Kambi ya Lowassa kazini: Askofu Laizer aunga mkono Lema kuondolewa Arusha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kambi ya Lowassa kazini: Askofu Laizer aunga mkono Lema kuondolewa Arusha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Apr 6, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Askofu laizer ni mshirika wa karibu wa Edward Lowassa. katika ibada kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid ameunga mkono uamuzi wa mahakama kumuengua lema katika ubunge huku waumini wakiguna kuonyesha hawakubaliani naye. Soma hii katika habari leo

  Askofu aikubali hukumu ya Lema

  Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha

  ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati,
  Thomas Laizer, ameunga mkono hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya kumpokonya
  ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na kusema ni haki na ukweli mtupu.

  Alisema hayo jana katika Ibada ya Umoja wa Madhehebu ya Kikristo, iliyofanyika kwenye
  uwanja wa Shekhe Amri Abeid, huku kauli yake hiyo ikipokewa kwa miguno na minong'ono kutoka kwa waumini.

  Akihutubia halaiki hiyo muda mfupi baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu, kuonya vyombo vya Dola na Mahakama nchini, kuacha kupoka haki za watu na kunyanyasa wananchi kwa kuwapiga, Laizer alisema anaunga mkono hukumu hiyo.

  "Mimi sijawahi kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Lema, lakini niliwahi kusikia kuwa Lema alisema katika mikutano yake, kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi wa Malaigwanani, kama alisema hivyo kweli na anastahili hukumu," alisema Askofu Laizer.

  Kauli hiyo ilionesha kuchukiza waumini waliofurika katika ibada hiyo na kuguna na kutokea minong'ono mingi, kuashiria kutokubaliana naye.

  "Hata kama ninayosema hamuyakubali, lakini huo ndio ukweli mtupu na anastahili hukumu, nafahamu wengi hamfurahii uamuzi wa Mahakama, lakini imetoa haki, hakuna kutupa lawama kwa Kikwete (Jakaya) wala Ridhiwani Kikwete," alisisitiza Askofu Laizer, huku watu wakiguna.

  Kauli ya Askofu Laizer ilikuja siku moja baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kumvua ubunge Lema ambaye Mahakama ilimkuta na hatia nane zikiwamo za matusi, kashfa na kejeli katika mikutano ya kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka juzi

  Askofu Lebulu, alisema hata wakati Yesu alipigwa makofi, wakati akisulubiwa na alipouliza sababu za kupigwa kwake, aliendelea kupigwa, hivyo hali hiyo inazidi kukithiri nchini kwa watu kupokwa haki zao za msingi.

  "Ngoja ninukuu maneno ya Biblia, kuna sehemu inasema Yesu alipigwa makofi, akauliza sababu za kupigwa kwake, hapa nafananisha na leo watu wanapigwa makofi na mahakama zetu, Serikali na vyama vyao, jambo ambalo linapaswa kukemewa lisiendelee," alisema.

  Alimwomba Mungu kumsaidia ili asiropoke, kwa sababu katika miaka 35 ya utumishi wake, hajawahi kuropoka.

  Alipomaliza hotuba hiyo kama Msemaji Mkuu wa Umoja huo, alishangiliwa na watu, huku wakipiga vigelegele na baadhi yao wakirukaruka kuashiria kuunga mkono hotuba yake.

  Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi, alipokaribishwa kusalimia waumini, alisema lazima watu wafike mahali wajue, haki inastahili kutolewa kwa watu kuheshimu haki na kufahamu wajibu wako.

  Alisema ni wajibu wa kila mtu kupata haki, ila haki hiyo itapatikana tu kwa mtu kuheshimu wajibu wake serikalini na katika familia, kisha unaweza kudai haki kwa wengine.

  MY TAKE: Hiyo ni dalili ya wazi ya watu kuendelea kumkubali Lema na jinsi maswahiba wa Lowassa wanavyoanza harakati zao kila kona
   
 2. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...alikunywa mvinyo kabla ya kupanda kwenye mimbari. Angeficha mahaba yake kwanza. Amekurupuka kama kurugenzi flani hivi.
   
 3. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  nadhani azabu ya kumzomea ilimstahili askofu huyu
   
 4. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  askofu huyu naye keshapewa fungu lake
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  anapingana hata na watu ambao ndio wapigakura na ndio waliomchagua Lema. ndio maana wakaguna baada ya kauli yake hiyo
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  ile kurugenzi imeshapoteza hadhi yake
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Si vyema kumkebehi askofu kwa kuwa ana miono kutoka mbinguni, heshimuni viongozi wa dini tusije pata matatizo katika taifa letu.
   
 8. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  askofu huyu aliunga mkono kikombe cha babu!
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  maaskofu wana elimu gani hivi?
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Inategemeana ni Askofu wa dhehebu gani!
  Kuna maaskofu ambao hawajamaliza hata LY, lakini pia wapo wa hadi Doctorate na Profs!
  Huyu Pro-EL wa leo ni msomi mzuri tu!
   
 11. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...teheeeeeeee!! Na kikombe kilitoka kwa nani vileeee....
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Askofu Laizer atagawa kanisa lake!
   
 13. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huyu si ndiye aliyemsupport babu wa Loliondo? Sishangai kwa kusema hili,
   
 14. T

  Topical JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Aisee mbona anachokisema hakifanani na msomi wa darasa la pili?
   
 15. k

  kahaluaJr Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ni Askofu njaa mie ni Mlutheri lakini kama ningekuwepo ningeguna sana tu mapaka hata ningetolewa hapo mahali tatizo njaaa Askofu acha njaaaa achana na siasa utahukumiwa vibaya sana
   
 16. kekuwetu

  kekuwetu JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 327
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  huyo ni askofu wangu, nilisikia ana undungu na Batilda, simshangai anapofungua domo lake hovyo yupo hovyo kwenye kuropoka lakini anapofundisha neno ndio 0 kabisa mahubiri yake yanawalaza wengi kanisani hajui kufundisha neno kabisa, sijui kwa nini asiingie kwenye siasa aumbuke kama sioi, kuna haja aombewe sala ya toba. sielewi ni sifa zipi zilimfanya akawa askofu, huyo amejichagua tu
   
 17. S

  SI unit JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Aangalie sana na asicheze na vichwa vya watu. Wanaweza kugoma kutoa sadaka kwa sababu ya *** wake.
   
 18. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati,
  Thomas Laizer, ameunga mkono hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya kumpokonya
  ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na kusema ni haki na ukweli mtupu.

  Alisema hayo jana katika Ibada ya Umoja wa Madhehebu ya Kikristo, iliyofanyika kwenye
  uwanja wa Shekhe Amri Abeid, huku kauli yake hiyo ikipokewa kwa miguno na minong'ono kutoka kwa waumini.

  Akihutubia halaiki hiyo muda mfupi baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu, kuonya vyombo vya Dola na Mahakama nchini, kuacha kupoka haki za watu na kunyanyasa wananchi kwa kuwapiga, Laizer alisema anaunga mkono hukumu hiyo.

  "Mimi sijawahi kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Lema, lakini niliwahi kusikia kuwa Lema alisema katika mikutano yake, kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi wa Malaigwanani, kama alisema hivyo kweli na anastahili hukumu," alisema Askofu Laizer.

  Kauli hiyo ilionesha kuchukiza waumini waliofurika katika ibada hiyo na kuguna na kutokea minong'ono mingi, kuashiria kutokubaliana naye.

  "Hata kama ninayosema hamuyakubali, lakini huo ndio ukweli mtupu na anastahili hukumu, nafahamu wengi hamfurahii uamuzi wa Mahakama, lakini imetoa haki, hakuna kutupa lawama kwa Kikwete (Jakaya) wala Ridhiwani Kikwete," alisisitiza Askofu Laizer, huku watu wakiguna.

  Kauli ya Askofu Laizer ilikuja siku moja baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kumvua ubunge Lema ambaye Mahakama ilimkuta na hatia nane zikiwamo za matusi, kashfa na kejeli katika mikutano ya kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka juzi.

  Askofu Lebulu, alisema hata wakati Yesu alipigwa makofi, wakati akisulubiwa na alipouliza sababu za kupigwa kwake, aliendelea kupigwa, hivyo hali hiyo inazidi kukithiri nchini kwa watu kupokwa haki zao za msingi.

  "Ngoja ninukuu maneno ya Biblia, kuna sehemu inasema Yesu alipigwa makofi, akauliza sababu za kupigwa kwake, hapa nafananisha na leo watu wanapigwa makofi na mahakama zetu, Serikali na vyama vyao, jambo ambalo linapaswa kukemewa lisiendelee," alisema.

  Alimwomba Mungu kumsaidia ili asiropoke, kwa sababu katika miaka 35 ya utumishi wake, hajawahi kuropoka.

  Alipomaliza hotuba hiyo kama Msemaji Mkuu wa Umoja huo, alishangiliwa na watu, huku wakipiga vigelegele na baadhi yao wakirukaruka kuashiria kuunga mkono hotuba yake.

  Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Raymond Mushi, alipokaribishwa kusalimia waumini, alisema lazima watu wafike mahali wajue, haki inastahili kutolewa kwa watu kuheshimu haki na kufahamu wajibu wako.

  Alisema ni wajibu wa kila mtu kupata haki, ila haki hiyo itapatikana tu kwa mtu kuheshimu wajibu wake serikalini na katika familia, kisha unaweza kudai haki kwa wengine.

  HabariLeo | Askofu aikubali hukumu ya Lema
   
 19. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Msipotoa sadaka hamtaiona mbingu tena msithubutu maana sadaka ni kwa faida yenu wenyewe
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  hotuba ya Askofu inaonyesha kujikanganya mwenyewe hapo aliposema ni haki Lema kupewa ile hukumu huku akisema serikali na dola yake imekuwa ikiwanyanganya watu wake haki alipofananishi Bwana Yesu kupigwa makofi. Hii ni kauli na tabia ya mtu mwenye kula chakuna na mikono yote miwili, tena bila hata kunawa. Rushwa aliyoimwaga EL makanisani imewapofusha kabisa baadhi ya viongozi na sasa hawasikii hawaambiliki na wata hawajijui.
  Uchaguzi uitishwe Arusha halafu raia tutamwonyesha Laizer jinsi maamuzi ya wengi yanavyopaswa kuheshimiwa na haki ya wachache hasa pale inapodhulumu haki ya wengi isivyopaswa kupewa kipaumbele.
  .
   
Loading...