kabla ya kuanza kuuadaa UMMA. Eti alikuwa anatafuta seat, Shut the hole. Kama alikuwa anatafuta seat, sasa alikuwa anataka mpaka seat ya SPIKA. Jamani sasa kutakuwa na Spika wangapi kwa mujibu wa sheria? Mie siamini kama Chenge yuko kwenye flow hata ya Kukaimu USPIKA kama Mama Makinda hayupo. Haya mambo Spika angekwenda kuwasimulia watoto wake walio chekechea kama anao na si watanzania wenye akili TIMAMU, ndiyo nimesema WATANZANIA wenye AKILI TIMAMU.
 
Heshima mbele wakuu,hili suala la ushirikina bungeni Spika Sitta amenukuliwa na vyombo vya habari vya hapa nyumbani akisema mkanda unao muonyesha mbunge huyo akinyunyiza unga kwenye viti vya wabunge upo na umepelekwa polisi kwa uchunguzi,kama kawaida yao ccm watu wa kulindana

Wah. Anna Abdallah and Lekule wamesema walikuwepo na hawakuona huo "uchawi" unozungumziwa - Source, Nipashe/Alasiri
 
Some thing must be fishing in our House az SS with others Mps, kuna vita vita kubwa sana ndani ya bunge inayoendelea bunge litatulia siku utakapo sikia SS kapigiwa kura ya kutokuwa na imani na wabunge az the revenge !kitu mbacho kwa sasa ndiokinachopikwa
 
Back
Top Bottom