Kamera, Kimera, Kamari na Kukamula! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamera, Kimera, Kamari na Kukamula!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 16, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kamera.... tangu soga ya ushirikina izuke Bungeni kuna habari za kutatanisha kuhusu matumizi ya kamera za Bunge. Kwanza taarifa zilisema Kamera zilikuwa wazi na zilimnasa bwana chenge akifanya alichokuwa anafanya. Tukaambiwa siyo tu kamera za usalama bali pia za mojawapo ya TV binafsi zinazorusha matangazo. Vyanzo vyangu vya uhakika vinasema TV hiyo binafsi kweli ilimnyaka bwana huyo na hilo usalama na bunge wanajua (halina utata). Baadaye zikaja habari kuwa hakuna Kamera iliyonasa hilo na hivyo hakuna clip ya tukio..Hata hivyo habari hizi zilizimwa mara ilipohakikishwa kuwa kweli jamaa alinaswa. Hata hivyo mwishoni hapa ikasemekana ni kamera moja tu iliyomnasa wakati zile za usalama za Bunge hazikumnasa (au ni moja iliyonasa).

  Hoja ya Kamera ya Bunge kuzimwa haiingii akilini. Ukumbi wa Bunge unatakiwa kuwa na usalama kwa masaa 24. Watu wanapoingia kusafisha n.k lazima wote waonekane in camera, itakuwajee kama msafishaji alikuwa ametumiwa kupandikiza kitu? Hivyo wote wanaoingia kwenye chumba cha Bunge wanarekodiwa (wanapaswa kurekodiwa) masaa 24. Kama ni kweli kuwa Usalama wa Bunge wanazima kamera zao baada ya kikao tu na kuna muda ambao ukumbi wa Bunge haonekani "in camera" hilo ni jambo la hatari kuliko ambayo nimewahi kuyasikia na inatishia kabisa usalama wa Bunge lenyewe na wabunge wetu.

  Hili linahitaji ufafanuzi, je Kamera za usalama wa Bunge zinazimwa wakati wowote ule na kwanini (kama zinazimwa)? Kama hazizimwi ni kwanini tumeambiwa kuwa kamera zilikuwa zimezimwa? Kama ilikuwa ni jitihada za kupotosha umma ni nani aliyetoa habari hizo (kuna mtu ambaye anajulikana kuwa chanzo cha upotoshaji huu na utawala wa Bunge ungemtimua kazi mara uongo huu utakapogundulikwa kwani alikuwa anajaribu kuficha uovu ambao unaweza kugharimu maisha ya viongoi wetu). Kamera zilikuwa zinawaka au zimezimwa?


  Kimera..a.k.a chimera Kule kusini kuna sumu kali sana inayotumiwa na watu mbalimbali. Sumu hii hujulikana sana kama kimera na tunasimuliwa kuwa ni very potent na kiasi kidogo tu kinaweza kumdhuru mtu ndani ya muda si mrefu. Sumu hii ambayo nadhani kwa kiingereza ni arsenic inaendana pia na sumu nyingine ya kimeta (anthrax) angalia majina yanavyofanana. Enzi za mababu sumu hii ilikuwa inawekwa kwenye ulanzi, togwa n.k kwa kutumia ukucha tu ambapo mtu anaweza kuigandisha na kwa "bahati mbaya" kutumbukiza ukucha kwenye kombe la ulabu. Sumu hizi mbili zimekuwa zikitumika katika jamii mbalimbali tangu enzi za warumi na wagiriki.

  Hata hivyo, chochote kilichokuwa kinafanyika Dodoma yawezekana siyo "Kimera" tunachokifahamu sisi bali kimera cha ushirikina tu. Lakini kwa mwanamazingaombwe kama mimi naamini kabisa kuwa siri ya mazingaombwe ni distraction yaani "kuzuga". Wakati unafanya hiki na watu wanakiona na kuamini lakini ukweli ni kuwa unafanya "kile" ambacho hawakioni na kukiamini. Ndio maana tangu mwanzo nimejaribu kukwepesha kabisa suala la ushirikina kwa sababu kilichotokea chawezekana siyo ushirikina na siyo kimera cha kiafrika bali distraction of what actually is happening. Itakuwaje kama Bw. Chenge ambaye hata kabla ya hapa amekuwa akitajwa kuwa ni "ntuzu" na baadhi ya watu na kuamrisha hofu ndani yao alikuwa hana lolote isipokuwa kupiga mahesabu kuwa watu wakiona anchofanya wataamini "ushirikina"?

  Miaka michache iliyopita nilikuwa kwenye msiba wa babu yangu ambaye alifariki kifo cha ghafla. Imani za kichawi zilishiriki sana na aliyedaiwa kuwani "mchawi" ni mtoto mdogo wa miaka kama 10 hivi ambaye inadaiwa alirithishwa "mkoba". Kwa vile nilikuwa kijijini nilipoondoka niliambiwa niongozane na kijana huyo kunionesha njia hadi kijiji cha jirani ambako ndiko barabara kuu ipo. Hata hivyo nilionywa kuwa kamwe nisimuache awe nyuma yangu! You can only guess what happened along a wooded stretch of about 10 mile on a sunny and dry day! However by the end of the trip bwana mdogo alikuwa rafiki "yangu".... alinipa tukinga kinga (sijui kama tunafanya kazi au ilibidi nikubali tu yaishe"!

  Yawezekana madai ya ushirikina ni uzugaji wa kitu halisi!


  Kamari... Hata hivyo maelezo yanayoendelea sasa kutoka kwa viongozi mbalimbali ni sawa na kucheza kamari wakijaribu kuona ni kipi wananchi watakikubali na kukiamini? Kwamba halikutokea, kwamba limetiwa chumvi, kwamba ilikuwa ni "kutafuta kiti" kwamba alipoteza "vijisenti" vyakee akawa anatafuta n.k Ni Kamari kwa sababu wanatarajia kuwa maelezo yao yatafunga mjadala na kufanya jambo hili liwe la kupuuzwa.

  Naamini when everything is said and done maelezo yatakayokuja ni ya kupuuzia na big misunderstanding. Chenge atasafishwa na mjadala utaziimwa kwa kutumia hekima za "supika". Mbadala mwingine ni pale Bw. Chenge atakapoweza kuona amefanya mambo ambayo ni kinyume na maadili ya chama au kukifedhehesha chama (kwa mujibu wa Katiba ya CCM). Katika mazingira hayo CCM inauchaguzi wa kumpa onyo, au karipio kali. Lakini kama kitakachothibitika ni kitendo cha uhalifu (kumbuka vitendo vya kichawi vinashtakika mahakamani) basi CCM itakuwa haina ujanja isipokuwa kuonesha kutokukubali kwake kulea, kuzoea, na kulinda vitendo vya kishirikina. Watafanyaje hilo sina uhakika, kumvua uanachama si rahisi. Hata hivyo option nyingine ni kama ataonekana kuvunja kanuni yoyote ya Bunge basi anaweza kujikuta akichukuliwa hatua za kinidhamu.

  kukamula...Katika yote haya, ukweli ni kuwa hadi tumefikia mambo ya kuzungumzia ushirikina badala ya bajeti maana yake tuna matatizo... yawezekana tumeshalogwa, au tuko mbioni kulogwa! Na Taifa zima linapologwa basi huyo mchawi ana nguvu kweli! Lakini wakituloga na tusipologeka uchawi huo unamrudia nani au unapotolewa tu hewani! Je yawezekana uchawi hauko kwenye kamera, kimera au kamari bali uko kwenye kukamula! Mwenye kukamula (kushika) ndiye mwenye kujua nani ana kimera mbele ya kamera anayejaribu kucheza kamari!
   
 2. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nilipatwa na wasiwasi mkubwa sana kwenye matumizi ya kamera bungeni. Hata mimi siamini kama kweli kamera zilikuwa zimezimwa au ilikuwa ni sehemu ya kufanikisha dili.
   
 3. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mze umeniacha hoi sikuwa nataka kuandika chochote kwa muda wa six weeks ila nalazimika japo hii post moja
   
 4. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Anthrax= Kimeta and not Kimera MMK kama ulivyoandika. Wabongo wengi wanaenda kwa waganga wa kienyeji lakini hawawezi kusimama mbele za watu na kuongelea mambo haya! Uchawi ndani ya CCM umekuwa ni kitu cha kawaida sasa, tukirudi nyuma toka enzi za Mwalimu na kifimbo chake- ameacha urithi mkubwa kwa wafuasi wake! Hata kipindi cha kampeni za JK, kama unakumbuka kuna siku JK alianguka ghafla Jangwani lakini cha kushangaza ni kwamba hakupelekwa Muhimbili ambako ni hospitali iliyokuwa karibu na eneo la tukio,cha kushangaza tuliambiwa anapelekwa Lugalo- unapita bagamoyo road kwenda huko!!!. John Pombe Magufuli alipopata uwaziri alitaka mawaziri wote waliojirithisha magari ya miradi wayarudishe na kupiga marufuku magari ya mawaziri kuonekana kwenye sehemu za starehe baada ya mida ya kazi, kwa kuwa alikuwa mgeni -alipopigwa kitu akakimbilia hospitali South Africa lakini akashauriwa na wataalamu arudi, baada yakurudi na 'kutengenezwa' leo hii anapeta na anapiga mzigo bila kumuogopa mtu yoyote. Kuna kina Kolimba na Malima ambao wote tunajua yaliyowasibu......I think some of us here have to start getting real!
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mwanakijiji shukran sana!

  sina la kuongeza. 'Spin doctors' wanatumia technic hii ku distract watu kwenye ukweli! Political scientists wa bongo wanajua udhaifu wetu ni imani za ushirikina,

  They can fool some people some time, but they cant fool all the people all the time...

  aaarrrgggh,

  usiku mwema wakuu
   
 6. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2008
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 375
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Heshima mbele wakuu,hili suala la ushirikina bungeni Spika Sitta amenukuliwa na vyombo vya habari vya hapa nyumbani akisema mkanda unao muonyesha mbunge huyo akinyunyiza unga kwenye viti vya wabunge upo na umepelekwa polisi kwa uchunguzi,kama kawaida yao ccm watu wa kulindana
   
 7. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MKJJ,,,awali bwa chenge alipozushiwa kufa ulipigia sim na ukamuweka hewani kwenye klh, vipi itawezekana kwa hili?? Tunaham tumsikie huyo bwana
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji,

  Rejea kauli ya Saidi Mwema kuhusu mafisadi wa EPA, "Taifa limetekwa Nyara"!
   
 9. Mswahilina

  Mswahilina Senior Member

  #9
  Jun 16, 2008
  Joined: Apr 7, 2008
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  He he he he he he ! ! ! ! Waswahili macho na masikio yetu.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jun 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Asante sana... I stand corrected.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jana Chiligati alisema ata NEC wamediscus ilo ila wakasema ati Chenge alikuwa akitafuta seat ya Kukaa baada ya Kupigwa chini.Si unajua alikuwa akikaa mbele.
  Sawa nakubaliana nao sasa issue inakuja je alikuwa anatafuta nafasi ya kukaa ata kwenye kiti cha spika!
   
 12. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  CCM wanadiscuss ishu ya Bunge au walimdiscuss Chenge ambae ni mbunge kupitia chama chao???
  Mwanakijiji,
  Hii nimeikubali they are realy playing smart....distract them bafore they are aware of what is happening and it will be too late for them to know!!! hope it aint workin anymore!
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wandugu Chenge anatafuta mahali pa kukaa baada ya kila mt kutoka alitaka kukaa il afanye nini humo ? Mbona wana majibu ya kijinga hawa watu ?
   
 14. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hayo ni majibu ya kijinga kabisa.
  Wakome kufikiria kwamba kila mTZ ni mjinga. Nasema wakome kabisa kuanzia sasa!!
  Halafu huyu mpuuzi amepewa dhamana ya kuongeza wizara nyeti.
  Tunuzidi kuelewa aina ya viongozi msanii aliyotuwekea.
  Amenitia hasira asilani.
   
 15. M

  Mama JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  hiyo kama ni kamari kweli basi imechezwa kiccm (strategic), wameweza kwa kudivert attention. All in all everything is possible under the sun, yawezekana tumeshalogwa! Na je tunajijua kama tumeshalogwa? inawezekana mchawi mmoja akaloga Taifa zima? sijui.
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hapa wakuu naona Chiligati anajitahidi sana kupoza mambo lakini ukweli utabaki kuwa ukweli siku zote hapa sasa wanacho fanya ni kutuzuga tu tuamini kuwa issue si kweli kama ilivyo reportiwa..
  Lakini ukweli utabainika tu.
   
 17. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kwa ufahamu wangu mdogo juu ya hizi cctv, kwanza kuna chumba maalumu(control room)hapa kunakuwa na screen moja au zaidi kwa ajili ya kuangalia matukio yote yanayoendelea ktk eneo husika.pia panakuwepo na recording machine,hii kazi yake ni kurecord matukio yote kutoka kwenye kamera zote (za eneo la bunge)kwa wakati wote bila matatizo.kutokana na jengo la bunge kujengwa hivi karibuni ni lazima wao watakuwa na latest kamera ambazo huwa zinaonesha picha kwenye screen pindi tu mtu au kitu kinapopita sehemu iliyokuwa tulivu.
  Kitendo cha kusema kuwa kamera zilizimwa waadanganye bibi na babu zetu huko huko vijijini,huo ni uongo tena wa mchana kweupe.cctv zote lazima zinarecord muda (saa ) wakati wote.hivyo wakati wa kufuatilia tukio ni rahisi kwa sababu unaangalia ilikuwa kati ya saa ngapi ana kamera namba ngapi ipo eneo hilo.
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chenge inaonyesha alikosea stepu alizopewa na mganga ,pengine alihitajiwa avue nguo zote asionekane hapo ndipo alipopaona pagumu na ndipo mambo yalipokwenda kwenye kamera.
  stepu tu hizo ndizo zilizomzamisha lakini angefanikiwa akaingia na katoka na hakuna kamera ambayo ingesense wakati akiingia hapo .
   
 19. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2008
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kama kuna wakati taifa limesimamishwa na viongozi wetu ni huu. ukiangalia wakati Mkulo anawasilisha bajeti yetu utaona kwamba alikuwa anatimiza wajibu tuu lakini alikuwa hana jipya la kuliambia taifa hili lenye kiu ya maendeleo endelevu!

  kinachotokea wanatafuta issue ya kutushugulisha ili wasipate tena kazi ya kuzunguka nchi nzima kuelezea uzuri wa bajeti kama yaliyowakuta mwaka jana. kwa maana nyingine hili la uchawi bungeni ni kujaribu kutuzuga na sisi tumestuka.... hatuzugiki!
   
 20. M

  Mama JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hivi report ya EPA, report ya kamati ya madini na ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati ya mwakyembe vinawasilishwa katika kikao hiki cha bunge wandugu?
   
Loading...