Kamati za bunge zifutwe!

Kamati za bunge zifutwe!

hizi kamati zitaendelea kutokuwa na meno mpaka wakati ambapo bunge litakuwa si la chama kimoja kama ilivyo kwa sasa
 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakipuuzwa mno.Hawathaminiwi.Hawasikilizwi.

Mifano ipo mingi...
Rejea mjadala wa Richmond, Jairo, Ekerege, Kiwira, Ushahidi wa Lema, na juzi tu Mawaziri wezi wa nchi hii.

Wabunge hawana la maana katika ujenzi wa Taifa hili? Kwanini wanapuuzwa?

Kama kila njia inashindikana,Wabunge wawe wa kwanza kujiuzulu...
 
Comrade ukiingiliwa na Nyoka ndani ya Nyumba kumkimbia sio Suruhisho dawa ni Kupambana nae humohumo ndani ili kufanikisha kumuua wabunge wapambane mulemule ndani sisi waamuzi huku nje tunaona na tutajua nani ni mshindi kwa hili la Bunge la Saba wananchi wote tumeona na tumesikia,
 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakipuuzwa mno.Hawathaminiwi.Hawasikilizwi.Mifano ipo mingi.Rejea mjadala wa Richmond,Jairo,Ekerege,Kiwira,Ushahidi wa Lema,na juzi tu Mawaziri wezi wa nchi hii.Wabunge hawana la maana katika ujenzi wa Taifa hili? Kwanini wanapuuzwa?

Kama kila njia inashindikana,Wabunge wawe wa kwanza kujiuzulu...

HIli wazo lako ni zuri, ila lingekuwa zuri zaidi kama wale walio wazalendo nadni ya CCM wangejiuzulu wao ili tuongeze ukubwa wa kambi ya upinzani, kwani CCM wanautumia wingi wao vibaya katika kuiwajibisha serikali. Kama uwiano ungekuwa 50-50, mambo yangekuwa yanaenda kama wengi watakavyotaka
 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakipuuzwa mno.Hawathaminiwi.Hawasikilizwi.Mifano ipo mingi.Rejea mjadala wa Richmond,Jairo,Ekerege,Kiwira,Ushahidi wa Lema,na juzi tu Mawaziri wezi wa nchi hii.Wabunge hawana la maana katika ujenzi wa Taifa hili? Kwanini wanapuuzwa?

Kama kila njia inashindikana,Wabunge wawe wa kwanza kujiuzulu...

Naunga mkono hoja hii!

Unajua nawaza mbinu nzuri ya kuleta mabadiliko dhidi ya matatizo haya, nafika mahali napata hasira ya kutukana. Inatakiwa litokee tukio kama la kusabotage! Natafakari mbinu ya kuwamobilize hawa wabunge, au wananchi na kuleta wito mmoja - Mtwara mpaka Kagera, Dsm mpaka Kigoma, kwa mara moja tukajikuta tuko Ikulu, au bungeni, au kwenye viwanja vile vilivyotumika siku ya Uhuru, ambavyo viko katika kila mkoa...............
 
Kweli inasikitisha sana, hakuna la maana wanalofanya bungeni zaidi ya kupiga kelele zisizo na maana. Ifike wakati sasa waoneshe kuwa wapo kwa maslahi ya taifa, waanze kwa kujiuzulu wenyewe na namna nzuri ya kutekeleza hilo ni KUPIGA KURA YA KUTOKUA NA IMANI NA RAIS ili uitishwe uchaguzi mwingine. Nafikiri hilo litakua fundisho kwa RAIS atakaekuja ili ajue kuwa wabunge wapo kwa ajili ya kuisimamia serikali.
 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakipuuzwa mno.Hawathaminiwi.Hawasikilizwi.Mifano ipo mingi.Rejea mjadala wa Richmond,Jairo,Ekerege,Kiwira,Ushahidi wa Lema,na juzi tu Mawaziri wezi wa nchi hii.Wabunge hawana la maana katika ujenzi wa Taifa hili? Kwanini wanapuuzwa?

Kama kila njia inashindikana,Wabunge wawe wa kwanza kujiuzulu...

Mkuu wabunge wenyewe hasa magamba ndo wanapendwa kupuuzwa na kufanywa kama watoto. Tumeona mara ngapi huwa wanaitwa na kuonywa kwenye vikao vyao vya vyama kama walikuwa wanaibana serikali yao bungeni?
So, forget about that thing broda.
 
Hata wa upinzani hupuuzwa pia..
 
Kwa taarifafa yako kuanzia Rais mpaka wabunge wengi wa CCM hawakuingia madarakani kihalali hivyo wao wako pale kwa fedha zao ama kwa kutumia dola, sasa wewe unataka watetee wananchi kwa mpango upi. Umeumia, waambie na wenzako aidha tufanye mapinduzi sasa ama mkae mtulie mpaka mwaka 2015.
 
Vipi tunawezi tukaungana ili tufanye hayo mapindizi?. Teh teh
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
That would set a good precedent lakini sio kwa hawa wachumia matumbo
 
Comrade ukiingiliwa na Nyoka ndani ya Nyumba kumkimbia sio Suruhisho dawa ni Kupambana nae humohumo ndani ili kufanikisha kumuua wabunge wapambane mulemule ndani sisi waamuzi huku nje tunaona na tutajua nani ni mshindi kwa hili la Bunge la Saba wananchi wote tumeona na tumesikia,

Mkuu I concur with you 100%. Nami naomba nimuulize; hivi nyani au nguruwe pori akivamia shamba dawa yake ni kukimbia na kulitelekeza shamba? Atamaliza mahindi asivyo na aibu wala soni. Dawa ni kumtandika mishale ukiwa humo humo shambani.

Ila kama na wewe utashirikiana na nguruwe wakati yeye akila wewe unaiba ili baadaye usingizie ni nguruwe alikula hapo utakuwa hutufai - unastahili mishale zaidi ya nguruwe. Bungeni kuna wachache wa aina hii lakini sio wote.
 
Kwa taarifafa yako kuanzia Rais mpaka wabunge wengi wa CCM hawakuingia madarakani kihalali hivyo wao wako pale kwa fedha zao ama kwa kutumia dola, sasa wewe unataka watetee wananchi kwa mpango upi. Umeumia, waambie na wenzako aidha tufanye mapinduzi sasa ama mkae mtulie mpaka mwaka 2015.

Wabunge wa CCM wametanguliza masilahi binafsi. Hivyo, ni waoga kwa viongozi wao Chama chao.
Waliowapigia kura ndio wametufikisha hapa.
 
Kwa nini tunawabebesha mzigo huo wote wabunge wetu?? sisi wananchi ambao ndio tunaumia direct na ufisadi na wizi wa hawa mawaziri tumechukua hatua gani? tunapigia kelele kwenye keyboads zetu na upepo ukipata tuanaufyata! Tulitakiwa tumeshatoka mabarabarani na kuandama kutaka serikali iondoke tukitaka kumuondoa Rais ni kuamua tu! Misri wameweza, Tunisia, Libya sisi je?? Kelele na porojo tu kama akina Zambi na wenzie??
 
Nawasalim kwanguvu ya umma,Jamani ktk kujaribu kuona jinsi watu wanaojiita
wapigania haki za wananchi na wana uchungu wanchi kifupi hawa wanaoitwa
wabunge pale wanavyokuwa majukwaani wakitokwa namisuli yashingo kujifanya
wanatetea wananchi, swali nikwamba hivi ingekuwaje kama kweli kila anaepiga
kampeni kwanguvu vile anamaanisha kuwatoa wananchi ktk bora maisha na sio
maisha bora kwa kila mtz kungekuwa na sera mpya kweli kwa wanaogombea?
na je matatizo yangekwepo hasa haya ambayo wazi hata yasiyohitaji darasa ambayo
hawa jamaaa gamba wanasema sio issue kwao? ni mtazamo tu hoja tafadhali.
 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakipuuzwa mno.Hawathaminiwi.Hawasikilizwi.

Mifano ipo mingi...
Rejea mjadala wa Richmond, Jairo, Ekerege, Kiwira, Ushahidi wa Lema, na juzi tu Mawaziri wezi wa nchi hii.

Wabunge hawana la maana katika ujenzi wa Taifa hili? Kwanini wanapuuzwa?

Kama kila njia inashindikana,Wabunge wawe wa kwanza kujiuzulu...

% kubwa ya wabunge waliopo mjengoni wapo kimaslahi binafsi, as long hiyo mijadala haiwagusi wao moja kwa moja si sababu ya wao kujihudhuru. Ni wakati muafaka sasa wa wananchi kuwabana pindi watakapo rudi majimboni watueleze ni kwa vipi wameshindwa kuiwajibisha serikali. wale party oriented MP's watimuliwe!
 
wabunge hawana tatizo na wa kulaumiwa ni sisi ,sisi watanzania ndio tumepeleka idadi ndogo ya wabunge kule mjengoni na haya ndio matunda yetu...box la kura
 
Back
Top Bottom