Mikael,
Kwa mfumo tulio nao sasa, wananchi wanaisimamia serikali kupitia kwa wawakilishi wao, yaani wabunge. Kamati za bunge zinafanya kazi kwa niaba ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuidhinisha mapato na matumizi ya fedha, na kukagua mwenendo wa matumizi hayo.
Alichokifanya spika (kuvunja kamati inayosimamia mashirika ya umma), ni kunyang'anya wananchi mamlaka ya kuisimamia serikali kupitia bunge. Huu ni uhaini. Hili ni moja.
Pili, maamuzi haya ya spika - ya kupora mamlaka toka kwa wananchi - yamekuja sambamba na hoja iliyowasilishwa na serikali ya kunyang'nganya (tena) watanzania - kupitia kwa wabunge wao - mamlaka ya kupokea na kuchambua taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali!
Nini tafrisiri yake?
Serikali haitaki kabisa 'usumbufu'. Hawataki kuulizwa wala kufuatiliwa kwenye utendaji wake ikiwa ni pamoja na kukaguliwa kwa matumizi ya kodi ya watanzania. Kwa sasa watanzania kujua matumizi ya kodi yao itakuwa ni 'fadhila' toka kwa rais.
Na huu ni mkakati wa kamati mpya wa kamati ya CCM chini ya Mangula, Kinana na Dr Asha Migiro, wa kuondoa 'transparency' kwenye governance system Tanzania. Kelele tulizozikia kule Addis Ababa, kwamba Tanzania imefanya vizuri kwenye utawala bora, ilikuwa ni ujenzi wa uzio ili wakifanya huu uharamia dunia isijue! Na hapa ndipo watanzania wanatakiwa kuwa macho zaidi.
lli kuokoa hii nchi na balaa linaloinyemelea basi 2015 ni vema bunge lisiwe dominated tena na wale wale walioruhusu 'uporwaji' huu wa haki ya wananchi kuisimamia serikali.
Kuhusu bunge
Kwa sasa hivi Tanzania hatuna bunge. hatuna! Tuna idara ya serikali inayokaa Dodoma -mara kadhaa kwa mwaka- ambapo wabunge toka vyama vingine wanaruhusiwa kuingia lakini kuongea inategemea mkalia kiti kaamka vipi siku hiyo. Hatuna bunge. Na kama kuna mtu amerudisha hii nchi nyuma, basi Makinda anaongoza. Makinda atakumbukwa kwa kuuwa Demokrasia Tanzania. Hili halina ubishi. Na huko tunakokwenda, ni mungu mwenyewe anaweza kuinusuru hii nchi na mabalaa yanayopaliliwa na huyu mama. Very unfortunate.
kama ni ukweli basi hakuna haja ya kuwa na bunge,sababu ni ipi ya kufuta kamati ya hesabu za mashirika ya umma?
Na yale mabilioni yaliyopo Uswiss na kwingineko nayo YAMEFUTWA?
Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, iliyokua inaongozwa na Edward Lowassa imevunjwa na kuundwa kamati mbili ya Ulinzi na Usalama na ingine ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma ya Zitto Kabwe, imefutwa kabisa.
Zaidi baadae
Ninadhani hii transparency wanayoificha, kuna kitu wanataka kukifanya ninahisi wanataka kuchota pesa za kampeni toka kwenye Mashirika ya umma kama NSSF, LAPF, GEPF,PSPF, PPF na NHIF!! ili wasije kuulizwa peso hiyo imekwenda wapi!! Watch out Tanzanians!!Mikael,
Kwa mfumo tulio nao sasa, wananchi wanaisimamia serikali kupitia kwa wawakilishi wao, yaani wabunge. Kamati za bunge zinafanya kazi kwa niaba ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuidhinisha mapato na matumizi ya fedha, na kukagua mwenendo wa matumizi hayo.
Alichokifanya spika (kuvunja kamati inayosimamia mashirika ya umma), ni kunyang'anya wananchi mamlaka ya kuisimamia serikali kupitia bunge. Huu ni uhaini. Hili ni moja.
Pili, maamuzi haya ya spika - ya kupora mamlaka toka kwa wananchi - yamekuja sambamba na hoja iliyowasilishwa na serikali ya kunyang'nganya (tena) watanzania - kupitia kwa wabunge wao - mamlaka ya kupokea na kuchambua taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali!
Nini tafrisiri yake?
Serikali haitaki kabisa 'usumbufu'. Hawataki kuulizwa wala kufuatiliwa kwenye utendaji wake ikiwa ni pamoja na kukaguliwa kwa matumizi ya kodi ya watanzania. Kwa sasa watanzania kujua matumizi ya kodi yao itakuwa ni 'fadhila' toka kwa rais.
Na huu ni mkakati wa kamati mpya wa kamati ya CCM chini ya Mangula, Kinana na Dr Asha Migiro, wa kuondoa 'transparency' kwenye governance system Tanzania. Kelele tulizozikia kule Addis Ababa, kwamba Tanzania imefanya vizuri kwenye utawala bora, ilikuwa ni ujenzi wa uzio ili wakifanya huu uharamia dunia isijue! Na hapa ndipo watanzania wanatakiwa kuwa macho zaidi.
lli kuokoa hii nchi na balaa linaloinyemelea basi 2015 ni vema bunge lisiwe dominated tena na wale wale walioruhusu 'uporwaji' huu wa haki ya wananchi kuisimamia serikali.
Kuhusu bunge
Kwa sasa hivi Tanzania hatuna bunge. hatuna! Tuna idara ya serikali inayokaa Dodoma -mara kadhaa kwa mwaka- ambapo wabunge toka vyama vingine wanaruhusiwa kuingia lakini kuongea inategemea mkalia kiti kaamka vipi siku hiyo. Hatuna bunge. Na kama kuna mtu amerudisha hii nchi nyuma, basi Makinda anaongoza. Makinda atakumbukwa kwa kuuwa Demokrasia Tanzania. Hili halina ubishi. Na huko tunakokwenda, ni mungu mwenyewe anaweza kuinusuru hii nchi na mabalaa yanayopaliliwa na huyu mama. Very unfortunate.
Je, huyu ndiye atakayeongoza hiyo kamati mpya ya bajeti:
![]()
"Mwenyekiti wa kamati Mahsusi iliyoundwa na Mhe Spika kuishauri serikali namna ya kuongeza uwigo wa mapato Mhe. Andrew Chenge akimkabidhi Spika wa Bunge Anne Makinda ripoti yao. Kamati hiyo iliundwa na Mheshimiwa Spika kwa lengo ka kuaandaa Mapendekezo ya kuishauri serikali kuhusu kuainisha vyanzo mbalimbali vya Mapato ndani ya serikali yaliyo ya kodi na yasiyo ya kodi" - H@ki Ngowi: Taswira Kutoka Ofisi za Bunge:Spika Anne Makinda apokea ripoti ya Mapendekezo kuhusu Mapato na Matumizi ya Serikali Leo
Zitto atapata wapi jukwaa la kueneza uongo wake
Mkuu nifafanulie kama una ufahamu.
Spika ndiye mwenye mamlaka ya kuunda na kufuta kamati?
If so, ni sheria ipi inayompa hayo mamlaka?
Hayo mamlaka anayafanya at her own discretion au anashirikiana na watu wengine?