Kambi ya Lowassa kazini: Askofu Laizer aunga mkono Lema kuondolewa Arusha!

Askofu kavimbiwa sadaka! wanaarusha mlio waumini wake badilisheni jinsi ya kutoa sadaka, nawashauri zipelekeni zinakohitajika, huyo inawezekana ni shetani amejihuzulisha mbele za wana wa MUNGU. Simuheshimu tena huyo anayedaiwa kuwa askofu "laizer"
 
Laizer ni kipofu tu, yeye si ndio alikuwa anamfagilia babu Mwasapile? Hana chochote huyu askofu.
 
...alikunywa mvinyo kabla ya kupanda kwenye mimbari. Angeficha mahaba yake kwanza. Amekurupuka kama kurugenzi flani hivi.

hawa watu wanaotegemea kula kwa sadaka za waumini(japokuwa wengine ni wafanyabiashara haramu) itafika hatua watajikuta wako peke yao kanisani kwa kushabikia uovu unaofanyika. Ndo maana mao alifuta dini nchini kwake kwa kukwepa wajinga kama hawa.
 
Askofu atapasuka matumbo shauri yake, hajasoma juu ya vipande 30 alivyopewa Yuda Iskariote?
 
Hana maono yoyote! Au tuseme maono yake ya kishetani! Si mnakumbuka alivyokuwa mbele kusupport kikombe? Viongozi vipofu!
 
Cheki nayeye kalikoroga! Anafikiri Hao wakristo wake ni MAMBUZI. Sintakaa ni muamini tena na ndio askofu wangu huyu ***** kama kweli anatabasamu kwa EL.!
 
Lowassa ameteka sana viongozi wa kanisa la kilutheri nasikia akiwa kanisani kwake anapiga hata siasa ya chama chake! Na waumini hubaki kukodoa macho tu!
 
Wana jf nilisha waambia mahakama kuu kuliko zote ni UMMA. Nafikiri hili linadhihirika pale nae Laizer alipoona hukumu ya jaji ni sawa na raia wote uwanja wa miguu wakatengeneza 'vetical eleven' kwa nyusozao. Huku wengine wakisema Lowasa amesha maliza hata huyu. # my take= naposema kitu mnielewe jamani! watu weeengi(UMMA) ndio mahakama kuu. kama huamini hii mahakama ndio yenye uamuzi yajuu kulikozote, nenda sokokuu ARUSHA jifanye unanunua hata nyanya halafu sema 'lema nae kazidi' kama ni mmoja kakusikia atakuonya. kamani wengi wamekusikia watakupaka nyanya hadi uwe mwe.kunduuuu!
 
anapingana hata na watu ambao ndio wapigakura na ndio waliomchagua Lema. ndio maana wakaguna baada ya kauli yake hiyo
halafu huyu askofu wala hakupiga kura yoyote, hana hata haki ya kuyasema mambo hayo
 
Kiby umejichanganya. Aliyesema haki inanyanganywa ni Askofu wa Kanisa Katoliki Lebule. Ila Laizer ndo anaunga hukumu ya Lema na kusisitiza kuwa hata kama watu hawapendi.
 
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati,
Thomas Laizer, ameunga mkono hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya kumpokonya
ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na kusema ni haki na ukweli mtupu.

Alisema hayo jana katika Ibada ya Umoja wa Madhehebu ya Kikristo, iliyofanyika kwenye
uwanja wa Shekhe Amri Abeid, huku kauli yake hiyo ikipokewa kwa miguno na minong’ono kutoka kwa waumini.

Akihutubia halaiki hiyo muda mfupi baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu, kuonya vyombo vya Dola na Mahakama nchini, kuacha kupoka haki za watu na kunyanyasa wananchi kwa kuwapiga, Laizer alisema anaunga mkono hukumu hiyo.

“Mimi sijawahi kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Lema, lakini niliwahi kusikia kuwa Lema alisema katika mikutano yake, kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi wa Malaigwanani, kama alisema hivyo kweli na anastahili hukumu,” alisema Askofu Laizer.

Kauli hiyo ilionesha kuchukiza waumini waliofurika katika ibada hiyo na kuguna na kutokea minong’ono mingi, kuashiria kutokubaliana naye.

“Hata kama ninayosema hamuyakubali, lakini huo ndio ukweli mtupu na anastahili hukumu, nafahamu wengi hamfurahii uamuzi wa Mahakama, lakini imetoa haki, hakuna kutupa lawama kwa Kikwete (Jakaya) wala Ridhiwani Kikwete,” alisisitiza Askofu Laizer, huku watu wakiguna.

Kauli ya Askofu Laizer ilikuja siku moja baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kumvua ubunge Lema ambaye Mahakama ilimkuta na hatia nane zikiwamo za matusi, kashfa na kejeli katika mikutano ya kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka juzi.

Askofu Lebulu, alisema hata wakati Yesu alipigwa makofi, wakati akisulubiwa na alipouliza sababu za kupigwa kwake, aliendelea kupigwa, hivyo hali hiyo inazidi kukithiri nchini kwa watu kupokwa haki zao za msingi.

“Ngoja ninukuu maneno ya Biblia, kuna sehemu inasema Yesu alipigwa makofi, akauliza sababu za kupigwa kwake, hapa nafananisha na leo watu wanapigwa makofi na mahakama zetu, Serikali na vyama vyao, jambo ambalo linapaswa kukemewa lisiendelee,” alisema.

Alimwomba Mungu kumsaidia ili asiropoke, kwa sababu katika miaka 35 ya utumishi wake, hajawahi kuropoka.

Alipomaliza hotuba hiyo kama Msemaji Mkuu wa Umoja huo, alishangiliwa na watu, huku wakipiga vigelegele na baadhi yao wakirukaruka kuashiria kuunga mkono hotuba yake.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi, alipokaribishwa kusalimia waumini, alisema lazima watu wafike mahali wajue, haki inastahili kutolewa kwa watu kuheshimu haki na kufahamu wajibu wako.

Alisema ni wajibu wa kila mtu kupata haki, ila haki hiyo itapatikana tu kwa mtu kuheshimu wajibu wake
 
huyu askofu laiza si ndo alishadadia babu wa loliondo? Na wasiwasi nae nadhani atakua ameshakula hela ya harambee ndo mana
 
Yeye mwenyewe anaunga mkono mafisadi mnategemea aseme nini? ndio maana mimi kwenye masuala ya imani nanijua mwenyewe na Mungu wangu..
 
Yep Laizer ndie aliyemshadadia sana babu wa Loliondo,askofu na uganga wa kienyeji wapi na wapi?anasema eti aliwahi kusikia Lema ametukana,kweli kazi ipo,anawachoresha tu walutheri wote nchini!
 
Yep Laizer ndie aliyemshadadia sana babu wa Loliondo,askofu na uganga wa kienyeji wapi na wapi?anasema eti aliwahi kusikia Lema ametukana,kweli kazi ipo,anawachoresha tu walutheri wote nchini!
Acha kumuongelea vibaya kiongozi wa dini. Hujui kuwa yeye ni Mungu wa duniani?
 
Back
Top Bottom